Live Star TV: John Mnyika na Job Ndugai

Live Star TV: John Mnyika na Job Ndugai

Wabunge wa CDM wawapo bungeni wanawakilisha maslahi ya chama badala ya wananchi; Mnyika amewasahau wana Ubungo awapo bungeni
 
Katika kipindi cha Tuongee asubuhi cha Star Tv kikibeba mada ya Vurugu bungeni, Naibu spika Job Ndugai amesema wabunge wa upinzani wanachokifanya ni usanii mbele ya kamera wawapo bungeni kwani majadiliano huanzia kwenye kamati ambako hukubaliana vuzuri!
Mnyika namwona anamtolea jicho meza moja!


im not so sure if he is competent enough.
 
Kiongozi mzuri lazima awe mvumilivu wa hoja za wenzio kwa hiyo ndugai si.......................
 
kweli nimeamin kua kada wa ccm kama ww unatakiwa uwe na akili ya maiti
Kamanda inawezekana hata wazazi wako walikuwa na akili za hivyo Chadema imeundwa miaka 22 iliyopita.
 
Muda wote Mnyika amekuwa kimya wakati Ndugai akichangia,ila Mnyika akiongea anamkatisha na kutaka kuendelea kuchangia.Nadhani Nduhai ni Kiongozi dhaifu asiye na uvumilivu.Na,ndio maana wapinzani wanapokuwa wanataka kuchangia hoja ambayo kwa CCM ni mwiba hatoi nafasi.Hili limejidhihirisha hata wakati mahojiano yanaendelea yeye anaingilia kati na kuvuruga hoja ya mpinzani wake.Watanzania wa leo sio wa mwaka 1922,hata wale ambao walikuwa hawaoni leo hii wanaona na wanatambua kuwa ipo siku moja nchi hii hataongozwa na CCM.Wanachojaribu kifanya ni kupindisha mambo kwa manufaa yao wenyewe na kwa ajili ya ulinzi wao wa baadae.Haina shida,hoja itapita ila CCM mkae mkijua siku upinzani ukiingia Ikulu na kuwa na Wabunge wa kutosha,mtafute pa kwenda.Maana vifungu vipofu na visivyoona vitafumuliwa.
 
Umeona eeeehhh. Dogo alikuwa wa kwanza kitaifa 2000. Alafu kama nlisikia wanaleta taarifa kuhusu origin ya Ndugai, mbona kama wameichunia?
 
Mtangazaji wa upande wa Dar amepwaya sana, wakati Ndugai akiongea Mnyika ananyamaza ila akipewa Mnyika nafasi Ndugai anamkatisha kuongea.

Hii inaonyesha wazi kuwa Ndugai anapenda sana Ubabe ndio maana anashindwa kuongoza Bunge. Halafu anadai kuwa eti huwa anajiona kwamba Wabunge wa Upinzani wanamuona Dhaifu.

Kama tu leo pale Star Tv Ndugai ameshindwa kuonyesha uvumilivu wa kumpa Mnyika nafasi ya kujibu hoja zake wakati yeye akipewa kuongea Mnyika ananyamaza,je unadhani inakuaje pale bungeni anapokua kakalia kiti?
 
Mkuu Ritz leo mjadala wa hawa jamaa ni mzuri tatizo la viongozi wetu ni kukosa uvumilivu. Yale yanayotokea hapa kwenye mjadala kuingiliana katika mazungumzo ndio yaleyale kule bungeni. Kejeli pia ni tatizo sana linalopelekea wabunge wetu kuparamiana. Kuna hoja moja ya msingi aliuliza mtangazaji kuwa huwa wabunge wengi waupinzani wanatumia mbinu ya kumchokoza kiongozi mtawala ili areact na hatimaye kupoteza tention katika mambo ya msingi na kuhamia kwenye majibizano yasio na tija. Hapo Mnyika alipinga na Ndugai akadai ni kweli hiyo mbinu ndio wanayotumia wapinzani. Ndugai amewaomba wapinzani pamoja na yote lakini wajaribu kuwaonea huruma wapiga kura wao kwani bungeni si mahala pa kufanyia siasa bali kujadili mambo muhimu yanayoathiri maisha ya mtanzania. Hata hivyo kipindi kimekwisha kwa malumbano kama yaleyale ya bungeni.

Nyie ndo mnapaswa kuwaonea huruma wanannchi kwa kutokuwatendea haki kila mahali!
 
Last edited by a moderator:
Magamba wanafanana wote... Hata nape alibanwa na nyika huyo huyo akaanza kutukana.. Hawana hoja kabisa
 
Ngugai mbona anamuingilia Mnyika? Alafu naona ata mtangazaji anampa muda mdogo Mnyika! Alafu Ndugai Kama amepanic vile!?

Ndugai asije akajisahau akamtoa nje Mnyika...!! Huyo jamaa akishapanic anakuwa kama kichaa....!
 
yaani sijaufulahia hata kidogo kwani ndugai alikuwa anaingilia katika ya hoja ya mnyika.na mwenyekiti(mtangazaji)sijui alikuwa anamwogopa kumkataza asiingilie hoja ya mnyika?!mimi binafsi sijafulahi hata kidogo kwani ndugai naona kwenye midahalo mingi anakosa uvumilivi hasa pale wengine wanapo wakilisha haja zao yeye anaingilia kati.
Kiboko yake alikuwa mh Lisu maana kuna wakati walikutano hapo star tv..alipokuwa akiingilia lisu anamwambia naomba uniache nimalize..subiri zamu yako..ndugai anavimba ila anakuwa kimya!
 
Namkubali sana Ndugai anajenga hoja ni mtu makini.

Samahani sijui km niliangalia vizuri km jibu ni ndiyo kwa mtazamo wangu NDUGAI alikuwa anajibu BAADHI ya hoja za Mnyika na kumkatiza katiza hoja na ushahidi aliokuwa anataka utoa
 
Jamani jamani..... Ningekuwa ndungayi ningeomba pooo...... Hii sasa ni aibu tupu kakamatwa vibaya hadi hafurukuti
 
Mh Ndugai umeonyesha ni jinsi gani ulivyo mbabe huko Bungeni ndivyo unavyoshindwa hata kuheshimu muda wa mwenzio kuchangia mjadala japo kuwa umetumia muda wako vizuri kwa kuongea upuuzi.Hongera sana mh Mnyika kwa uwezo wako mkubwa wa kupanga hoja vilivyo,nimeamini ccm haina watu makini,leo Ndugai amefurahi kipindi kilivyofika tamati!
 
Back
Top Bottom