Masiya
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 7,602
- 7,344
Star TV wangetumia kanuni zinazofanana na za Bunge naona mheshimiwa mmoja angetolewa nje mapema sana. Kama unaamini watu unaowaongoza wanakuona mnyonge kazi iliyobaki ni kuwaonyesha kwa kutumia madaraka yako wewe si mnyonge hivyo si ajabu kwa hulka ya binadamu ukapindisha kanuni. Hasa kama ni wapinzani wako. Hali inakuwa mbaya zaidi unapokuwa si msikilizaji mzuri na una jazba ya karibu. Haya yote tumeyaona leo. Patamu zaidi ni pale unapokumbuka kuwa nafasi yako ya kesho inategemea chama chako na ukionyesha uvumilivu inaweza ikala kwako kama ilivyokula kwa 6.
Kwa style hii "Bunge la Katiba" kama litakwenda kwa kanuni za sheria iliyopitishwa tutegemee vurugu zaidi au kususiwa na makundi fulani. Ikitokea hivyo tutakuwa na katiba ya wa Tanzania?
Kwa style hii "Bunge la Katiba" kama litakwenda kwa kanuni za sheria iliyopitishwa tutegemee vurugu zaidi au kususiwa na makundi fulani. Ikitokea hivyo tutakuwa na katiba ya wa Tanzania?