Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Huu ushindani kwasasa ni Mkubwa lakini hauwezi kudumu kwa miaka mingi kwasababu si ushindani wa Kitimu bali ni ushindani binafsi wa Pep na Klopp tokea Ujerumani.

Wakiondoka PEP na KLOPP tu pale EPL basi huu ushindani utapotea na kuwa mechi ya kawaida tu kama zamani.
 
Hili swali lingekuwa zuri sana kwenye post inayomjadili Mane. Kwenye hii niliwalenga Matip na Jota.

Kitu pekee ninachoona mimi ni kuwa Mane Kapungua uwezo wake na sio issue za Consistency.
So far this season Matip ndio amekuwa beki wetu bora wa kati. Makosa huwa yapo ndio lakini muda mwingine inasababishwa na unaocheza nao kushindwa ku provide enough cover (backup).

Kuhusu issue ya consistency napingana na wewe bado. Labda kama mimi sielewi maana ya hili neno.

Consistency ninavyoelewa mimi ni uwezo wa mchezaji ku deliver week in week out. Yani mchezaji anakuwa na impact katika team regularly kama Salah alivyo. Mchezaji anakuwa na return kubwa in terms of goal involvement in terms za kufunga goli, ku assist, key passes. Kama ni beki ni cleensheets n.k


Sasa huwezi kusema kuwa Mane kapungua uwezo na sio consistency. Form na consistency ni the same thing mkuu. Mchezaji anaefunga goli game mbili halafu akapotea game sita na kuja kufunga game moja tena na kupotea game nne huyo tunasema hayupo form/hana consistency. Meaning uwezo umepungua pia.

So huwezi kusema Jota hayupo consistency halafu useme Mane na consistency ila uwezo ndio umepungua.

Wote hawana consistency kabisa. Ndio maana wanafunga game mbili tatu wanapotea tena wanaibuka wanapotea tena. Tofauti na mtu kama Salah ambae week in week out ana deliver. Huyo ana consistency.

Labda kama mimi nakosea mnielekeze ndugu zangu.
 
Okay nimeelewa hapo sasa mkuu. Nadhani hii ni mbinu pia ya kulinda homegrown players.
 

Uwezo na Consistency ni vitu viwili tofauti Boss.

Gini Wijnaldum hakuwa na uwezo kama Pogba lakini alikuwa na Consistency for years, but Pogba ana uwezo mkubwa lakini ni mchezaji anayeongoza kutokuwa na Consistency.

Hivyo mane sio issue ya Consistency kwa mtazamo wangu bali Kapungua uwezo.
 
London yenyewe imekushinda kuitawala mpaka leo Arsenal ndio wanajiita wenye London ije kuwa ENGLAND mjusi Kafiri kweli wewe.
Jaribu uwaulize mashabiki wa Arsenal watakuambia ninani KING OF LONDON,Chelseafc inaziwakilisha timu za London vizuri sana nawewe unalijua hilo sema tu umeamua kujitoa ufahamu.
 
Duuuh noma sana bila TAA ki ufupi tunakua toothless kwenye attacking inakua hatuna consistency na kwa staili ya Klopp hua anatumia dynamic RB na LB kama ma winga timu inavyoshambulia hivyo kumtegemea Milner ni jipu aisee lazima tutakwama... TAA kwenye ku defend hayupo powa sana lakini kwa vile ni damu changa on his day hua anacheza vyema sana na pia kwa msaada wa Henderson inakua safi.

Liverpool tukicheza as a unit tunakua hatari sana ila mchezaji mmoja tu akiwa hayupo uwanjani basi tunapoteana kabisa na kusubiri individual glory design kama goli la Salah ooh my my..

Kwenda mbele lazima Klabu iingie sokoni kununua understudy wa TAA kama walivyofanya kwa Robertson kumleta Tsimikas ambae ameonyesha uwezo upo kabisaaa...

YNWA
 
Consistency kwako wewe ni nini?
 
Sure thing Captain. Hatuwezi kumtegemea Millie tena hasa ikiwa RB kwake ni makeshift position. Umri wake pia umeenda hawezi ku perform at the highest level ukitegemea yenyewe anapambana na vijana wachanga ambao wepesi sana na technically gifted.

Neco Williams bado anahitaji ku prove kuwa ana uwezo wa kufill in when needed.

As of now tunatakiwa kuingia sokoni tu tupate raw talent kama backup ya TAA kule RB.
 
Ukweli Mimi n mwanachesii damu damu lakini hii Liverpool hatuiwezi inatisha kama nini.. Huyo Salah sijui hata kwanini tulimuuzaga maana kwa sasa ndiye mchezaji bora ulaya anafunga kama kalogwa na mzigua ... Sasa lile pipa letu sijui kama litafikisha hata nusu ya goli za salah mwisho wa msimu... Sijui nihamie kwa majogoo maana nauhakika sisi Chelsea n wasindikizaji tu
 
Wewe nimamuruki tu,hakuna shabiki wa Chelsea kama wewe,wambie walikutuma kuwa tumekushitukia.
 
Umeamua kuweka silaha chini ...

League ngumu wewe ,wanaume tu ndio wanaweza[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Umeamua kuweka silaha chini ...

League ngumu wewe ,wanaume tu ndio wanaweza[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mi ni liver damu nimaamua tu niwakere ze blauzi [emoji1][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…