Live Star TV: John Mnyika na Job Ndugai

Live Star TV: John Mnyika na Job Ndugai

Leo Ndugai ameonyesha udhaifu mkubwa sana,sijui nani kamshauri akubali huu mjadala wakati hajajiandaa,angetafuta ujanja ufanyike siku nyingine akiwa na nondo za kutosha,

Leo hakuwa na wale wazee wa ndioooo wanaompa support anapofanya ujinga wake,na huwa anatoa kauli za kujihami huu ndio udhaifu mkubwa leo amethibitisha hilo,


Akiwa mtetezi wa matendo ya ccm, hakuna cha nondo wala nyaraka za utetezi, dhambi na udhalimu wa ccm, viongozi na nk ni mambo yaliyowazi kabisa utayatetea kwa namnagani.......kuendelea kudanya zaidi na zaid? hawezi.......vinginevyo nikuonekana chizi zaidi....
 
Kiukweli uwezo wa Ndugai ni mdogo sana anashindwa kujifunza hata kwa bi mkora au Jenister..... Mwanaume anapaniki kirahisi hivi.

kwakweli watu wamejionea jinsi alivyo dhaifu.
 
Ndugai unapenda kuogopwa, kuheshimiwa na kuabudiwa wakati hana sifa hizo.!!
 
Mtazuungusha maneno tuu lkn chanzo cha tatizo hilo ni Mh mbowe kwa nn alikataa kutii amri iliyomtaka kukaa chini kwanza? anafahamu muongoza mjadala ni spika na lazima uwepo ustaarabu , alichokifanya mh mbowe alikuwa anajuwa matokeo yake ili wapate sababu ya.kushindwa kwao kujadili muswaada huo. lkn mbinu hz chafu zina mwisho wake ama watakapo kuwa madarakani ama watakapokuwa wanaendelea na upinzani. cdm chama ambacho.kinqjipatia umaarufu kwa nji ya hira na wananchi wengi hawajatambua hilo wanawaunga.mkono pasipo kujuwa na madhara yake hayataonekana leo lkn ipo cku watu watajuwa mbivu na mbichi.
 
Big up mh.Mnyika,umeonyesha uwezo wako mbele ya media na si tu bungeni.huyu mh.Ndugai kwa tunaomjua wala hatupi shida na anayozungumza.
 
Nimecheka sana...eti ndungai anasema mnyika haeshimu kaka zake...!!
 
Katika kujibu hoja leo, Mnyika kamuacha mbali sana ndugai. Kama vile kuwalinganisha kiuwezo Messi na Ngasa yaani Mnyika ni Messi na Ndugai ni Ngasa.
 
Mtazuungusha maneno tuu lkn chanzo cha tatizo hilo ni Mh mbowe kwa nn alikataa kutii amri iliyomtaka kukaa chini kwanza? anafahamu muongoza mjadala ni spika na lazima uwepo ustaarabu , alichokifanya mh mbowe alikuwa anajuwa matokeo yake ili wapate sababu ya.kushindwa kwao kujadili muswaada huo. lkn mbinu hz chafu zina mwisho wake ama watakapo kuwa madarakani ama watakapokuwa wanaendelea na upinzani. cdm chama ambacho.kinqjipatia umaarufu kwa nji ya hira na wananchi wengi hawajatambua hilo wanawaunga.mkono pasipo kujuwa na madhara yake hayataonekana leo lkn ipo cku watu watajuwa mbivu na mbichi.

chanzo cha tatizo tumekiona leo labda kama wewe peke yako ndio haukuona hilo. ndungai kadhihirisha kuwa ana inferiority complex kabisa.
 
MH. NDUGAE amepokea MEMO na kuna wakati alikuwa akisoma jambo kwenye simu yake. Kama mahojiano haya yamemwelemea kiasi cha kuhitaji ''busta'' je, katika kuongoza bunge tukufu inakuwaje? Kama kashindwa kumhimili mtu 1 je wale mia tatu na zaidi inakuwaje?
 
Wana JF,Habari za asbh,kwa ss Ndugai na mnyika ndio wapo studio za star tv .na Ndugai anawasifia srar tv kuwa ndio kituo cha habari number moja Tz kwa maoni yake.

Mura ndugai hana kitu kabisa
 
Ingenoga zaidi kama na KUB Mbowe angekuwepo. Baadhi yetu tulitaka kufahamu kisa cha yeye kukaidi amri halali ya kumtaka akae alioitoa NS Ndugai.
 
dah,nimekosa uhondo leo.nilikuwa church ila jf kuna watu makini nimefuatilia hapa.
ila nimegundua chadema kuna watu makini sana na sijafanya makosa kui support!
 
Back
Top Bottom