Lowasa kusomewa mashtaka mapya Zanzibar

Lowasa kusomewa mashtaka mapya Zanzibar

Chabruma umesahau boss wako Membe alivyomtesa kibanda kisa urais leo unasema ni kibaraka wa Lowassa? Membe anamchukia sana kibanda ameshindwa tu kumuua.
 
Habari ya lowasa
 

Attachments

  • 1421005455014.jpg
    1421005455014.jpg
    46.6 KB · Views: 3,032
  • 1421005500905.jpg
    1421005500905.jpg
    52.9 KB · Views: 519
Mkakati wa kumfukuza Lowassa CCM waiva

Posted by:-Saed Kubenea-57 mins ago0 Comments-57 Views

MBUNGE wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa, aweza kuvuliwa uwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), muda wowote kutoka sasa.-Saed Kubenea, anaripoti.

Hoja ya kumvua uwanachama Lowassa imepangwa kuwasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu (CC), kinachotarajiwa kufanyika Jumanne wiki hii, mjini Zanzibar.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema, mkakati wa kumvua uwanachama Lowassa, unasukwa kwa ustadi mkubwa na baadhi ya viongozi wandamizi ndani ya CCM ili kumzua kutimiza ndoto yake ya kuwa rais.

“Ni lazima tumfukuze uwanachama katika chama chetu. Hakuna namna nyingine ya kukinusuru chama hiki,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama hicho.

Amesema, “Bwana huyu (Lowassa), amekuwa akikivuruga chama chetu kwa muda mrefu. Tumemvulia, lakini sasa tumechoka. Nilazima tumuondoe ili kukinusuru chama chetu.”

Ajenda ya kumfukuza Lowassa kutoka ndani ya chama hicho, imejificha katika kinachoitwa, “Tathmini hali ya kisasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.”

Lowassa alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika serikali ya Jakaya Kikwete. Anatajwa kuwa miongoni mwa makumi ya wanachama wa CCM waliotangaza au kutajwa, kusaka urais kwa udi na uvumba katika uchaguzi mkuu ujao.

Januari mwaka jana, Lowassa na makada wenzake kadhaa walipewa “onyo” kwa kile kilichoitwa, “kuanza kampeni kabla ya muda kufika.”

Mtoa taarifa wa gazeti hili anasema, kabla ya kikao cha CC, kutafanyika kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili na Nidhamu, ambacho kitafanya tathmini ya adhabu zilitolewa kwa Lowassa na wenzake.

Lowassa anatuhumiwa kuendelea na mkakati wake wa kampeni kwa kukusanya watu na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, jambo ambalo viongozi wake wakuu wanamtuhumu kukipasua chama chao.

Anasema, kikao cha CC kitatekeleza mradi huo kwa kutumia ripoti zilizotengenezwa na timu za maofisa usalama wa chama hicho, zilizotumwa mikoa yote ili kukusanya kile kilichoitwa, “mkakati wa Lowassa wa kusaka urais.”

Kutokana na hali hiyo, Kamati Kuu iliitaka Kamati ya Maadili kufanya marejeo na kuangalia utekelezaji wa adhabu kwa makada



Upendo na huruma ziko wapi Tanzania? Gharama yote aliyotumia mwenzenu mnamtakia nini CCM na CC yenu?

Muhimu tunahitaji AMANI.
 
Afukuzwe tu kwani ana faida gani? Cha kushangaza wanaokuwa na hofu ni Kibanda na Kubenea ambao walikuwa wanufaika wa fedha za Fisadi Lowasa
Tangu umzabe vibao mzee Warioba naona akili yako imevurugika! Hivi hawa wazee wamekukosea nini?
 
Afukuzwe tu kwani ana faida gani? Cha kushangaza wanaokuwa na hofu ni Kibanda na Kubenea ambao walikuwa wanufaika wa fedha za Fisadi Lowasa

Mkuu umetubu lakini!!Una laana kubwa sana na haiwezi kukuacha kamwe!!
Afu ndani ya chama chenu cha ESCROW yupi ni msafi ukianzia kwa m/kiti wenu mpaka kwa katibu mkuu??Acha upofu maana nahisi pesa unazolipwa kuwachafua watu zinakupofusha!!
Lowassa lazima awe rais wa tz hata mkimfkuza CCM anaweza kusimama kwa miguu yake na akashinda hawategemei WAMA km yule anayekutumia kama CONDOM!!!
 
Huyu kichaa nanevampe madaraka hivi nyie kwa mini mnawadharau wa Tanzania slaa no kichaa jamani bora Freeman anahekima sana
sasa hawa mbowe na slaa wanahusiana nini kwenye mada hii? Zingatia mada usikurupuke...
 
Jamani lait hii habari ingekuwa movie bas ningefowArd ili nione mwisho upoje
 
Nimeshindwa kuweka link mwenye kuweza aende kwenye Twitter ya absolam kibanda kuna hii habari,vilevile kubenea kafichua njama za kumfukuza uanachana Lowasa.
nyingine hizo
 

Attachments

  • 1421006991943.jpg
    1421006991943.jpg
    77.4 KB · Views: 424
akifukuzwa huyu mtoa rushwa papa, nitakuwa wa kwanza kuingia barabarani kuserebuka
 
CCM nyote mu wafu tu na huyo fisadi wenu mwenye nywele kama mdori wa kigabachori
 
Back
Top Bottom