Lonely Me...... Nimefiwa na baba yangu

Pole kwa msiba
Mungu akutangulie katika safari yako
na akutie nguvu.
 
Pole sana mkuu,tuko pamoja kwenye kwenye kipindi hiki kigumu cha majonzi.
 
Pole sana bujibuji. Nakutakia safari njema ya kwenda na kurudi Usukumani. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi
 
Pole blaza buji, nashukuru unakoenda si unyakyusana, si unajua misiba yao inavyokuwaga?
 
Pole sana Bujibuji kwa kuondokewa na mpendwa wako, tuko pamoja nawe na tunakuombea heri usafiri salama.

Pamoja na masikitiko hayo, nakuomba next time usijaribu kutabiri kifo cha mtu yeyote. Sorry kama kuna mtu nitakuwa nimemkwaza kwa hili.
 
Wenzangu wana JF, nasikitika kuwajulisha kuwa nimefiwa na baba yangu mdogo, ambaye tulikuwa tumeshibana naye sana, na alikuwa ndiye baba yangu pekee aliyenijali na kunitunza tangu alipofariki baba yangu mzazi.
Nimeachwa mpweke sana, na kesho natarajia kwenda Usukumani kwa ajili ya maziko.
Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu.

Kakak Bujibuji pole sana MUNGU akupoze machungu.
RIP Baba

Buji safari njema na uzike salama.
 
Pole sana Bujibuji,kifo ni hatua ya mwisho ya maisha binadamu yoyote.Jisikie myenye amani.Mungu anakupenda.Safiri salama ukianza safari ya kwenye mazishi na uturudie salama.
 
Back
Top Bottom