Liyumba (wa BoT) na wenzake kizimbani Kisutu

Mkuu mtindio yaani hii ya Liumba na mimi inanipa shida sana kuamini na akam ni hivyo ndivyo BOT inavyoendeshwa basi kuna haja ya kutengua the whole BOT uongozi na kuleta consultant hapo (ulaji mwingine.. lol) atutengeneee tructure ya kueleweka!!!!!

Mkuu hata mimi nashindwa kuelewa hii inakuwaje kuwaje..watu 2 wana-handle 200 billion na kuzi-drain in open air..

May be..Lakini kama ni hivyo hii itabidi iingie kwenye GUINESS BOOK OF RECORDS ..


Only in Bongo..!
 

...maamuzi yoyote ya Bodi yanapewa baraka na Bodi Nzima ya Wakurugenzi. Bodi yoyote ni 'colegial' body na kama kuna makosa kwa pamoja bodi yote inapaswa kuwa mshukiwa.

Swali la kujiuliza, kwa nini bodi ya BOT ambayo ndo yenye dhamana ya uongozi isishtakiwe kwa kulitia hasara taifa?



Kama mambo yenyewe ni hivi, ni vema Liumba na Kweka wakaachiwa iwapo haiwezekani kuwaunganisha wajunmbe wengine wa bodi katika sakata hili. Inavyoonekana, kosa la Liumba na kweka ni dogo sana katika sakata zima-kutioa ushauri mbovu kwa bodi ambayo ndiyo iliidhinisha mradi uliosababisha hasara hii yote. Kumshitaki Liumba na Kweka kwa kosa la kusababisha hasara bila kuihusisha bodi nzima, ni kuwatoa kafara
 
Kwa tabia ya mswahili pesa yote ile, inawezakuwa ilisha kwenye matanuzi.
No investments.Mahakama inapo demand bail amount kama hiyo ya 50%,hapo ndipo majuto yanapoanzia.If what is said is true,kwamba huyo Liyumba alikuwa na maisha ya HOVYO,basi ataozea huko mahabusu.
SOMO HILO WAKULU.

unakosea... jana hiyo hiyo on the spot liyumba alitoa nyaraka za mali yenye thamani ya bilion 55 na kwa sasa ni uhakiki tu wa mahakama unafanyika atatoka saa yeyote kuanzia sasa!!!! UKWASI HUO TUNAITA
 
Haya hizo hapo sehemu ya mashitaka yenyewe.

Nina maoni ambayo nahitaji wanasheria wanisaidie. Shitaka la kwanza linasema Liyumba alifanya uamuzi bila kuishirikisha bodi, mashitaka yanayofuatia wanaambiwa waliipotosha bodi iliyofanya uamuzi wa kutoa fedha hizo. Sasa shitaka la tatu linalifuta la kwanza kwa kuwa kama waliipotosha bodi ikafanya maamuzi ina maana kwamba waliishirikisha bodi.

Hoja ya pili ni kwamba kwa mashitaka haya ina maana kwamba watendaji wote watashitakiwa kwa makosa ya uamuzi wa bodi zao na kwamba bodi itasifiwa tu kwa mambo mazuri mabaya waachiwe wenyewe.

Hapa si kwamba Liyumba na mwenzake ni safi sana katika hili lakini ni kwamba wote walihusika na hapa hakuna cha bodi wala watumishi wa idara husika, wote wezi
 

Attachments

  • LIUMBA_doc.JPG
    LIUMBA_doc.JPG
    52.2 KB · Views: 114
  • LIUMBA_Doc2.JPG
    LIUMBA_Doc2.JPG
    84.9 KB · Views: 118
Comrade Mpayukaji

Re: Liumba (wa BoT) na wenzake kizimbani Kisutu

Ama kweli ukishangaa ya Musa utaona ya firauni!!! Mbona Rais mstaafu wamemwacha kwenye hili la Twin Towers?

Kwa kweli hata mimi nshangaa. Lakini jambo moja ni dhahiri, Rais Mstaafu alijua kuwa nchi hii ina ufisadi mwingi na kuna ule msemo: "if you can not fight them, join them". Nadhani hicho ndicho alichokifanya, na kwa kuwa alikuwa anamalizia muhula wake wa utamu hakuona sababu ya kujihangaisha maana lisingemwongezea chochote kwa wananchi wanyonge wa Tanzania.



Invisible

Kwa sasa ishakuwa ngumu. Wamepelekwa Keko kwani bail yao ilikuwa ni nusu ya kiwango kinachoaminiwa kuibiwa (Bilioni 221).

Vogue ya Liumba ameiacha pale PCCB[/QUOTE

Yaani hii nchi yetu ni tajiri wa kutupwa! Kabisa, anayebisha mwache abishe! Haiwezekani mabilioni yote hayo yakwapuliwe- EPA akaunti moja tu ya BoT tena kwa mwaka mmoja tu2005 (tena hiyo ni sample katika ukaguzi wa Ernst and Young, wangefanya in datails zingekuwa pesa nyingi zaidi), Twin Tower plus yale tusiyoyajua. Hii ni aibu kubwa kwa Rais Mstaafu na nathubutu kusema kuwa kwa kweli hakusaidia ila alijisaidia mwenyewe na kuwawekea mizizi mirefu Mafisadi. Nataka kuamini kuwa ni shemu ndogo mno ya pesa za Serikali na Wafadhili hutumika ipasavyo.

]
Kuna haja ya ku-revisit the foundations of this nation na kuona ni wapi tulienda wrong. Siku zote tumekuwa tukibeza corruption ktk Nigeria lakini kumbe na sisi wamo kwa sana tu. Hata ile taasisi ya kuhunguza/ kuevaluate ufisadi TI - Tranparency international nadhani imekaa kimazabe mazabe tu si walituambia kama miaka mitatu iliyopita kwamba ufisadi umepungua mno nchi hii!!!!!!!

You are quite right Nyambala, tunahitaji Kiongozi Mwingi mabaye atakuwa Mwasisi wa Maendeleo ya Tanzania, kabisa!
 
Haya hizo hapo sehemu ya mashitaka yenyewe.

Nina maoni ambayo nahitaji wanasheria wanisaidie. Shitaka la kwanza linasema Liyumba alifanya uamuzi bila kuishirikisha bodi, mashitaka yanayofuatia wanaambiwa waliipotosha bodi iliyofanya uamuzi wa kutoa fedha hizo. Sasa shitaka la tatu linalifuta la kwanza kwa kuwa kama waliipotosha bodi ikafanya maamuzi ina maana kwamba waliishirikisha bodi.

Hoja ya pili ni kwamba kwa mashitaka haya ina maana kwamba watendaji wote watashitakiwa kwa makosa ya uamuzi wa bodi zao na kwamba bodi itasifiwa tu kwa mambo mazuri mabaya waachiwe wenyewe.

Hapa si kwamba Liyumba na mwenzake ni safi sana katika hili lakini ni kwamba wote walihusika na hapa hakuna cha bodi wala watumishi wa idara husika, wote wezi

[media]https://www.jamiiforums.com/attachments/jukwaa-la-siasa/3403d1233134756-liumba-wa-bot-na-wenzake-kizimbani-kisutu-liumba_doc.jpg[/media]

[media]https://www.jamiiforums.com/attachments/jukwaa-la-siasa/3404d1233134756-liumba-wa-bot-na-wenzake-kizimbani-kisutu-liumba_doc2.jpg[/media]
 
Hivi Ballali yuko wapi?yeye atakuwa anajua vizuri sana kuhusuina na haya.Hata kama tulizugwa amekufa si aliacha ushahidi kwa Mwanasheria wake?

Mie haingii akilini kuwa BOT walitumia zaidi ya billioni 221 bila ya ofisi hizi kufahamu.

1.Wizara ya fedha
2.Gavana wa Benki Kuu
3.Katibu Mkuu Kiongozi
4.Wakurugunzi wa bodi ya BOT
5.OFISI ya CAG


 
Wakati tunasema mwanzoni kuwa serikali ya JK ni ze comedy na mkulu mwenyewe ni joti mlifikiri ni utani sasa subirini muone what will happen, no body atafungwa na hawa wote wameshambiwa kuwa hakuna wa kufungwa lakini ili kukipa uhai chama cha mafisadi inabidi watolewe kafala na kufikishwa mahakamani.

Ni kweli hakuna ushaidi wa kuwepo kwa rushwa lakini kuna mazingira ya rushwa hapa ni vigumu kuwashitaki kwa rushwa na kuwashitaki kwa makosa waliyoshitakiwa nayo ni sawa na mchezo kwani hakuna mtu anayeweza kufungwa kwa makosa ya kuzembea na kuitia serikali hasara.

Today's decision may be relevant to the ciecumstances but may be irrelevant to next days circumstances, hizi body duties zao ni nini kama mnapitisha kila kinacholetwa na wao wapelekwe mahakamani, kama hawakupelekwa then no body atakuwa convicted kwani wao wajibu wao ilikuwa kushauri body na body inaweza kukataa au kukubali ushauri wao.

Sijui upande wa sheria lakini mshauri anaweza asibebe mzigo wa decision ya mtu mwingine unless otherwise stated kwenye duties zake kwamba ushauri wake utakuwa ndio wa mwisho ili body ifanye decisions.

Enron ilipokufa kamouni ya mahesabu haikushitakiwa ila ilikufa kifo cha kawaida kwa kupoteza credibility ya intergrity kwenye proffessional, hata hawa it will be the same washachukua mapesa yao watakaa chini wale vizuri labda hadhabu waliyopata ni kutokuwa kazini na wengine waliachwa mpaka wakastaafu wenyewe kwahiyo kodi za watanzania wataendelea kuwalipa pension pamoja na kuwaibia mabilioni.

Ama kweli tanzania ni shamba la bibi.
 
Yaani hata ukifikiri haingii akirini, hivi BOT hawana audit commitee ya wataalamu wanaofanaya kazi kwa kufuata taratibu zao, au walikuwa wanatoa ushauri unafichwa kwenye makabati.

Hivi mkurugenzi wa internal audit anafanya nini pale maana siku hizi internal audit department lazima wafanye Value For Money Audit (VFMA) kwanini hawakugundua kuwa mradi umekuwa inflated, kama walijua kwanini hawakusema, kama walisema kwanini hatua hazikuchukuliwa, kama hawakusema mbona hawako mahakamani.

Mkaguzi wa mahesabu wa serikali aliyestaafu kabla ya uto, analiability gani kwenye hili, kwanini hakuliona, kama aliliona kwanini hakulilipoti kwa mkuu wa nchi kama anavyotakiwa, kama alilipoti kwanini mkuu Che Nkapa hakuchukua hatua, kama hakuchukua hatua Mbona hayuko mahakamani.

Tushukuru mungu pamoja na ubaya wa serikali ya JK kuna mambo makubwa anayofanya yatakayojenga nchi yetu miaka kadhaa ijayo mojawapo ni hili la kuruhusu report ya CAG kujadiliwa bungeni sasa tunaweza kuona nani anawajibika na wizi kama huu, maana hatuwezi kujua kiasi gani Mkapa anahusika na hili lakini binafsi nafikiri anahusika nalo.

Mkuu wa kaya JK kwa hili you have my support kwani responsible government starts with financial responsibility. Ahsante kubwa sana
 
Huyu si ndiye yule aliwahi kuzungumzwa na mmojawapo wa viongozi wa juu nchi hii siku ya ukimwi duniani kuwa akiwanunulia visichana magari mekundu, nguo nyekundu na kufanyia mapenzi kwenye shuka nyekundu and of course akiwalipa noti nyekundu nyekundu za 10 thousand? SI ndiye huyu? Huyu hakuhusika na kusimamia ujenzi wa twin towers huyu? Jamaa mbwembwe na maringo mengi sana akitembea mabega juu. Yuko mwingine pia alihusika na kuileta Net Group Solutions pale TANESCO akishirikiana na shemeji wa kigogo mmoja wa awamu ya tatu. Naye alikuwa anapiga maji sana kwam vile fedha ilikuwepo mpaka maini yakaungua na figo kujaa mawe. Kufuru ya fedha na ufisadi. We acha. Kweli malipo ni hapa hapa duniani.
hahaha Simon hizo nyingine ni chachandu yaani mashuka mekundu? Mlijuaje? na je alikuwa akiingia gust anaagiza kabisa mashuk aya rangi hiyo au alikuwa anatembea nayo garini ili akifika tu chumbani anatandika?... ah kama mchawi basi!!!


All in all nafurahi kuona sheria ikichukua mkondo wake. Kwa wale aliowaajiri kwa kupitia mgongo wa nyuma basi wachunguzwe kama wanazo sifa sahihi za kazi wanazozifanya la sivyo wafukuzwe na kisha nafasi hizo zitangazwe ili wenye sifa (naamini wapo kibao wanasaga lami kutafuta kazi mtaani) wajitokeze.
 
Napenda kutoa maoni yangu kama watanzania wengine huyo bwana Liumba pamoja na kuajiri watoto wa vigogo alikuwa anatumia pesa alizotuibia kufanyia mambo yake ya kishenzi, bora hizo pesa angezitumia kujenga hata hospitali kijinini kwao,na hili swala la kuajiri watoto wa vigogo halipo BOT pekee kwani kuna mashirika kibao e.g PSPF,PPF,ect kuna watoto wa vigogo

Huu utamaduni ukomweshwe tunapoenda sio kuzuri, kwani wazalendo wa manzese,Tandika,mbagala N.k iko siku watadai watoto wao nao waajiriwe BOT
Patatosha kweli
 
unakosea... jana hiyo hiyo on the spot liyumba alitoa nyaraka za mali yenye thamani ya bilion 55 na kwa sasa ni uhakiki tu wa mahakama unafanyika atatoka saa yeyote kuanzia sasa!!!! UKWASI HUO TUNAITA

Nadhani sasa ni muhimu kuwa na sheria/taratibu/ etc za kuelezea mali uliyonayo umeipataje na sio kuziandikisha tu tume ya maadili......ishu ni kuwa nani amfunge paka kengele kwa sababu majority ya watumishi wa umma ni wizi mtupu unaendelea miongoni mwao.
 
Hivi Ballali yuko wapi?yeye atakuwa anajua vizuri sana kuhusuina na haya.Hata kama tulizugwa amekufa si aliacha ushahidi kwa Mwanasheria wake?

Mie haingii akilini kuwa BOT walitumia zaidi ya billioni 221 bila ya ofisi hizi kufahamu.

1.Wizara ya fedha
2.Gavana wa Benki Kuu
3.Katibu Mkuu Kiongozi
4.Wakurugunzi wa bodi ya BOT
5.OFISI ya CAG



Umesahau, na OFISI YA RAIS
 
Haya majengo ni bonge la scandal. PCCB bila msaada wa hao wataalam waliopewa kazi ya kufanya ukaguzi itakuwa ngumu kuwatia mbaroni kina Liumba maana malipo yote alipewa mkandarasi moja kwa moja. watu wanajua ukweli wa kila kitu ni waliokuwa washauri wa ujenzi na mkandarasi mwenyewe.

PCCB ikiwa haijajipanga vizuri watarudi uraiani mda si mrefu. Technical Audit ya wataalam ni muhimu sana. Kujenga jengo lenye gharama ya US$ 8000 kwa mita ya mraba TZ ni ndoto, sijui liwe na nini. kuna mambo mengi yatagundulika kama uchunguzi na kesi vitaenda sawasawa
 
Mkuu mtindio yaani hii ya Liumba na mimi inanipa shida sana kuamini na akam ni hivyo ndivyo BOT inavyoendeshwa basi kuna haja ya kutengua the whole BOT uongozi na kuleta consultant hapo (ulaji mwingine.. lol) atutengeneee tructure ya kueleweka!!!!!

...Nyambala unaumiza kichwa nini........just check again "Director of Personnel and Administration"........halafu
1.kumbuka......yule jamaa aliyepelekwa Mwanza ilikuwaje
2.huyu bwana aliingia sana ktk procurements....consultants and the likes
3............

.......Nyambala......kwa mara ya kwanza huu mradi ulipokuwa unaanza gharama zake zilikuwa Billioni 40......Mkurugenzi wakati huo alikuwa Ndg Nyoni........wakati huo ukapigwa chini kwani gharama zake zilionekana kubwa..............cha kushangaza.....ukaja kupitishwa kwa gharama almost 10 times........na ndio maana unaona leo tuko mahakamani...........well.....once again KUDOS to the Government kwa hatua hiyo
 
Hawa jamaa si wataifishiwe mali zao tu kieleweke.
Mtu kala bilioni 200 na usheee duh akimpa hakimu bilioni 1 itakuwaje hapo agawane na wenzake.

Waziri mkuu alishajisemea hawa watu ni vigumu kuwashtaki. tehetehe
 
Back
Top Bottom