Liyumba (wa BoT) na wenzake kizimbani Kisutu

Digits zinazoonyesha jamaa wametia hasara kubwa mno jamani, hakuna namna nyingine ya kuwaongezea mashitaka jamani? Kwanini na PPRA wasiruhusiwe na wao kutinga na watu kwa court manake mikaba mingi ya manunuzi bongo ni fake na wahusika wa kutoa zabuni wametumia kuwanyonga watanzania.

Majengo ya BOT ni mradi mmoja lakini mikataba mingi ya ujenzi, huduma na consultants inafanana sana kilichotokea BOT ni bora sasa kuchunguza na tender zilizotangazwa, mikataba na kuwafikisha watu kwa korti na kuwabana warudishe walichochukua.

Kama jamaa alikuwa anatoa RAV 4 basi nazo zirudi kwanza zipigwe mnada wananchi warudishiwe cha kwao.
 
Mkuu Field Marshall ES,

Nakushukuru kunisaidia kujibu hoja za wale wanaona ambayo wengine hatuyaoni... ati Mkuu wa Nchi ndiye Jaji pia, na Ndio Hakimu pale... Kisutu... ati mpaka wafungwe watuhumiwa wote ndio serikali itakuwa imefanya kazi.

Ndio wale wanaosema uchaguzi huru na haki ni pale chama pinzani kinaposhinda tu... Tarime uchaguzi ulikuwa huru, Mbeya vijijini uchaguzi umeibiwa, daftari la kudumu la wapiga kura lina mapungufu, as if hili daftari limeandikishwa juzi, wakati lilikuwepo muda mrefu si wangefuatilia.


Ndio wale wanawapa kichwa CUF kwamba waende mahakamani kusema uchaguzi umeibiwa kura... si wakishinda mahakamani si watarudi kupigiwa kura tena,,, je watashinda...
Hivi wananchi wa tanzania ni wajinga kiasi gani? kuchagua watu ambao wanapatikana wakati wa uchaguzi tu.

Tanzania yetu inasikitisha... nijuavyo mimi upande wa Serikali umekamilisha... si cheo cha Felesi kiko kikatiba in fact haitwi yuko ndani ya Serikali. Maana ana uhuru wa kukataa au kupeleka jambo mahakamani kulingana na anavyoona... ndio maana Hakumpeleka faili la Karamagi.

Mkuu Kasheshe

Huna hata chembe ya unafiki kwa hayo uliyoandika?

Kwamba hakuna mkono wa Mkuu wa nchi katika swala la kuwafikisha au kutowafikisha mahakamani watuhumiwa wa uhujumu wa uchumi wa nchi hususani EPA?

Kwamba ilikuwa ni lazima na haki kisheria kwake kutoa agizo kwa Mwanyika, Hosea na Mwemakuchunguza na kumpelekea taarifa za uchotaji wa fedha za EPA kabla ya yeye kuhamua ni nani wapelekwe na ni nani wasipelekwe?

Kwamba DPP na TAKUKURU kwa kutumia madaraka waliyopewa kikatiba wasingeweza kupeleka kesi hizo mahakamani bila Mkuu wa nchi kuingilia?

Ni wapi katiba imetenga na kutofautisha kesi za kupitiwa na Rais kabla ya kupelekwa mahakamani na za kupeleka pasipo kufikisha kwa Rais? Kwamba kwa mfumo tulionao, DPP na TAKUKURU wapeleke kesi za KAGODA,Deep green, Mwananchi nk pasipo kupata kibali cha Rais?

Kumbuka kashifa zote hizi zilipigiwa kelele kitambo lakini zikakingiwa kifua na wasaidizi wa Rais. Rejea baadhi ya makampuni ya EPA kuhusishwa na usalama wa nchi (Waziri Meghji), pia Tume ya Rais kuhusu EPA kutishia wananchi kuwa wakifikishwa mahakamani nchi inawaka moto.

Ninachotaka kusema ninatofautiana kabisa na wewe kwamba hakuna mkono wa Mkuu wa nchi kwenye vyombo vya sheria kuhusiana na upelekaji au kutokupeleka watuhumiwa(kagoda) wa EPA mahakamani au aina ya mashtaka
wafunguliwe. Mkono wake ni mkubwa na mrefu tu, vinginevyo...


Hizo rumbana nyingine za vyama vyote vya siasa za siku zote haziwezi kuchanganywa na swala hili muhimu la UHUJUMU WA MALI YA TAIFA yahani EPA, Twin tower, Richmond nk. Hili ni la kitaifa, ni la pamoja, tulipigie kelele wote pasipo kuchanganya vyama. Vinginevyo mafisadi watashinda.


 
Kwa hiyo... naomba kuuliza,
Je bado tuamini JK ni legelege kama tulivyokuwa tunahubiriwa na kundi la "wabadilisha fikra"?

Mkuu Kasheshe hebu pitia kidogo magazeti ya IPPmedia yalivyokuwa nyuma ya serikali ya JK mwanzoni mwa utawala wake (2006) na jinsi "wabadilisha fikra" walivyotuhumiwa:-

1. http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/.../20/68711.html
2. http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/.../20/68735.html
3. http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/.../20/68702.html
4. http://www.ippmedia.com/ipp/guardian.../20/68695.html

Hayo ni baadhi tu lakini baada ya macho yao kufunguka na kuona uovu unavyokumbatiwa hivi sasa msimamo wa IPPmedia bila shaka hata wewe unaujua.

Halafu soma haya maelezo ya Dr. Slaa kwa nini aliondoa hoja yake bungeni mwaka uliofuatia 2007.

MBUNGE wa Karatu, Dk Wilbrod Slaa (Chadema), amefuta kusudio lake la kuwasilisha bungeni hoja binafsi ya kutaka iundwe kamati teule kuchunguza ubadhirifu katika taasisi nyeti za umma, ikiwamo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kile alichoeleza kuwa Spika wa Bunge, Samwel Sitta, hajaiweka hoja hiyo katika shughuli za Bunge tangu alipoiwasilisha.


Dk Slaa alitangaza kufutwa kwa kusudio hilo mbele ya waandishi wa habari mjini hapa jana, huku akieleza kuwa suala hilo limezua mzozo ambao utakuwa na madhara kwa mustakabali wa Tanzania. Pia, mbunge huyo alitangaza mchakato mbadala wa kutaka suala hilo sasa lianze kushughulikiwa kwa njia mbalimbali ili hatimaye ukweli uweze kudhihiri na kuwekwa wazi.

Akiongozana na wabunge karibu wote wa kambi ya upinzani, akiwamo Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed (Wawi-CUF), Dk Slaa alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kubaini kutokuwapo kwa dhamira thabiti na dhati ya Bunge, chini ya Spika Samwel Sitta kuweza kukaa, kusikiliza, kujadili suala hilo nyeti wakati wa kikao cha Bunge kinachomalizika leo.

Licha ya kuvipongeza vyombo vya habari nchini kwa kuwezesha kufichuliwa kwa maovu mengi, Dk Slaa alieleza kuwa vikwazo alivyowekewa tangu mwanzo na Spika Sitta alipoamua kueleza dhamira ya kuanza rasmi mchakato huo, vimemkatisha tamaa. Jumanne asubuhi, kabla ya Bunge kuanza kusikiliza hoja binafsi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (aliyesimamishwa), Zitto Kabwe, Spika Sitta alieleza kwa ufupi kuhusu hoja ya Slaa.

Alieleza kuwa suala hilo ni zito, lakini linalohitaji ushahidi, lenye kumtaka pia yeye (Spika) ajiridhishe kwanza na ushahidi wowote ambao unawasilishwa kwake na mtoa hoja (Slaa). Akizungumza kwa umakini mkubwa, lakini wenye kuonyesha dhahiri hasira, Dk Slaa alieleza kuwa licha ya kutotakiwa na kanuni za Bunge kumridhisha kwanza Spika Sitta kabla ya kuamua kuwasilisha hoja binafsi, lakini Agosti 13 aliwasilisha ushahidi na vielelezo vyote.

Jambo hilo alisema alilifanya ili kuthibitisha unyeti wa suala lenyewe na kuonyesha kitabu ambacho alisema ushahidi umekusanywa kwa umakini mkubwa kutoka hata ndani ya taasisi za serikali kwa mujibu wa sheria. Aliyataja maeneo mahsusi ambayo hoja yake ilikuwa imejielekeza zaidi kuwa ni makampuni ya Mwananchi Gold, Meremeta, Tan Gold na Land Gold na kuongeza kuwa ushahidi wote ulikuwa katika vipengele A-F.

Alieleza mshangao kuwa licha ya Spika kukabidhiwa tangu Agosti 13, lakini hadi jana hakuwa ameonyesha dhamira ya kuiweka hoja hiyo katika taratibu za mikutano ya Bunge. "Ni dhahiri kwamba tumebaini licha ya uzito wake, lakini hoja hii nzito yenye maslahi kwa wananchi inaendelea kupigwa danadana na kutokana na uamuzi huo tumeamua kutafuta njia nyingine kulishughulikia ikiwa ni pamoja na kukata rufaa kwa wananchi," alisema Dk Slaa na kuongeza;

"Tuna wasiwasi kwamba hizo ni mbinu za makusudi za kuificha ili isiweze kufahamika kwa wananchi wetu ambao ndio wametutuma na kutuingiza hapa bungeni. Viongozi wetu, watueleze wanachokiogopa ni nini hasa," alihoji Slaa na kuongeza; "Lakini, viongozi wetu watambue kuwa hata kama Tanzania inaendelea kusifiwa kimataifa, lakini uovu kama huu unaofanyika sasa, unafichwa na matokeo yake walalahoi ambao ni maskini wanaendelea kuteseka ungefichuliwa ungesaidia kulijengea heshima Bunge ambalo ni taasisi inayotakiwa kusimamia serikali," alieleza mbunge huyo.

Aliongeza kuwa inashangaza kuona viongozi wengi walioko madarakani wanapenda kuwasiliana hata na mashirika na wahisani walioko nje, ikiwamo Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa lengo la kujikosha ili waonekane wasafi, kumbe kuna mambo wanaficha ukweli wake.

Bila kuwataja viongozi wahusika, Dk Slaa alidai kuwa viongozi hao wameikosesha nchi kiasi cha Sh2 bilioni kutoka kwa wahisani hao hao tangu mwaka jana kutokana na kutorejeshwa kwa fedha walizokopeshwa na zilizotokana na mfumo wa ununuzi wa madeni.

"Tuna wasiwasi. Tuhuma hizi za wizi na ubadhirifu ni nzito, zinahitaji uchunguzi na kuchukuliwa hatua zikiwamo za kuwasimamisha wahusika, lakini tunashangaa kuona wanakingiwa kifua," alieleza. Aliongeza kuwa wasiwasi wao ni kuwa hicho kinachojaribiwa kufanywa kwa sasa si kizuri, huenda ni kutaka kuuchezea hata huo ushahidi, vielelezo vyote ambavyo vimewasilishwa kwa Spika na huenda ndiyo maana kumekuwapo na ucheleweshaji usio wa msingi.

Mbunge huyo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chadema, alisema baada ya kuondolewa kwa hoja hiyo, upinzani umedhamiria kuchukua hatua kadhaa zikiwamo za kisheria, kuwasiliana na wananchi kwa njia mbalimbali, ukiwamo mkutano wa hadhara ambao utafanyika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam kesho. Hatua nyingine, aliitaja ya kuwaeleza pia wafadhili na wahisani mbalimbali ndani na nje ya nchi wakiwamo Benki ya Dunia na IMF kuhusiana na suala hilo.

Hata hivyo, alisema kuwa rufaa pekee na kubwa itakuwa ile ambayo kwa kutumia umoja wa wapinzani, itakatwa kwa wananchi wote wa Tanzania ambao ndio wamepewa dhamana ya kuwaweka wao madarakani.
Kuhusu madhara yanayoweza kutokea kutokana na kuondolewa kwa hoja hiyo bungeni, Dk Slaa alisema wamejiandaa kukabiliana nayo ikiwa ni pamoja na kukumbana na vitisho kama vile ambavyo wamekuwa wakipata vikiwamo vya kutishiwa maisha.

"Tunajua athari zake, mbona tumekuwa tukipokea SMS kwa kutumia simu na namba binafsi, baadhi zinatishia maisha yetu, nasi tuko tayari kwani hii ni vita ni sawa na askari shupavu anayefia vitani akipigania nchi yake," alisema. "Hatuna tone la hofu, tunapigania haki ya maskini wa Kitanzania walio wanyonge," alisema mbunge huyo na kuongeza kuwa wamekatishwa tamaa, kiasi cha kuamini kuwa hata ikiwasilishwa bungeni hoja hiyo ingezimwa kama nyingine.

Naye Hamad Rashid Mohammed alionya dhidi ya tabia ya viongozi wa Tanzania kutoishi na kuheshimu viapo ambavyo waliapa wakati wakiingia madarakani na kukumbatia maovu. Alisema kutokana na kukosa aibu na utii kwa viapo vyao, ndio maana wamekalia kimya tuhuma za ujenzi wa minara pacha ya BoT ambayo imeiingizia nchi hasara inayofikia dola milioni 600, lakini hakuna kiongozi anayejali au kusumbuliwa na suala hilo.

Aliongeza kuwa hata wakaguzi wa hesabu wamenyimwa taarifa muhimu hivyo kutia mashaka juu ya suala hilo. Alidai kuwa BoT bila ruksa, uhalali wowote imetoa mikopo inayofikia Sh30 bilioni bila dhamana , jambo ambalo alisema wataendelea kulipigia kelele kama ambavyo wanafanya.

Mkuu Kasheshe kama kuna wa kupongezwa ni hao "wabadilisha fikra" waliosimama kidete licha ya vitisho na vijembe kupigania kile wanachoamini kina maslahi kwa taifa. JK muda wote amekuwa kama gari la mkono linalosimama pale pale mpaka lisukumwe - bahati mbaya zaidi gari lenyewe ni kuu kuu na legelege na haliwezi kubeba vizito.
 
- Kama kufikishwa kwenye sheria kwa hawa wakuu wa BOT ni uamuzi wa rais, basi Tanzania huenda hatuna sheria kabisaa meaning kwamba ni a lawless nation kama Sodoma na Gomora, is that so?
 
- Kama kufikishwa kwenye sheria kwa hawa wakuu wa BOT ni uamuzi wa rais, basi Tanzania huenda hatuna sheria kabisaa meaning kwamba ni a lawless nation kama Sodoma na Gomora, is that so?

Hotuba ya mwisho ya Kikwete bungeni aliligusia hilo la madaraka MAKUBWA ya Rais wa Tanzania. Akasema hata wako kwenye mpango wa kuyapunguza (mhhh!!!, no comment). Akitoa mfano akasema watu wanakuja kwake wanasema "Mkamate Slaa". Akaongeza kuwa, anaweza kuagiza ukamatwe na uwekwe ndani. Polisi wakiuliza kwa kosa gani anasema wee muweke ntafikiria. Ikipita miezi mitatu, anaulizwa vipi huyu jamaa? Yeye anasema "mpe wiki mbili zaidi halafu mfungulie. Kosa wee fikiria lolote".

Sasa kama anaweza KUKUWEKA ndani, na anaweza kukutoa ndani (mfano TID), je KUKUPELEKA MAHAKANI au KUTOKUKUPELEKA hili hana uwezo nazo??
Au mie naona KIHINDI HINDI??
 
Wakati tunasema mwanzoni kuwa serikali ya JK ni ze comedy na mkulu mwenyewe ni joti mlifikiri ni utani sasa subirini muone what will happen, no body atafungwa na hawa wote wameshambiwa kuwa hakuna wa kufungwa lakini ili kukipa uhai chama cha mafisadi inabidi watolewe kafala na kufikishwa mahakamani.

Ni kweli hakuna ushaidi wa kuwepo kwa rushwa lakini kuna mazingira ya rushwa hapa ni vigumu kuwashitaki kwa rushwa na kuwashitaki kwa makosa waliyoshitakiwa nayo ni sawa na mchezo kwani hakuna mtu anayeweza kufungwa kwa makosa ya kuzembea na kuitia serikali hasara.

Today's decision may be relevant to the ciecumstances but may be irrelevant to next days circumstances, hizi body duties zao ni nini kama mnapitisha kila kinacholetwa na wao wapelekwe mahakamani, kama hawakupelekwa then no body atakuwa convicted kwani wao wajibu wao ilikuwa kushauri body na body inaweza kukataa au kukubali ushauri wao.

Sijui upande wa sheria lakini mshauri anaweza asibebe mzigo wa decision ya mtu mwingine unless otherwise stated kwenye duties zake kwamba ushauri wake utakuwa ndio wa mwisho ili body ifanye decisions.

Enron ilipokufa kamouni ya mahesabu haikushitakiwa ila ilikufa kifo cha kawaida kwa kupoteza credibility ya intergrity kwenye proffessional, hata hawa it will be the same washachukua mapesa yao watakaa chini wale vizuri labda hadhabu waliyopata ni kutokuwa kazini na wengine waliachwa mpaka wakastaafu wenyewe kwahiyo kodi za watanzania wataendelea kuwalipa pension pamoja na kuwaibia mabilioni.

Ama kweli tanzania ni shamba la bibi.
Wakulu
Haya mambo kama HAMFAHAMU yanayoendelea nyuma ya pazia ni bora kuingia hapa kama guest.Siyo lazima tupost.BAADA YA VERDICT , HAKUNA ATAKAYERUDI USWAHILINI.
 
Haya majengo ni bonge la scandal. PCCB bila msaada wa hao wataalam waliopewa kazi ya kufanya ukaguzi itakuwa ngumu kuwatia mbaroni kina Liumba maana malipo yote alipewa mkandarasi moja kwa moja. watu wanajua ukweli wa kila kitu ni waliokuwa washauri wa ujenzi na mkandarasi mwenyewe.

PCCB ikiwa haijajipanga vizuri watarudi uraiani mda si mrefu. Technical Audit ya wataalam ni muhimu sana. Kujenga jengo lenye gharama ya US$ 8000 kwa mita ya mraba TZ ni ndoto, sijui liwe na nini. kuna mambo mengi yatagundulika kama uchunguzi na kesi vitaenda sawasawa
Mkulu
Usichanganye mambo.UCHUNGUZI umekamilika ndio maana wamepelekwa mahakamani.

PCCB ni agency ambayo inauwezo wa kutosha wa kuchunguza madudu yaliyopo kwenye system yetu.Hata Richmond, initial report ya vijana walioenda site walitoa taarifa ya MAANA, ambayo baadaye ikaja kuwadoctored.Na hata Mwakyembe kwenye taarifa yake bungeni alizungumzia upotevu wa taarifa ile ya awali.

Nachojaribu kusema hapa tusiangalie PCCB kama ka agency fulani kalikochoka in terms of its capacity to investigate the same.Pale kuna watu wanajua kazi zao.Tumewapa dhamana na sasa wanatuonyesha nini wanaweza kudeliver kwetu sisi kama waajiri wao.TUSIZUNGUMZE AS IF HIVI NI VIJIKESI NA WAMEKURUPUKA NA UCHUNGUZI UNAENDELEA.

NO, MAMBO YAMEKAMILIKA.

BIG UP TO ALL WAZEE KWA VIJANA , WALIOWEZA KUTUWEKEA SYSTEM HII ,AMBAYO LEO HII INAEXPOSE YOTE HAYA.
 
Hivi hawa jamaa wakati wanapanga kuiba hizo fedha walijua kuwa ni Bilioni 221?

Najiuliza katika Tanzania hiyo mtu unawezaje kufikiria kuiba Dola Mil 221..!!!
__________________


MITHALI 23:7 """AJIONAVYO MTU NDIVYO ALIVYO"" WAACHEN WAFU WAZIKE WAFU WAO
 
Hivi kuna watu wanamtetea KIKWETE? Teh teh teh teh.... Kodi zetu zitawalipa fidia mafisadi wakishinda kesi.....na watashinda nakwambieni. Wanatengenezewa dili tu..

Mafisadi wanafisadi kwa UZEMBE wa mkuu wa kaya..."boss akilala tunazichapa tu...." WIZI MTUPU!
 
Hii kesi ya akina Liyumba sijaielewa vizuri. Kwa ufinyu wa uelewa wangu ni kuwa idhini ya ujenzi ama upanuzi wa majengo ya BOT pamoja na ulipaji wake hutolewa na BODI. Iweje Mkurugenzi wa Utawala na Meneja Miradi ndio pekee waliweza kuidhinisha malipo makubwa kama hayo? Je! ni kweli kwamba hakuna wajumbe wa bodi walioshiriki kwenye uchafu huo, Kama wapo mbona hawajaunganishwa na hawa jamaa kwenye kesi inayowakabili?
 
Date::2/17/2009
Liyumba apata dhamana ya Sh882milioni, wakili wa serikali alalamika
Na Nora Damian
Mwananchi

HATIMAYE aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA) katika Benki Kuu Tanzania (BoT) Amatus Liyumba, amepata dhamana ya Sh882milioni, huku serikali ikilalamika nje ya mahakama kutoridhika na hatua hiyo.

Dhamana hiyo ni thamani ya nyumba yake iliyoko Mbezi Juu jijini Dar es Salaam.

Dhamana kwa Liyumba na wenzake wanaokabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh221bilioni, imekuja baada ya safari ndefu ya kujinasua na machungu ya mahabusu, ikiwa ni pamoja na kujaribu kutaka kiasi cha fedha za dhamana kipunguzwe.

Hata hivyo, baada ya safari hiyo ndefu ya nenda rudi kutoka gerezani akijaribu kutafuta dhamana huku akigonga mwamba, hatimaye jana mahakama ilimpatia dhamana hiyo.

Uamuzi huo kwa mtuhumiwa huyo ulitolewa jana saa 8:00 mchana na Hakimu Mkazi, Hadija Msongo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambaye alisema kuwa mshitakiwa huyo atakuwa nje kwa dhamana ya Sh882milioni, wakati mahakama ikijiridhisha na hati nyingine zilizokataliwa na upande wa mashitaka.

"Mshitakiwa utatakiwa kutimiza masharti ya dhamana ya kiasi kilichobaki cha Sh54,417,344,800.23 endapo mahakama itaona kuwa hati hizi zina kasoro," alisema Msongo.

Hata hivyo, akizungumza mara baada ya mahakama kuisha, wakili wa serikali Justus Mulokozi, alisema hawajaridhika na maamuzi yaliyotolewa na kwamba watakaa kuyajadili na kuyatolea maamuzi.

"Sisi kama serikali tunashangaa tutakaa kujadili suala hili na kulitolea maamuzi kupitia ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali," alisema Mulokozi.

Kabla ya kutolewa uamuzi huo, Hakimu Msongo aliahirisha kesi hiyo saa 6.34 mchana baada ya kutokea malumbano baina ya upande wa mashitaka na wa utetezi juu ya hati zilizowasilishwa mahakamani hapo na hati ya kusafiria.

Mmoja wa mawakili wanaomtetea Liyumba, Hudson Ndusyepo alisoma hati na leseni za makazi kwa maeneo ambayo hayajapimwa lakini upande wa mashitaka ulikubali hati moja ambayo ni ya nyumba ya Liyumba iliyoko Mbezi Juu yenye thamani ya Sh 882 milioni.

Wakati wa kusoma hati hizo wakili Ndusyepo hakutaja namba wala mahali iliko bali alitaja jina lililoko kwenye hati husika.

Mbali ya Liyumba majina mengine yaliyoko kwenye hati hizo ni Jamila Nzota, Abubakar Ogunda, Avogati Chiwendo, Mikidadi Mtumbati, Seleman Kaboke, Justus Samson, Gideon Chipande, Hashimu Mwinyimvua na John Ngutiro.

Hata hivyo Wakili wa Serikali Mulokozi alipinga kupokelewa kwa hati hizo kwa madai kuwa nyingi zina mali zisizokuwa za kudumu kama vile kuku, ng'ombe na mbuzi ambazo alidai haziwezi kuwasaidia kama dhamana.

Sanjari na hilo pasipoti yake iliyowasilishwa mahakamani hapo yenye namba A032 0091 yenye jina la mshitakiwa, ilionyesha kuwa iliisha muda wake Desemba 2, 2007.


"Hati nyingi tulizoziangalia zina mali zisizodumu kama kuku, ng'ombe na mbuzi na hazimtambulishi mtu aliyefanya uthamini hakuna hata mihuri tuna wasiwasi zisije zikawa za mitaani," alisema Mulokozi.

Licha ya kutokuwa na barua za waajiri wao kama masharti ya dhamana yanavyotaka, wadhamini ambao ni wafanyakazi wawili wa BoT, Benjamin Nduguru (Mhasibu wa benki hiyo) na Agaterus Oto (Afisa Usalama wa Ndani wa BoT) walikubaliwa na mahakama.

Katika hatua nyingine, mahakama hiyo ilikubali upande wa Jamhuri kumchukua mshitakiwa wa pili, Deograthias Kweka kwa ajili ya upelelezi na imetoa amri upelelezi ufanyike wakati wa saa za kazi.

Hakimu Msongo alitoa ruhusa ya siku mbili Februari 18 na 19 mwaka huu na kwamba wakati wa upelelezi, mshitakiwa ataruhusiwa kuwa na mawakili wake binafsi.

Liyumba na Kweka walipandishwa kizimbani Januari 27, mwaka huu kwa tuhuma za kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia Seriakali hasara ya zaidi ya Sh221bilioni, Kweka bado hajapata dhamana.

Mradi wa majengo pacha ya BoT Makao Makuu, unaelezwa kutumia kiasi kikubwa cha fedha zaidi ya Sh500 bilioni, ambazo thamani yake (Value for Money) imejaa utata.
 
Back
Top Bottom