Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,778
Tupate break kidogo kutoka kwenye siasia,
Tracey na Edwin ni vijana wa ki-Tanzania waliokutana Durban South Africa wote wakiwa wanafunzi, Tracey alisomea banking na Edwin alikuwa mchumi. Walianza urafiki kwakua walikua na mengi yanayolingana, wote walitoka (nyumbani) si mnafahamu mkiwa ugenini hili ni neno muhimu sana.
Tracey alikuwa mzuri sana katika masomo yake, alipokuwa mwaka wa pili, alipelekwa placement kwenye bank moja hapo hapo mjini Durban, kwa utendaji wake wa kazi, walimpenda sana na waliahidi kumwajiri mara amalizapo shule kwa ahadi pia ya kutafutiwa vibali vya kazi. Baada ya ile placement pia kulikuwa na kazi walimpa afanye kwa muda wake na walimpa ujira uliolingana na kazi ile, pesa ile ilmsaidia sana Tracey.
Edwin na Tracey walishavalishana pete, walichosubiri ni kumaliza shule. Baada ya Tracey kupata kazi Edwin aliamua kurudi nyumbani, amefika nyumbani aliishi kwa wazazi wake huku akitafuta ajira. Baba yake na uncle wengine wote walimsaidia na alifanikiwa kupata kazi kwenye kampuni ya wa-Irish.
Mshahara wa Edwin ulikuwa mzuri kwa elimu yake, aliamua kuhama nyumbani ili aishi maeneo karibu na kazini. Alifanikiwa kupata nyumba ya vyumba vitatu vya kulala yenye master bedroom. Tracey alikuwa anakuja holiday Tanzania kila baada ya miezi sita na hapa kati Edwin alikwenda Durban kumtembelea Tracey.
Tracey alitoka kwenye familia kidogo wako strict, kwahiyo akitoka Durban huwa alispend siku mbili na Edwin ndiyo anachukua tax kwenda kwao. Huku nyumbani majukumu yalipoanza kuwa mengi, Edwin aliamua kutafuta dada atakaemsaidia shughuli za ndani.
Edwin alimpa dada funguo za nyumba za akiba na mara nyingi hawakuonana, dada alifika wakati Edwin akiwa kazini, kama kuna maagizo yeyote nje ya ratiba aliyakuta juu ya meza ya chakula.
Kuna wakati Edwin alipata homa kali sana, alilazwa hospitali kwa siku mbili, alipopata nafuu alikwenda nyumbani lakini alikuwa weak sana, dada wa kazi alipika soup, mchemsho, soup ya mchicha, mtori, na vitu vingi vya kumpa Edwin nguvu. Dada alijitolea kuja J'mosi na J2 ingawa hazikuwa siku zake za kazi, basi Edwin aliporecover, yeye na dada walikuwa wamezoeana sana.
Sasa bwana baada ya muda dada alipata ujauzito, kwakweli Edwin alisikitika, katika maisha yake Tracey ndiye alikuwa mchumba na future wife, kwa upande mwingine, hajawahi kuitwa baba, hata kama hakupanga hii ilikuwa mara ya kwanza mwanamke anamwambia ana mimba yake. Edwin alimshauri dada ahamie walee ile mimba pamoja.
Tracey ametoka Durban bwana anafika mjini kuchukua tax huyo kwa Edwin, nikamsurprise, kufika anakuta neppy ziko kwenye kamba, jamani ni hii nyumba ya Edwin, akagonga mlango, anamkuta dada wa kazi ambae wanafahamiana, dada anamtoto ananyonyesha, basi Tracey alikaa kidogo, mwenyewe alisoma alama za nyakati, alimwaga dada vizuri tu akamwambia Edwin akija msalimie.
Edwin jioni anarudi anapewa salamu zake, huku mama watoto ameshakuwa mke, hakuna kutoka unakwenda wapi? Khe basi Edwin alisubiri mpaka kesho yake, ilibidi aombe ruhusa kazini kwenda kumuona Tracey, alimweleza hali ilivyotokea, Trace alilia sana.
Hujui maisha yako Mungu aliyapanga vipi, yakitokea ni kumshukuru na kuendelea kumuomba akupe alichokupangia.