Ndugu wa Kop hivi yule assistant coach wa Klopp cjawahi kumwona anacheka aise. Anaitwa Brain buvac. Yeye hata timu ishinde 5 yy yuko serious tu. Yule jamaa mshawah kumwona?
TUMFAHAMU KIDOGO BRAIN BUVAC (KOCHA MSAIDIZI WA LIVERPOOL)
Jina lake la kwanza ni Zeljko likifuatiwa na Buvac. Ni m' Bosnia kwa utaifa na ndiye kocha wa kwanza msaidizi Liverpool ambako alijiunga mwaka 2015, mwezi wa kumi.
Buvac na bwana Klopp, ama Kloppo kama Buvac apendavyo kuita, wamekuwa marafiki wa karibu sana tangu wakicheza pamoja klabu ya FC Mainz kwenye mwanzo wa miaka ya 1990.
Huko (Mainz, na hata baadae Rudar Ljubija, Banja Luka, Rot Weiss Erfurt na Neukirchen) alikuwa kiungo mshambuliaji. Na alitundika daruga akiwa na miaka 36.
Kwenye timu yake ya mwisho kucheza, Neukirchen, ndipo alipoanza kuchukua hatua yake ya kwanza kwenye tasnia ya ukocha kabla hajaenda kuwa msaidizi wa Klopp kule Mainz mwaka 2001.
Lakini tuweke akilini kwamba, Buvac na Klopp waliweka nadhiri ya kwamba baada ya kutundika daruga basi watajihusisha na kazi ya ukocha. Na hivyo basi kwakuwa walikuwa wameshibana sana, wakaweka pia nadhiri ya kwamba kati yao, yeyote yule atakayekuwa wa kwanza kupata kazi ya ukocha, atamuita mwenzake awe msaidizi wake. Hiko kiapo kinaishi mpaka leo hii.
Pale Klopp alipotoka Mainz kwenda Borussia Dortmund, akaenda tena na mfuasi wake huyu, mwaka 2008.
Ilikuwa kwenye ground ya Westfalenstadion ndipo philosophy ya Klopp na Buvac ikachanua. Makombe ya Bundesliga mwaka 2011 na 2012 yakawafanya watu wawarushie macho makocha hao na kuwapa heshima inayostahiki.
Mwaka 2013, Borrusia Dortmund ikiwa kama timu inayocheza mpira mzuri na wa kuvutia Ulaya, walifika fainali na Buyern Munich ingawa bahati haikuwa kwao wakasogezwa kando.
Buvac aliungana na Klopp kwenye kuikacha Dortmund msimu wa mwaka 2014 - 15, lakini mapema akachepukia Liverpool na bwana Klopp wakitumai kuendeleza mafanikio yao.
Na July 8, Liverpool ilitangaza Buvac ameungana na Klopp pamoja na Krawietz kwenye kusaini mkataba mrefu na Liverpool.
KUHUSU U 'SERIOUS' WAKE.
Kwa namna moja ama nyingine, Buvac huonekana ni mtu mtulivu asiye na papara. Makini na asiyependa kupanua mdomo wake pasi na sababu shinikizi. Hulka yake hii imetengeneza ukuta fulani na wachezaji.
Inasemekana pale Buvac anapoongea jambo, huwa basi lina mkazo ndani yake. Ni mkali, kuliko Klopp. Na muda mwingine pale ambapo Klopp anakuwa 'frustrated' ama 'mad' basi hapo ndipo Buvac huchukua fursa kuwapa 'kavu' wachezaji. Au pale Klopp anapokuwa speechless, ama kuremba maneno, Buvac basi hupaka rangi halisi.
Hili limekuwa likiwasaidia kutimiza na kufanya kazi yao vizuri zaidi kutokana na kamgawanyo haka ka madaraka mbali tu na kupeana maoni, mawazo na maono.
BUVAC THE BRAIN, OR THE RIGHT HAND.
Kwa mujibu wa Klopp, Buvac kwake ni ubongo kwani humtegemea sana kwenye mawazo. Ila hili Buvac amekuwa halishabikii sana japo anali 'appreciate'.
Na kuthibitisha zaidi hili, amekuwa pia akimuita mkono wake wa kuume, kumbuka si wa kushoto. Hivyo basi waweza kuona ni kwa namna gani wanategemeana.
Kwa mujibu wa Nuri Sahin, mchezaji aliyewahi kupata huduma ya Klopp na Buvac, asema ya kwamba: hakuna tofauti yoyote kati ya Buvac na Klopp. Namna Klopp anavyouona mpira basi ndivyo Buvac hufanya vivyo hivyo. Hilo amelishuhudia walipokuwa timu moja kiasi kwamba hata pale Klopp alipokuwa anaadhibiwa kwa kuwekwa nje ya uwanja, uwepo wa Buvac unajaza nafasi barabara!