Benki za Biashara Tanzania zinaogelea kwenye faida. Je, nini kimefanyika awamu ya sita?

Rais wa Matajiri

JF-Expert Member
Sep 14, 2018
1,475
607
Wachumi mtusaidie hili, Hivi mabenki yetu ya biashara kupata faida ya TZS 471B kwa miezi tisa tu,Wakati huko nyuma yalipata TZS 286B kwa mwaka ina maana gani kwa Uchumi wa nchi yetu?Je! ni Vyuma kulegea?

Mtakumbuka kwa mara ya mwisho hapa Tanzania mabenki yetu ya biashara kurekodi faida ya kihistoria ilikuwa ni mwaka 2015 pale ambapo yalirekodi Jumla ya faida ya TZS 438BL hii ni baada ya kulipa kodi ya Serikali.

Mtakumbuka pia kwamiaka mitano mfululizo iliyopita mabenki haya hayajaweza kabisa kuivunja rekodi hii zaidi sana wakati flani faida zao zilishuka mpaka kufikia Jumla ya Tshs 286BL mwaka 2017 hii ilikuwa ni Jumla ya faida kwa mabenki yote ya biashara nchini kwa mwaka huo.

Leo chini ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan tena kwa kipindi kifupi cha Jan -Sept mabenki hayo hayo kwenye nchi hii hii yameivunja ile rekodi iliyowekwa na Dk Jakaya Kikwete kwa faida ya Tshs 438BL kwa zaidi ya 7.53% na hii ni kwa robo tatu tu ya mwaka.

Kwalugha rahisi miezi michache ya Rais Samia mabenki yamevunja rekodi ya faida ya tangu uhuru ambayo ilivunjwa kwa mara ya mwisho na Mzee Jakaya Kikwete kwa thamani ya faida ya Tshs 438BL leo Samia ameivunja kwa thamani ya faida ya Tshs 471BL na hii ni kwa miezi tu, tunaposema Rais Samia hakamatiki tunamaa hii.

Kwa tathimini iliyofanywa kwa mabenki 13 ya kibiashara nchini kati ya 14 yanayotengeneza faida kila mwaka ni NMB na CRDB tu ndio wamebeba 80% ya faida yote ya Tshs 471BL kwa kuwa na faida ya Jumla ya Tshs 379BL,Wakati huohuo NPL yaani Non Performing Loans au mikopo " Chechefu " ikishuka na kufikia chini ya 35.7% kwa baadhi ya mabank huku thamani yake ikupungua kutoka tshs 395.69BL mwaka 2020 hadi tshs 392.4BL kwa lugha ya kibenki (arrears -zimepungua )

Sababu kubwa yaongezeko hili kubwa la Faida kwa mabenki yetu ya biashara nchini zinatajwa kuwa ni Sera nzuri za ki-Uchumi za Serikali ya awamu ya Sita Chini ya Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na miongozo mathubuti toka BOT kama mlezi wa mabenki haya hasa kwenye kupunguza vipimo vya risk kwenye utoaji mikopo ikiwa ni pamoja na kutoa fedha maalumu "Stimulating fund " kiasi cha Tshs 1trl ili kuziongezea Ukwasi baadhi ya Benki zetu za biashara zilizokaukiwa hii imesaidia sana kuinua sekta ya fedha ambayo utoaji mikopo kwa mujibu wa BOT umepanda toka 2.5% 2020 hadi 9.8% hivi sasa,

Kwamsiofahamu zaidi ya 80% ya faida yote ya mabenki ya biashara inabebwa na mikopo na Ukiona mabenki yanapata faida sana maana yake yamekopesha sana na wateja wao wameweza kurejesha mikopo yao ( EMI) kwa wakati na ndio tunasema NPL imeshuka au mikopo isiyolipika|chechefu imepungua na ndio sababu faida imepanda na kwa maana hiyo biashara mtaani inakua au inakwenda vizuri ndio maana mteja X aliyekopa katika benki Y ameweza kuchukua mkopo Benki na kununua bidhaa na kisha kuziuza na mwisho kupeleka marejesho ya Benki kwa wakati yaani (Purchasing Power-Uwezo wa kununua kwa Watanzania) umeongezeka, Hongera Sana Rais Samia hakika unaupiga mwingi.


photo_2021-11-03_09-27-35.jpg
 
Promising time as Tanzania's banking sector set for record profit
MONDAY NOVEMBER 01 2021

Bank pic
Summary
Shareholders of commercial banks must be wearing smiles as the banking sector edges closer to a record profit this year
An analysis of 13 out of the 14 most profitable commercial banks in Tanzania shows that they cumulatively registered a total of Sh471 billion in net profits during the period between January and September 2021.

Josphine picBy Josephine Christopher
More by this Author

Dar es Salaam. Shareholders of commercial banks must be putting on broad smiles as the banking sector is set to register a record profit this year.

An analysis of 13 out of the 14 most profitable commercial banks in Tanzania shows that they cumulatively registered a total of Sh471 billion in net profits during the period between January and September 2021.

The amount – which was characterised by declining levels of Non-Performing Loans (NPLs) by most lenders - is 35.7 percent higher than the Sh347.2 billion that the 13 entities went home with during a similar period last year.

The highest amount in profits to be registered by commercial banks in Tanzania’s recent history, was Sh438 billion that was recorded in 2015.

Since then, the amount kept going down, reaching Sh423 billion and Sh286 billion in 2016 and 2017.

This means that the Sh471 billion that was registered during the first nine months of the current calendar year is also 7.53 billion higher than the net profit for the entire 2015 calendar year.

ADVERTISEMENT

As it has always been, the two largest lenders (NMB Bank and CRDB Bank) got the lion’s share of the sector’s net profit, accounting for close to 80 percent (Sh379 billion) of the Sh471 billion.

CRDB Bank’s net profit tax rose significantly by 39.2 percent to Sh168 billion during the first nine months of the current calendar year from Sh120 billion recorded during a similar period last year.

Similarly, that of NMB Bank rose by 43 percent Sh206 billion.

Top executives of the lenders attribute the rise in profits to a number of factors, including the stability of Tanzania’s economic conditions and accommodative monetary policy measures as adopted by the Bank of Tanzania (BoT). They also attribute the performance to individual bank’s initiatives in aspects such as optimizing costs and prudent approach to risk management among others.

“….reflects continued stability in economic conditions and accommodative monetary policy measures adopted by the BoT. Our strategy execution remains on track, with our continued market share gains translating into higher profits. We continue to maintain a relentless customer focus and have seen strong lending and deposits growth momentum throughout the period,” said NMB Bank chief executive officer, Ms Ruth Zaipuna.

For CRDB Bank, the rise in profits was largely due to prudent approach to risk management and the efficacy of the bank’s digital-first customer-centric business strategy which, according to CEO Abdulamajid Nsekela, helped keep loan growth steady while still being able to moderate cost in the period.

“Once again, the Bank has shown resilience in delivering on its commitment to shareholders, stakeholders, and the investing public as evident in the strong positive financial metrics recorded in the reporting period. We are focused on driving efficiencies while maintaining strong controls, and we are confident of achieving the Bank’s 2021 targets,” he said.

At the peak of the global Covid-19 pandemic last year, the BoT came up with various measures to cushion the economy from the adverse impacts of viral disease.

The BoT cut the discount rate from seven percent to five percent and reduced the statutory minimum reserves (SMR) requirement from seven percent to six percent effective from June 2020 to boost liquidity. It also allowed the commercial banks to discuss with their customers the possibility of restructuring loans and asked them, in collaboration with mobile network operators, to increase transaction limits from Sh3 million to Sh5 million and daily balance from Sh5 million to Sh10 million.

With a cummulative net profit of Sh26.12 billion, the National Bank of Commerce (NBC) was third in terms of profitability. It must also be remembered that during a similar period last year, the lender reported a Sh9.23 billion loss due to some legal obligations.

In the fourth slot was Standard Chartered which recorded a cumulative net profit of Sh24.51 billion while KCB Bank came fifth with a net profit of Sh11.15 billion. Absa Tanzania and Diamond Trust Bank came sixth and seventh respectively with a profit after tax of Sh9.43 billion and Sh8.48 billion respectively.

The eighth, ninth, 10th, 11th, 12th and 13th positions were occupied by Citibank (Sh6.87 billion), Exim Bank (Sh4.66 billion), Bank of Africa (Sh4.49 billion), I&M Bank (Sh3.41 billion), Azania Bank (Sh1.35 billion) and Stanbic Bank (Sh177 million) in that order.


 
Mimi sio mchumi isipokuwa kwa akili yangu ya kawaida tafsiri yake ni kwamba uchumi unafunguka, uwekezaji unaongezeka vikiambatana na ongezeko la mzunguko wa fedha kupitia ajira na huduma kupitia uwekezaji utakaofanywa na mikopo hiyo iliyozaa faida hiyo.

Nadhani ni hatua nzuri kiuchumi.
 
Mimi sio mchumi isipokuwa kwa akili yangu ya kawaida tafsiri yake ni kwamba uchumi unafunguka, uwekezaji unaongezeka vikiambatana na ongezeko la mzunguko wa fedha kupitia ajira na huduma kupitia uwekezaji utakaofanywa na mikopo hiyo iliyozaa faida hiyo........

Nadhani ni hatua nzuri kiuchumi....
Unayohaja, Uchumi unakua kwa kasi,
 
Mimi sio mchumi isipokuwa kwa akili yangu ya kawaida tafsiri yake ni kwamba uchumi unafunguka, uwekezaji unaongezeka vikiambatana na ongezeko la mzunguko wa fedha kupitia ajira na huduma kupitia uwekezaji utakaofanywa na mikopo hiyo iliyozaa faida hiyo.

Nadhani ni hatua nzuri kiuchumi...
Naungana na wewe 100% kwenye hili
 
Maana yake nchi iko vizuri sana,
Maana yake biashara zimefunguka
Maana yake Sera za kiuchumi za awamu ya tano zinalipa,
Maana yake Samia anaupiga mwingi,
Maana yake Tanzania tunakwenda vizuri

Hebu hizo TAKWIMU za benki zitakazoonesha faida kiasi gani imetokana na kukopesha na faida kiasi gani inatokana na bank charges!! Hapo tutajua kama benki zinakopesha au mapato na faida zao zinatokana na TOZO!
 
Hebu hizo Benki sito TAKWIMU zitakazoonesha faida kiasi gani imetokana na kukopesha na faida kiasi gani inatokana na bank charges!! Hapo tutajua kama benki zinakopesha au mapato na faida zao zinatokana na TOZO!!!
Mkuu hili lifanye wewe kwa bank uliyokaribu nayo,
Ukikuta tofauti njoo jukwaani kanusha
 
Mkuu hili lifanye wewe kwa bank uliyokaribu nayo,
Ukikuta tofauti njoo jukwaani kanusha

Mimi sitafuti kuwa DATA wanayotoa ni COOKED hapana; mimi nataka kujua mgawanyo wa hiyo faida, kiasi gani kinatokana na kukopesha wateja na kiasi gani kinatokana na makato wanayowakata wateja wao basi!!!
 
Mimi sitafuti kuwa DATA wanayotoa ni COOKED hapana; mimi nataka kujua mgawanyo wa hiyo faida, kiasi gani kinatokana na kukopesha wateja na kiasi gani kinatokana na makato wanayowakata wateja wao basi!!!
Nimekuelewa ila mkuu ila hii ni average nadhani unaelewa maana yake
 
Back
Top Bottom