Live Star TV: John Mnyika na Job Ndugai

Ndugu MoD"s nashindwa kujuwa kwanini nimekuwa banned ..


Huu ni mwendolezo wa uonevu mkubwa unaoendelea hapa jamvini .....sababu ya kunifungia mnasema nimeandika ****** .....sasa sijui hapo ni makosa gani nimefana kiasi kuwa hayahitaji hata ONYO ....Kama utaratibu wa kawaida ....hivi hata mkiwaeleza members wengine kuwa mmemfungia mtu kwa sababu hiyo utaeleweka ...
Inawezekana kabisa katika baadhi ya makabila yetu kukawa na makosa tunayoweza kufanya bila kuyajuwa .....mfano ukitoa karatasi hapa ukiwapa wanafunzi IMLA ,,,,kuna maneno watu wanaweza kuandika kutokana na madhara ya mother tongue.....mfano REMMY Watu wataandika LEMMY...RAIS ni LAISI..
Sisi kwetu mtu ukimuambia aandike kitu kinachoishia na I....Wengi wataandika Y...sasa kama tutakuwa tunaadhibiana kibabe namna hii HII NI HATARI KIASI KUWA INAASHIRIA ULE UHURU ULIOKUWA HUMU NDANI LABDA UMEISHA ...AU TUMESHAUZWA BILA KUJIJUWA KWA WATU AMBAO WANAJIAMULIA TU KUFUNGIA WATU BILA KUFUATA UTARATIBU ..
Wakati mwalimu nyerere [nyelele] anaaongelea juu ya azimio la Zanzibar alipata kusema kuwa ...."wenzetu baada ya kutoka zanzibar ...wakaanza kufanya mambo ambayo hayaendani na Azimio la Arusha..basi wenye akili tukajuwa tayari...."
Sasa msitake kutupa mashaka kama tunaanza ku bann watu bila hata kutaka ufafanuzi .....uliona ugumu gani kuni PM na kuniuliza.." mkuu unamaanisha nini uliposema ******" ....mimi to be honest mpaka naona huu ujumbe wa ban ...ndio nimeenda kwenye website ya bunge na kuangalia jina la Ngugay kwa makani nikakuta kuwa linaandikwa NDUGAI...Ifahamike kuwa mimi mnanijuwa ningetaka kuandika kwa nia ya kumkashfu nisingemungunya maneno na wala nisingeshangaa sana kwa hili..


Mimi naona sasa ma MoD Aidha wanatumia madaraka vibaya au kuwa wengine ambao wanatumika kugandamiza uhuru humu ndani kinyume kabisa na MISINGI na MILA za JF....Ifahamike kuwa sio kazi ngumu baadhi ya watu au makundi kuwaweka baadhi ya ma MoD kwenye payroll ...kama watashindwa kuinnunua JF nzima kimsimamo....


Siandiki kuomba kufunguliwa ..la asha ...bali nawataka tu mtafakari hili..na kujitazama kama kweli mlitenda haki...na iwapo itawapendeza basi mnaweza kuamua mpendavyo ....,hata ikibidi kuniondoa kabisa humu .!!!!


Nawasilisha !!


Wenu katika uwazi na kulipenda Taifa!


MKUU PM.
 
Back
Top Bottom