Live on ITV - UZALENDO: Dr Slaa vs Mangula

Status
Not open for further replies.
Kwanza, kipindi kinaonekana kutoleta tija ya aina yoyote ile kutokana na kupotosha dhana nzima ya "uzalendo". Uzalendo kamwe haufungamani na siasa. Uzalendo ni kitendo cha kuipenda nchi yako kwa moyo wako wote, na kutaka kuitumikia pamoja na wenzako, bila kujali itikadi za kisiasa, dini, rangi au kabila. Jambo ambalo ni muhimu ni kwamba mzalendo huithamini sana nchi yake na kila kilicho chema ndani yake. Kile kibaya, mzalendo wa kweli atajaribu kupunguza athari zake kwa ushauriano na wahusika. Mzalendo mara nyingi na ucha Mungu ambapo huwa hana hofu ya kupoteza maisha yake akitetea haki, amani, upendo na mshikamano nchini mwake. Maneno ubaguzi, udini, rushwa na ufisadi hayana nafasi moyoni mwake. Kazi yake yeye ni kuyapinga tu!

Pili, nikikifanyia tathmini ya awali kipindi hiki, ninachokibaini ni kwamba, kwanza, kipindi hiki hakina tofauti na kipindi cha mahojiano cha "Dakika 45", ambacho kimebainika kuwa kipindi cha "kuwapa promo" watendaji wa Serikali, na pili, uongozi wa ITV umeona kwamba kipindi hicho hakina maslahi na kuamua kukikacha, na kuleta kipindi kingine chenye maudhui ya kisiasa.

Tatu, nikiwa nawafahamu vema wanahabari wenzangu, ambao wengi wao ni wazembe wa kufanya utafiti wa kina kabla ya kubuni vipindi, ni dhahiri kwamba kipindi hiki cha "Uzalendo" tayari kimeshindwa malengo yake, hata kabla ya kuenda hewani kwa mara ya kwanza. Iwapo kina mdhamini, dhahiri haitachukua mwezi mmoja kabla ya mkataba wake kuisha, kwani aliyemwuzia mdhamini huyo hakumpa undani wake, au alidhindwa kufikisha ujumbe, au ujumbe ulitafsiriwa katika namna tofauti kuliko ilivyokusudiwa na kumfanya mdhamini kukubali kukidhamini.

Kama "mbunifu" wa kipindi hicho angekuwa na hata chembe ya ubunifu, angemfuata swahiba yangu, mtu ninayemheshimu kwa weledi wake, ambaye licha ya kusingiziwa mabaya lukuki, bado anapeta, Mheshimiwa Mzee Dunstan Tido Mhando, ambaye sasa, kama sikosei, ni Afisa Mtendaji Mkuu au Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited, inayomiliki magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Spoti Starehe.

Kaka Tido, kama anavyojulikana, japokuwa ni mtu wa makamo ya wastani, umri uliokwenda kiasi, na busara tele, ni mtu ambaye ukienda kumwona lazima uwe umejipanga. Si mtu wa kuendekeza siasa, propaganda wala chuki. Tangu uongozi wa Nation Media umnyakue, amefanikiwa kuyaimarisha magazeti yote ya MCL kiasi cha kufikia kiwango cha kimataifa.

Mbunifu wa kipindi hicho, dhahiri alitafuta njia nyepesi zaidi badala ya weledi. Kashindwa kuitambua hazina ya Taifa tuliyonago katika Kaka Tido, halafu anakuja na ----- huu usio na kichwa wala miguu?

Dada yangu Joyce? Hivi kweli you cant come up with something better than that? If I wasnt indisposed I would have offered my services for half my price. Too bad. You cant have me. Your program has failed before it goes on air.

Uelewa na uzoefu wangu katika fani hizi za uandishi wa habari, ambapo, licha ya kuwa na kipaji cha kuzaliwa cha uandishi, nimeisomea fani hii ya Journalism nchini Marekani, ambapo pia nilipata fursa ya kufanya kazi kwenye Print, Radio na Television media, kwa zaidi ya miaka 3 kabla ya kuhitimu mafunzo yangu ya Economics, Journalism na Computer Science.

Sikufikia kiwango cha Master of Science. Nina Bachelor of Science.

Lakini watendaji wengi wa leo kwenye media institutions wana kiwango cha Master of Science, au MBA au MA. Kinachostaajabisha ni kiwango chao duni cha kufikiria na utendaji.

Hivi kweli inaingia akilini kwamba, kwa kuwa watu kama Dr. Slaa na Philip Mangula ni watu mashuhuri katika siasa nchini, basi ndio watakuwa na mvuto wa kutosha kuwakamata watazamaji?

Tuwaachieni wanasiasa wafanye kazi yao kwenye majukwaa sahihi, kama vile Mchakato Jimboni, ambacho kiliwaumbua wagombea wengi wa upinzani wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010. Kipindi hiki, kama sikosei, kilibuniwa na Tido Mhando, huku mwendeshaji wake akiwa Shaaban Kissu, ambaye sasa anasikika zaidi kwenye redio ya TBC Taifa. Changamoto za redio hiyo ni nyingi kiasi kwamba nikianza kuzizungumzia ni makala nyingine.

Ushauri wangu kwa ITV ni kwamba, kama mnataka kuzungumzia siasa, nendeni mitaani mkawahoji watu kisha mkawaonesha luningani. Badilisheni jina la kipindi kuwa "Alama za Nyakati", jina ambalo lina mvuto mkubwa zaidi. Mtafanikiwa. Watu wanataka kujiona luningani. Wanaona fahari. Hawataki kuwaona wanasiasa wakilumbana kwenye hoja ambazo, pengine, kwa sasa, hazina haja kwao. Hatujafika 2015 tayari kampeni zimeanza na michezo michafu nayo...

Dada yangu Joyce Mhaville, una weledi mkubwa katika tasnia hii. Kwa nini unakubali kuburuzwa na kuingia katika mambo ambayo hayana tija kwako? Kama ni mdahalo, waachieni Vox Media. Ninyi kachimbeni hoja za wananchi. Mengi mtayapata.

Joyce, surely you can do better! N'est-ce pas? Je dit: Bien sur!
 
View attachment 105205

1:00 USIKU leo alhamisi Usikose kuangalia kipindi kipya kabisa cha UZALENDO kikuhusu mambo yanayojiri katika medani ya siasa nchini na waalikwa wakiwa wanasiasa kutoka vyama tofauti wakichambua hoja mbalimbali kuhusiana na hali inavyoendelea nchini.Katika kipindi cha leo tutakuwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Bwana Philp Mangula na Katibu Mkuu wa Chadema,Dk.Wilbroad Slaa

Mbona hujaelezea ni channel ipi?
 
Baada ya hapo watuletee wafuatao;
Mwigulu Nchemba vs Zitto Kabwe
Nape Nnauye vs John Mnyika.

FREEMAN MBOWE vs..................!?
TUNDU LISSU. vs................!?
GODBLESS vs.....................!?
HALIMA MDEE. vs..............!?
PETER MSIGWA. vs...........!?
JOSHUA NASSARI. vs........!?
JOSEPH MBILINYI(SUGU) vs......!?
VICENT NYERERE. vs..............!?
EZEKIEL WENJE. vs..................!?
HAINES KIWIYA. vs.................!?
SAIDI AMOR ARFI vs..............!?

Na wengineo wengi. Mwenye kuweza kujaza nafasi zilizo wazi pls naombeni ajaze! Nina uhakika kwa CCM hakuna tena wa kupambana na hawa niliowataja hapo juu.km yupo niambiwe!
 
Nani kakwambia Tido anafanya vizuri MCL? zamani kabla yake magazeti ya mwananchi yalisomwa maeneo mengi nchini the same day tena asubuhi sawa na Dsm lakini sasa mathalani mza wanasoma jioni saa 12 wkt kuna ndege, usimpe shavu tido anaiua Mcl.
 
Mbona unakuwa si mzalendo kama kipindi kiitwavyo? Kama uongo usipost kama ukweli sema channel, watu tuna uchungu na nchi hii...

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
FREEMAN MBOWE vs..................!?
TUNDU LISSU. vs................!?
GODBLESS vs.....................!?
HALIMA MDEE. vs..............!?
PETER MSIGWA. vs...........!?
JOSHUA NASSARI. vs........!?
JOSEPH MBILINYI(SUGU) vs......!?
VICENT NYERERE. vs..............!?
EZEKIEL WENJE. vs..................!?
HAINES KIWIYA. vs.................!?
SAIDI AMOR ARFI vs..............!?

Na wengineo wengi. Mwenye kuweza kujaza nafasi zilizo wazi pls naombeni ajaze! Nina uhakika kwa CCM hakuna tena wa kupambana na hawa niliowataja hapo juu.km yupo niambiwe!

mbowe+(wasira),
lissu/nchimbi
lema/lusinde
mdee/bulaya
msigwa/bulembo
nassari/makamba
mbilinyi/nkamia
nyerere/membe
wenje/mabula;Airo lameck
kiwia/msolla,filikunjombe, dr kamani
arfi/pindi chana, jenista mhagama, steven massele
sema lingine leta orodha yako ya akina saanane nk.
 
kinarushwa teleivision gani au redio gani pls niambie nataka niwahi toka ofisini ili niangalie
View attachment 105205

1:00 USIKU leo alhamisi Usikose kuangalia kipindi kipya kabisa cha UZALENDO kikuhusu mambo yanayojiri katika medani ya siasa nchini na waalikwa wakiwa wanasiasa kutoka vyama tofauti wakichambua hoja mbalimbali kuhusiana na hali inavyoendelea nchini.Katika kipindi cha leo tutakuwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Bwana Philp Mangula na Katibu Mkuu wa Chadema,Dk.Wilbroad Slaa
 
kinarushwa teleivision gani au redio gani pls niambie nataka niwahi toka ofisini ili niangalie

Wewe ni mmoja wa mnaorudisha maendeleo ya kazi zenu nyuma.
Angalia muda wa kazi una cheza na jf. unawahi kufunga ofisi kisa udaku.
 
Wadau tunaomba tupeane updates muda ukifika.Tupo mbali na tv!
 
Mi nikajua kinaonyeshwa azam tv. Ntakuwepo kumiangalia rais wangu ajaye dr wa ukwe'e. Mia
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom