Lodge au hotel nzuri ndani ya mkoa wa Arusha!

Lodge au hotel nzuri ndani ya mkoa wa Arusha!

Mlina panafaa Sana
Kwa mkoa wa Arusha... Nafikiri ungekuwa specific kwa kutaja eneo hasa unapoenda huko Arusha ingekuwa rahisi zaidi kupata msaada maana mkoa wa Arusha una wilaya kadhaa.

Kwa nyongeza tu pamoja na msaada utakaopata hapa si vibaya tukajenga mazoea ya kutumia apps kama Booking.com, TripAdvisor na HotelTonight kupata maelezo mengi ya hotel zilizopo huko unakotarajia kwenda mfano jina la hotel, picha ya hotel, mawasiliano yao, umbali kutoka katikati ya mji, bei na picha za vyumba, uwepo wa nafasi yaani chumba, mazingira ya ndani na nje ya hotel, comments za wateja wengine waliowahi kufikia hapo hotelini n.k.
 
Kila unakokwenda jitahidi uwe na mwenyeji jifunze kanuni rahisi kabisa itakusaidia kwa mambo mengi
 
Uchangiaji ni wa aina nyingi sana..

Wapo wanaochangia kwa kutaja app/website ambayo mtu anaweza kutumia.. Kwa mfano, nimejifunza kuna hotelTonight ambayo sikuwahi kuijua.. Uzuri wa app inakupa instant uhakika wa utakapofikia nikimaanisha booking confirmation, picha za sehemu na namba za kuwasiliano nao incase unachelewa, kuwahi au kucancel..

Wanaotaja sehemu ni kutokana na experience ambayo yawezekana wamelala hiyo hotel/lodge/motel/guest house before au walipeleka ndugu/rafiki/mpenzi.. Nao hutoa ushuhuda wao ambao hauna makosa yoyote.. Raha yake watakuelekeza mpaka chocho za kupita na mida ya kuingia ndani au kuzurura.. Utatajiwa baa za kuepuka (kama haupendi biashara mbadala) na kona ambazo hautakiwi kugeuka ukishapita (lasivyo utajulikana ni mgeni)..

Nayasema haya nikielewa app/website kwa sisi sio hotel nyingi ambazo zimejisajili.. Especially hizi zetu za buku 40 kushuka chini.. Na kama zimejisajili, basi bei utakayokuta huko ni tofauti na ukiwazamia ukauliza bei..

Sijazunguka sana ulimwenguni na experience niliyonayo ni limited.. Kikubwa najua mtu anapouliza hivyo (1) anapata mawazo ya maeneo yanyokubalika (2) anajenga mazoea maana yupo mtu anaweza mfuata dm na kumpa detail zaidi (3) anajiweka open kwa msaada mbele ya safari.. Rule namba moja ya safari (ukienda sehemu ambayo ni ngeni kwako au haujafika miaka mingi) ni kuandaa watu wa kazi mji unaoenda kwa kuwaelezea siku utakayofika na utakayosepa ili lolote likitokea wajue watakusaidiaje.. Mbili ni kutambua utakapofikia na maeneo yanayozunguka I.e. hospitali, hotel kubwa, kambi ya jeshi au kituo cha polisi.. Tatu aina ya usafiri unaoweza kutumia taxi, bajaj, daladala, pikipiki, miguu au hata baiskeli..

Safiri salama msafiri..
 
Kweli kabisa ndugu. Jiji la mijambawazi lile sijaona. Unaona jitu liko litanishati, kila j2 kanisani kwa sanaa, ukiuliza shughuli yake halali ipi ? Zero! Baadae unaambiwa lili sijui jambazi na hivi, mara vile! Mara unasikia huyu jambazi wa kuiba majani ya lisho la mifugo na kuwauzia wafugaji!


Ujambazi kwa wachagga ni ujira na ndiyo maana unaona vijana wao wengi wamejikita huko.
 
Back
Top Bottom