Loan department kwenye benki nyingi hawana privacy

Trubarg

JF-Expert Member
Jan 8, 2020
4,260
6,908
Unakuta watu wamepanga foleni kusubiri kuingia hizo wanazoziita ofisi za mikopo..so kila atakayeingia bank atakusoma kwamba unaenda kutafuta mkopo...wengine wameweka desk hapo hapo karibu na tellers, kila unachoongea wateja wengine wanasikia.. Sasa why mnashindwa watunzia privacy ya wateja kiasi Hiki... Mnazingua Sana nyie mabank
 
Mkopo sio jambo la siri

Kudaiwa sio jambo la aibu wala sio jambo la ajabu kuchukua mkopo.

Hata mabilionea wote unaowaona wanadaiwa.
Watu hawajui kutumia mikopo, hivyo imewaumiza mpaka wanaona kama kukopa ni dhambi na tendo la aibu.
 
Privacy inahusu taarifa zako na sio privacy ya umbo lako!!!

Ni kutokana na hilo ndo maana hata kwenye banking halls tunaingia bila kuambiwa tufumbe macho ili tusiwaone wateja wengine waliokuja kufuata huduma za kibenki!

Hata kwenye sekta ya afya, Daktari au hospital crews kwa ujumla wake hawaruhusiwi kutaja hata ugonjwa unaoumwa lakini haimaanishi unapoenda kuonana na daktari, watu wengine wote wataambiwa wafumbe macho ili hatimae uingie chumba cha daktari!!

Hata unapoenda kupima ngoma, watu watajua tu kwamba umeenda kupima ngoma lakini haimaanishi hospitali/Kituo husika hawana privacy!
 
Mshkaji anaona noma akionekana ameenda kukopa acha kuona noma wewe ndio wale wanakopa hata mke hajui mwisho wa siku unaumbuka baada ya kuwa defaulter...
 
Privacy inahusu taarifa zako na sio privacy ya umbo lako!!!

Ni kutokana na hilo ndo maana hata kwenye banking halls tunaingia bila kuambiwa tufumbe macho ili tusiwaone wateja wengine waliokuja kufuata huduma za kibenki!

Hata kwenye sekta ya afya, Daktari au hospital crews kwa ujumla wake hawaruhusiwi kutaja hata ugonjwa unaoumwa lakini haimaanishi unapoenda kuonana na daktari, watu wengine wote wataambiwa wafumbe macho ili hatimae uingie chumba cha daktari!!

Hata unapoenda kupima ngoma, watu watajua tu kwamba umeenda kupima ngoma lakini haimaanishi hospitali/Kituo husika hawana privacy!
Masterpiece..

Nakumbuka ulimuua sana yule jamaa mkenya na IQ ranking zake uchwara
 
Unakuta watu wamepanga foleni kusubiri kuingia hizo wanazoziita ofisi za mikopo..so kila atakayeingia bank atakusoma kwamba unaenda kutafuta mkopo...wengine wameweka desk hapo hapo karibu na tellers, kila unachoongea wateja wengine wanasikia.. Sasa why mnashindwa watunzia privacy ya wateja kiasi Hiki... Mnazingua Sana nyie mabank
Kwani mkopo ni Siri?ni huduma tu Kama ya kuweka au kutuma pesa.kukopa ni ushujaa
 
Mkopo sio jambo la siri

Kudaiwa sio jambo la aibu wala sio jambo la ajabu kuchukua mkopo.

Hata mabilionea wote unaowaona wanadaiwa.
Haujamuelewa mleta mada. Yeye anazungumzia swala la kuwa na privacy baina ya watoa huduma na wateja wao.

Kwann aanike mambo yake hadharani na mtu mwingine awe ana sikiliza?! Na kuna majitu huwa yanatega sikio kabisa kusikiliza unachozungumza.

Sio tu bank, bali hata hospital, na sehemu kadha wa kadha
 
Yah..watu wanajibu tu bila kuelewa concern yangu
 
Uelewa wa WaTz, unatia kichefuchefu! Ati mkopo sio siri!
 
Back
Top Bottom