Lowasa kusomewa mashtaka mapya Zanzibar

Lowasa kusomewa mashtaka mapya Zanzibar

Afukuzwe tu kwani ana faida gani? Cha kushangaza wanaokuwa na hofu ni Kibanda na Kubenea ambao walikuwa wanufaika wa fedha za Fisadi Lowasa
Kichama mmaowaita mafisadi a.k.a magamba mlishindaa kuwacua magamba...leo hii mnaungana na waliowataja na kuwaambieni kuwa mna magamba lakini muxa wa kuchukia hatua mlibisha kila mlichoambiwa kihusu hawa mabwana wakubwa
 
Afukuzwe tu kwani ana faida gani? Cha kushangaza wanaokuwa na hofu ni Kibanda na Kubenea ambao walikuwa wanufaika wa fedha za Fisadi Lowasa

Kwanza timizeni ile ahadi ya kumvua gamba. Au siku 90 mlizowapa yeye na Chenge bado hazijatimia?
 
Hakuna wa kumgusa Lowassa , hao wakina Nape wanajishaua tu
 
Nimeshindwa kuweka link mwenye kuweza aende kwenye Twitter ya absolam kibanda kuna hii habari,vilevile kubenea kafichua njama za kumfukuza uanachana Lowasa.

kama kuweka link umeshindwa weka picha
 
Afukuzwe tu kwani ana faida gani? Cha kushangaza wanaokuwa na hofu ni Kibanda na Kubenea ambao walikuwa wanufaika wa fedha za Fisadi Lowasa

Laana ya kumpiga Mzee Warioba itatafuna Vizazi vyako vyote kama unavyo.
Btw, nasikia unataka kugombea ubunge ubungo,Mnyika utamuweza wewe lakini ?
 
afukuzwe kwa kosa lipi? acheni hofu Lowasa anaogopwa maana anawajuwa wapiga dili wote wanamjuwa muziki wake akipita ofisini watu hakutakalika
 
Mimi nawauliza wana ccm hivi ni EL peke yake tu ndiye aliyevunja makubaliano ya adhabu aliyopewa ? Nani asiyejua kuwa adhabu yote ilikuwa juu yake na imeonekana kuwa pamoja na vizuizi vyote ndugu huyu anaendelea kuchanja mbuga. Mimi nawashauri wanaCcm kuwa wasije kata tawi wililo kalia na kakupatikana madhala ushindi wa CCM 2015 ni EL piga ua kwanza ni mkristo halafu anakubalika kote japo ninyi kundi dogo hapo juu hamtaki likini habari ndiyo hiyo
 
hivi mbona lowasa anawasemaji wengi sana????? na wengine wapinzani hii ni hatari kubwa kwa mtu anayetaka kuwa kiongozi mkuu wa nchi
 
Mkakati wa kumfukuza Lowassa CCM waiva

Posted by:-Saed Kubenea-57 mins ago0 Comments-57 Views

MBUNGE wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa, aweza kuvuliwa uwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), muda wowote kutoka sasa.-Saed Kubenea, anaripoti.

Hoja ya kumvua uwanachama Lowassa imepangwa kuwasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu (CC), kinachotarajiwa kufanyika Jumanne wiki hii, mjini Zanzibar.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema, mkakati wa kumvua uwanachama Lowassa, unasukwa kwa ustadi mkubwa na baadhi ya viongozi wandamizi ndani ya CCM ili kumzua kutimiza ndoto yake ya kuwa rais.

“Ni lazima tumfukuze uwanachama katika chama chetu. Hakuna namna nyingine ya kukinusuru chama hiki,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama hicho.

Amesema, “Bwana huyu (Lowassa), amekuwa akikivuruga chama chetu kwa muda mrefu. Tumemvulia, lakini sasa tumechoka. Nilazima tumuondoe ili kukinusuru chama chetu.”

Ajenda ya kumfukuza Lowassa kutoka ndani ya chama hicho, imejificha katika kinachoitwa, “Tathmini hali ya kisasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.”

Lowassa alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika serikali ya Jakaya Kikwete. Anatajwa kuwa miongoni mwa makumi ya wanachama wa CCM waliotangaza au kutajwa, kusaka urais kwa udi na uvumba katika uchaguzi mkuu ujao.

Januari mwaka jana, Lowassa na makada wenzake kadhaa walipewa “onyo” kwa kile kilichoitwa, “kuanza kampeni kabla ya muda kufika.”

Mtoa taarifa wa gazeti hili anasema, kabla ya kikao cha CC, kutafanyika kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili na Nidhamu, ambacho kitafanya tathmini ya adhabu zilitolewa kwa Lowassa na wenzake.

Lowassa anatuhumiwa kuendelea na mkakati wake wa kampeni kwa kukusanya watu na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, jambo ambalo viongozi wake wakuu wanamtuhumu kukipasua chama chao.

Anasema, kikao cha CC kitatekeleza mradi huo kwa kutumia ripoti zilizotengenezwa na timu za maofisa usalama wa chama hicho, zilizotumwa mikoa yote ili kukusanya kile kilichoitwa, “mkakati wa Lowassa wa kusaka urais.”

Kutokana na hali hiyo, Kamati Kuu iliitaka Kamati ya Maadili kufanya marejeo na kuangalia utekelezaji wa adhabu kwa makada

Lowasa ana vuruga vipi chama? hao waoga tu acheni ngoma ichezwe.huyo lowasa ndo kiboko yao hana muda wa kumuweka mtu kipolo. supu ya mbwa inaliwa ikiwa bado ya moto.kiama cha wapiga dili kimewadia. hata onyo la mwaka jana kaonewa. pinda alitangaza nia ya kiwania ubwana mkubwa akiwa ughaibuni mbona hajaonywa na alitamkaga dhamira yake mwanza hakuonywa. hali kadhalika naibu katibu mkuu bara kamanda mwiguru mbona hajaonywa? Tunataka haki itendeke Lowasa akakataliwe kwa kura halmashauri kuu na siyo kjmfanyia uhuni. CCM inapita kwenye bonde la misukosuko na vigingi kibao kwa hivyo kuna mambo lukuki ambayo cc wanatakiwa kujadili kuliko kukaa na kudiscuss umbea. kwa mfano taathimini ya uchaguzi wa serikali za mitaa. jinsi ya kuhakikisha amani inatawala kwenye uchaguzi mwaka huu. namna gani watadhibiti rushwa kura za maoni na general election. uhusiano na wadau wa maendeleo. utekelezaji wa maazimio ya bunge kuhusu escrow scandal,utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wahoji kwanini tumeshindwa kupeleka meli mpya kule bukoba n.k badala ya kujadili mipasho.
 
hili jukwaa tamu sana.
1. akiwa anazungumziwa ZZK utaona wanaccm wanavyomtetea kwa nguvu zote.
2. akiwa anazungumziwa EL utaona wanaukawa wanavotunisha misuli kumtetea.

duh sielewi elewi vile!!
 
Nimeshindwa kuweka link mwenye kuweza aende kwenye Twitter ya absolam kibanda kuna hii habari,vilevile kubenea kafichua njama za kumfukuza uanachana Lowasa.
http://-----------online.com/mkakati-wa-kumfukuza-lowassa-ccm-waiva/
 
hili jukwaa tamu sana.
1. akiwa anazungumziwa ZZK utaona wanaccm wanavyomtetea kwa nguvu zote.
2. akiwa anazungumziwa EL utaona wanaukawa wanavotunisha misuli kumtetea.

duh sielewi elewi vile!!

Kama kawaida yetu mkuu! Ndio tulivo sisi
 
jamani Lowassa hata simpendi huyu jamaa vijana wanapiga bodax2 za kifisadi kwa mgongo wa lowassa njaa zitawaua mnaojiita TEAM LOWASSA

sipati hata senti ya lowassa lakn jamaa nampenda ni jembe shabikia ujinga sasa liwekwe limembe uone utakavyokaa mia mingne kumi bila raisi
 
Utabiri wa machafuko makuu katika chama cha mapinduzi yanaweza kutokea bila kujua chanzo chake na dunia ikashangaaaa !!!
 
Kikao Zanzibar kilifuta Azimio la Arusha na kuleta anguko la maadili CCM !
Kikao Zenj kumfukuza Lowasa ni anguko kwa CCM
 
Tunataka Rais atoke UKAWA lakini kama ni lazima Rais atoke CCM, kati ya wagombea wote wa CCM aheri Lowasa, angalao ana kauli na maamuzi ya kiuongozi. Membe hakuna tofauti na Kikwete, Mwigulu muuaji (huyu asubirie mashtaka), Pinda hata kwa nafasi ya uwaziri mkuu hakuna alichoweza kusimammia (hata hao nyuki anaotamka kila siku hakuna chochote), Kigwangala (hastahili hata kujadiliwa - totally hopeless), January hajaonesha uwezo wa kusimamia chochote. Lowasa, leadership commanding authority anayo.

Above all I know stands Dr. Wilbroad Slaa.
 
Back
Top Bottom