Lowassa afunika dar

JK anawasiwasi kwamba akimrejesha jamaa anaweza kumgeuzia kibao.
PM anakuwepo kwa mujibu wa sharia labda akubaliane na fitna za akina Membe again...ila kwa sasa kama nchi tunamuhitaji Lowassa, ukiangalia kwa makini karibu kila wizara na idara zimeparalise... serikali iko likizo, PM PINDA hajui alifanyalo...
 
Kwa wenye akili ya senene lazima watasifia sana huyu Mwizi.
 
Ndo ivyo makamanda wenzangu.Sisi tuko bize na mabishano,mwenzetu anapita njia za panya.Jamaa kajipanga,yani hatanii amedhamilia kushika MADARAKA.Ameshajua udhaifu wa watanzania,sasa ndo anatumia vizur fulsa.MBOWE,SLAA,na makamanda wengine take care.DISCO LIMEINGIWA NA MMASAI.
 
Akigombea Lowasa 2015 ntahakikisha Mimi na rafiki zangu wapatao 100 tunampigia kura za Ndiyoooo
 

Tatizo la nyerere alikua na wivu wa maendeleo... alipenda watz 2we masikini daima.
 
Nakubaliana na wewe ila kwa mujibu wako unaonekana unasema hakuna solution nchini. Mimi bado naamini kwamba mtu asiye rafiki wa hawa watu anaweza kuvunja mitandao yao. Kwa CCM ni Mwakyembe tu. Kina Dr. Slaa wanaweza maana wameonesha nia toka wako Bungeni, sasa sijui kwa nini sasa hivi tu doubt nia yao.

Lowassa ni mwizi tu. Anachokifanya ni kutafuta watu wepesi (cheap Tanzanians) kama boda boda...afu anasema boda boda oyeee! hivi katika karne hii unaweza kumwambia kijana wako kwamba bodaboda oyee??? kwamba tutafanya harambee hili kuongeza bodaboda? hii si sawa sawa na kuwambia wanafunzi kwamba tutaleta div. 5 hili kila mmoja ashinde ifikapo 2015? Huyu anaonga watu kwa njia ya kisasa. Anacheza na mawazo yao kwa sababu watu wenyewe hawajitambui. Dawa ya umaskini sio kumugawia kila mtu hela au gari au nyumba. Hili si tatizo letu Tanzania. Tatizo ni kwamba watu wachache, akiwemo yeye Lowassa, wanaliibia taifa na hivyo tunakosa maisha bora, yaani shule za kuandaa vijana kujitegemea, hospitali safi, barabara na matokeo yake tunakuwa na jamii ilojaa div.5 au madreva wa bodaboda...ambao Lowassa anawapenda (kwa mujibu wake). Huu ni ujinga at its best. Lowassa anatoa rushwa kwa watu cheap.

Nakuhakikishia watanzania mkifanya mistake, Lowassa atawafanya mumuone Kikwete kama geneous. Mkataeni haraka.
Nahisi anapoteza fahamu akiwa anaongea...angalieni video yake (bodaboda). Huyu mtu anahararisha umaskini.
 

Mkuu umemaliza kila kitu na sioni cha kuongeza!
Watanzania tu wavivu wa kufikiri na wasahaulifu wa kutupwa! Haiingii akilini kumshabikia mhalifu ambaye katika nchi za watu walio 'serious' na maendeleo yao alipaswa kuhukumiwa kunyongwa kwa madhira aliyoliletea taifa hili.
Ni Lowassa huyuhuyu aliyelitumbukiza taifa kwenye tatizo kubwa la umeme linalolisumbua taifa na litakaloendelea kulisumbua kwa miango mingi ijayo wakati yeye, familia yake na rafiki zake wakiendelea kunawiri! Watanzania wanalalamikia kupandishwa kwa gharama za umeme huku wakimshabikia 'mchawi' aliyesababisha madhira yote hayo! Lowassa na genge lake bado wanaendelea kupata migawo ya rushwa toka makampuni yaliyohusika na rushwa, na ni huyuhuyu; genge lake wakiwemo vibakauchumi mapapa walioko ndani ya chama lao la CCM walionunua pia hisa kwenye makampuni mbalimbali yakiwemo ya mawasiliano na kupata mgawo mkubwa huku wakiwakingia kifua wasilipe kodi! Wakati wenzetu jirani makampuni ya mawasiliano ndiyo yameshika usukani katika uchangiaji wa pato la taifa sisi huku hayamo hata katika ishirini bora! Yanapitwa hata na makampuni ya ulinzi kama Group 4!
Si kwamba hawalipi, ila wanagawana kodi yetu na wahalifu hawa.
Watanzania ni nani aliyeturoga?
Kwa ushabiki wa kijinga namna hii ipo siku nchi itaangukia mikononi kwa majambazi kama hili ambalo sehemu salama kwake ni Segerea, Ubena na magereza kama hayo.
Ushabiki umewahi kuiletea dunia matatizo yaliyoacha makovu yanayoonekana hadi leo kama pale kwa ushabiki wajerumani walipomweka Adolf Hitler kuwa kiongozi wao! Kilichotokea nadhani wengi tu tunakielewa. Na sasa kwa ushabiki wa kijinga huu huu tunataka kuiingiza nchi mikononi mwa majambazi na wauaji wakubwa!
 
Last edited by a moderator:
we kwanza nani kakupa ruhusa yakuchngia yasiyo kuhusu,manake we ni muahamiaji haramu,ile operation kimbunga bado haijakufikia,mambo ya nchi yetu tuachie sis watanzania tuamuwe,nenden kwanza mkasuluhishe ugomvi wenu na alshabab

mkuu tumia ubongo kufikiri. Huyu jamaa nyerere alimkataa, iweje leo mnashabikia?
Pia ujitambue kuwa mambo operation kimbunga si yakutolea mifano, maana imeacha sifa mbaya kwa viongozi
 

sasa unalia liaa nn,manake hata familia yenu inamkubali lowassa,sema tu ww ndo umekuwa kicnwa ngumu,lakin hatushangai,manake ili jamii itwe jamii lazma watu kama ww wawepo
 
Msaliti huyo hafai kabisa anapenda sifa anauma anapuliza unakataa posho kumbe unavuta mkono wa pili huo si unafiki
 


Huyo ndiye Laigwanan Edward N. Lowassa.

Kusema kweli makundi ya vijana wanampenda. Ukipita vijiweni utasikia wakisema kwamba Lowassa ni jembe. Yeye na Magufuli ndio tegemeo la vijana wanaiunga mkono CCM na hata wasioiunga mkono.
 
Zito ni sawa na Mandela kwa kusimamia kile anachoamini. Mambo ya kusema usaliti hayana mashiko, mtu akipanga mkakati wa kutaka uongozi wa juu kidemokrasia anaitwa msaliti. Eti anataka kufanya mapinduzi! Mapinduzi ni ile hali ya kumwondoa mtu kwenye uongozi kabla ya muda lakini kama unapanga kuingia kwa njia ya kidemokrasia halafu unaita huo ni usaliti - Nadhani hicho kitu wanaweza kuelewa baadhi ya watu wa Kaskazini na misukule yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…