TOPU OFU ZE TEBO

Ni umahiri tu wa Martin Dubravka ndio umefanya Liverpool kufunga magoli 4 lakini siku nyingine yoyote basi inakuwa hata 7 kama sio 8 kabisa, kwa aina bora za nafasi walizotengeneza leo dhidi ya Newcastle

Kuna muda tunaongea sana kuhusu mifumo na mbinu lakini kuna vitu ambavyo ni muhimu sana vikifanyika kwa usahihi timu inakuwa imara uwanjani .... walivyofanya Liverpool leo
1: Runs nzuri sana kwenye spaces zilizo wazi ( Salah , Diaz , Darwin , Jones , TAA )
2: Kukabia juu haraka sana pale mpira ukipotea kwa idadi kubwa ya wachezaji ( risk sana lakini inalipa . Maana ukikabia juu sana maana yake nyuma unaacha walinzi wawili tu wa kati )
3. Pass and Move : achia mali halafu tembea kwenye nafasi ni ngumu sana kukabiliana nayo maana kama Newcastle unashindwa kujua nani yupo wapi wa Liverpool
4: Piga mpira golini unapopata nafasi ya kufanya hivyo badala ya kuongeza pasi ( stop overplaying )
Hivi vyote Liverpool walifanya kwa usahihi sana , mapungufu yalikuwa sehemu tatu tu leo kwao
1: Kuna nyakati kadhaa walikuwa wanapoteza mali kirahisi sana tena hata bila kwenye presha : Hasa Szobo : katika mechi kama tatu hivi amekuwa chini sana ya kiwango
2: Umaliziaji wao : hii inamuangukia Darwin Nunez nafasi kama tatu nzuri sana . Amuangalie mwenzake Alexander Isak
3: Walipokuwa wanakabia juu sana : TAA na Gomez nao wanasogea juu sana maana yake wanaacha space kubwa ambapo mara kadhaa Newcastle walipokuwa wanaishinda pressing ya Liverpool walikuwa wanatumia space ambayo wanaiacha TAA na Gomez .

Newcastle kiukweli leo ilikuwa ishu ya kucheza kwa matumaini , kwamba Dubravka kwenye ubora wake na wao wafunge magoli ya counter attacks au mipira iliyokufa .
NOTE
1: Gordon dribbling yake na kasi yake
2: Isak kama haendi vile kumbe anaenda aisee
3: Ile pasi ya Mo Salah kwenye goli la tatu " Outer Pass "
4: Luis Diaz leo nimeona kile kiwango kama alichokuja nacho
5: Jones kama alivyocheza dhidi ya Arsenal na leo hivyo hivyo
6:Martin Dubravka saves za leo

kapunguza sana idadi ya magoli
7: NIMEFURAHI ( mtajua wenyewe kwanini nimefurahi ushindi wa Liverpool )

wale wana kelele sana
FT: Liverpool 4-2 Newcastle
AMBANGILE