niko uwanjani hapa makamanda wanagonga viroba hatari, nasikia vimetoka kiwandani kwa sugu vinaitwa DEIWAKA GIN.
ccm si mnamiliki viwanda vya konyagi na nyie muwape ili waje kwenye mikutano yenu nje na hapo basi mtakuwa wajinga kwa kuandika porojo
niko uwanjani hapa makamanda wanagonga viroba hatari, nasikia vimetoka kiwandani kwa sugu vinaitwa DEIWAKA GIN.
Ngojea tusikie porojo za dj sasa
......anzeni kufungasha wenye nchi wanakuja
Wakuu.
Kama kawaida, muda huu tunafanya mkutano wa amsha amsha hapa makao makuu ya kanda ya Magharibi Tabora, kanda hii inaundwa na mikoa ya kigoma, Katavi na Tabora.
Mkutano huu ni maalum kwa ajili kuamsha hamasa ya kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.
Yanayojiri
- Ukiingia unakutana ma sura ya kilio cha umaskini ccm wameuwa kilimo kwa kuuwa viwanda vya nguo mfano Mwatex.
- Wakulima wa Tumbaku na pamba kwenye maeneo mengi ya Tabora leo hawana matumiani tena ya kuendelea na kilimo, kinana alikuja hapa akalia kinafiki leo matatizo ya wakulima yako palepale.
- Kikwete anaachia dhahabu anapewa vitabu vya Shule badala ya kuifanya dhahabu itunufaishe tununue vitabu wenyewe.
- Ccm wanasubiri UKAWA tuvurugane au tutengane, hatutengani kamwe tunataka kwa pamoja kwa umoja wetu tutatue matatizo ya watanzania.
- Matatizo ya watanzania ndio yametuunganisha pamoja baada ya kusimamia maslahi yao bungeni. Na sasa tunaenda kusimamisha mgombea mmoja kwenye kila nafasi wakati wa uchaguzi.
- UKAWA hatugawi vyeo tunagawana majukumu. Sisi Chadema tutakuwa wa mwisho kuhujumu UKAWA.
Kuhusu kujiandikisha.
- Kila kijana aliyeoko hapa uwanjani ahahakikishe yeye na vijana wenzake 20 wanaenda kujiandikisha na kuhakikisha watu wote wenye sifa za kupiga kura wanajiandikisha zoezi litakapo anza rasmi kwenye mkoa wa Tabora.
- Vijana wa Tabora huu ni wakati wenu wa kufanya mageuzi ya kweli katika nchi hii, na hamuwezi kufanya mageuzi ya kweli kama hamtajiandikisha na kwenda kupiga kura na kuzilinda kura. Lazima mjue kuwa hakuna mtu wa kuwaletea mageuzi kwenye mkoa wenu kwenye nchi yenu bali ni nyinyi wenyewe. Kujiandikisha ni lazima ili mageuzi hayo yatokee.
- Vijana wenzenu wa Njombe walikomaa na wengine walikua wanaamka usiku wa manane kwenda kupanga foleni vituoni ili wajiandikishe. Na nyinyi anzeni kujipanga mhakikishe mnaamshana usiku muwahi kwenda kupanga foleni mjiandikishe. Hakuna kulala kwenye hili zoezi. Kujiandikisha ni nini.... Lazima
- Utamaduni wa kujaza nyomi kwenye mikutano yetu lazima sasa uendane na mujibu ya uchaguzi. Wengi hamkuwa na sifa sasa hivi fursa imekuja. Lazima tuitumie.
Nitawajuza zaidi...
Hapo hamna fisi wala watu walio bebwa na malori Kinana ameona hiyo?? Jamani yule jamaa aliye wahi msituni alikuwa anawasaidia ccm sana watu kwenda kucheza taarabu. sasa sijui mwaka huu itakuwaje?? Au ndiyo style ya fisi??
Mkuu Mohamed Mtoi, asante kwa hii...
zile T-shirt na kofia, na ile shibe ya mlo wa siku moja, ndio the magic!, na sio umati!.
All the best katika amsha amsha, only isije kuwa, badala ya kuamsha, amsha, ndio kwanza mnawaamshia!.
Pasco
kwa hiyo huniamini au?
Ngojea tusikie porojo za dj sasa
View attachment 232750