Kwa mkoa wa Arusha... Nafikiri ungekuwa specific kwa kutaja eneo hasa unapoenda huko Arusha ingekuwa rahisi zaidi kupata msaada maana mkoa wa Arusha una wilaya kadhaa.
Kwa nyongeza tu pamoja na msaada utakaopata hapa si vibaya tukajenga mazoea ya kutumia apps kama Booking.com, TripAdvisor na HotelTonight kupata maelezo mengi ya hotel zilizopo huko unakotarajia kwenda mfano jina la hotel, picha ya hotel, mawasiliano yao, umbali kutoka katikati ya mji, bei na picha za vyumba, uwepo wa nafasi yaani chumba, mazingira ya ndani na nje ya hotel, comments za wateja wengine waliowahi kufikia hapo hotelini n.k.