Hebu tuache sanaa za kitoto.
Baada ya utekelezaji wa ahadi za Magufuli kuwa na kasi ya jet hatimaye tumeanza kuona sanaa za kutaka kujinasua na sekeseke la kutumbuliwa majipu.
Wakati wa kampeni na mara baada ya kuapiswa Magufuli na serikali yake aliwataka wanaomiliki mashamba makubwa bila ya kuyaendeleza wayaendeleze kabla serikali haijayachukua.
Sasa kuna wasanii na wajanja wajanja wanataka kuhadaa umma kuwa wanayaendeleza mshamba hayo kwa kuchunga ngo'mbe.
Usanii wa namna hii hautawaondolea sifa ya kuwa majipu ya kutumbuliwa.
Lukuvi ataaangalia hati inatakutaka kuliendeleza vipi hilo shamba na kama umeshindwa litatwaliwa na kugaiwa kwa wananchi wasio na mashamba.