Mohamedi Mtoi
R I P
- Dec 11, 2010
- 3,321
- 6,331
Wakuu.
Kama kawaida, muda huu tunafanya mkutano wa amsha amsha hapa makao makuu ya kanda ya Magharibi Tabora, kanda hii inaundwa na mikoa ya kigoma, Katavi na Tabora.
Mkutano huu ni maalum kwa ajili kuamsha hamasa ya kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.
Yanayojiri
- Ukiingia unakutana ma sura ya kilio cha umaskini ccm wameuwa kilimo kwa kuuwa viwanda vya nguo mfano Mwatex.
- Wakulima wa Tumbaku na pamba kwenye maeneo mengi ya Tabora leo hawana matumiani tena ya kuendelea na kilimo, kinana alikuja hapa akalia kinafiki leo matatizo ya wakulima yako palepale.
- Kikwete anaachia dhahabu anapewa vitabu vya Shule badala ya kuifanya dhahabu itunufaishe tununue vitabu wenyewe.
- Ccm wanasubiri UKAWA tuvurugane au tutengane, hatutengani kamwe tunataka kwa pamoja kwa umoja wetu tutatue matatizo ya watanzania.
- Matatizo ya watanzania ndio yametuunganisha pamoja baada ya kusimamia maslahi yao bungeni. Na sasa tunaenda kusimamisha mgombea mmoja kwenye kila nafasi wakati wa uchaguzi.
- UKAWA hatugawi vyeo tunagawana majukumu. Sisi Chadema tutakuwa wa mwisho kuhujumu UKAWA.
Kuhusu kujiandikisha.
- Kila kijana aliyeoko hapa uwanjani ahahakikishe yeye na vijana wenzake 20 wanaenda kujiandikisha na kuhakikisha watu wote wenye sifa za kupiga kura wanajiandikisha zoezi litakapo anza rasmi kwenye mkoa wa Tabora.
- Vijana wa Tabora huu ni wakati wenu wa kufanya mageuzi ya kweli katika nchi hii, na hamuwezi kufanya mageuzi ya kweli kama hamtajiandikisha na kwenda kupiga kura na kuzilinda kura. Lazima mjue kuwa hakuna mtu wa kuwaletea mageuzi kwenye mkoa wenu kwenye nchi yenu bali ni nyinyi wenyewe. Kujiandikisha ni lazima ili mageuzi hayo yatokee.
- Vijana wenzenu wa Njombe walikomaa na wengine walikua wanaamka usiku wa manane kwenda kupanga foleni vituoni ili wajiandikishe. Na nyinyi anzeni kujipanga mhakikishe mnaamshana usiku muwahi kwenda kupanga foleni mjiandikishe. Hakuna kulala kwenye hili zoezi. Kujiandikisha ni nini.... Lazima
- Utamaduni wa kujaza nyomi kwenye mikutano yetu lazima sasa uendane na mujibu ya uchaguzi. Wengi hamkuwa na sifa sasa hivi fursa imekuja. Lazima tuitumie.
Kwa muhtasari hoja zilizo ongelewa kwenye mkutano huo.
1. Mwelekeo wa kuandikisha wapiga kura kwenye mfumo wa BVR
2. Kura ya maoni na msimamo wa UKAWA kususia kura hyo
3. Maandalizi ya UKAWA kuelekea uchaguzi Mkuu
4. Kuimarisha Ulinzi na Usalama wa Chama na msimamo wetu kuhusu vikosi vya Res brigade na Blue Guards vya CUF
5. Hatma ya Kilimo cha Tumbaku na serikali kutochukua hatua dhidi ya ufisadi wa Bodi ya Tumbaku.
Msisitizo mkubwa Ulikuwa kwenye hamasa ya kujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi mkuu.