live: Mkutano wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga

live: Mkutano wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga

Wakuu.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Kamanda Freeman Mbowe, akiongozana na viongozi kutoka makao makuu pamoja na wabunge wa Kanda ya Ziwa Mashariki, punde wanaelekea kwenda kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Shinyanga, eneo la Nguzo nane, Mahakama ya Mwanzo, ni baada ya kikao cha ndani kilichomalizika muda mfupi uliopita.

Ni sehemu ya mikakati ya kuimarisha kanda hiyo ambayo ni kati ya ngome kubwa za CHADEMA.

UPDATES:

• Meshack Opulukwa: kama kuna mikoa inaombea na ina hamu kubwa uchaguzi mkuu ufike haraka wafanye mabadiliko makubwa kuiondoa CCM ni Shinyanga na Simiyu. Wananchi wameshachoka na kushindwa kwa CCM!

• Chombo chochote kikitumika sana kinaingia uchakavu. CCM imeshaingia uchakavu, haiwezi tena kutumika kuleta ukombozi wa maendeleo. Kwa kauli ya Pinda maana yake ni kwamba mihimili 3 haina maana kwa serikali ya CCM. Anasema chama cha magamba, chama cha wezi kimeamua kuwateketeza na kuwatelekeza wakulima wa pamba. Haiwezi tena kuwatetea. Kazi hiyo inafanza na CHADEMA, waiunge mkono.

Updates combination chini ya Tumaini Makene itawajuza.

Kijana naona unatembea sana kwa ustawi wa chama.Hongera sana.Songea to Shinyanga.
 
Heche anahimiza vijana kujiandikisha na kypiga kura ili tuache mfumo wa hovyohovyo
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1374329433414.jpg
    uploadfromtaptalk1374329433414.jpg
    116.4 KB · Views: 148
  • uploadfromtaptalk1374329486625.jpg
    uploadfromtaptalk1374329486625.jpg
    97 KB · Views: 144
Kodi ya simu ni mbaya kwani wewe mama mpika chapati, muuza mchicha , mama ntilie, wanafunzi watalipa sawasawa na Mengi, Bakharesa, Dewji , wabunge, Rais, ........Heche.
 
Aliyeko mbele apige picha aziupload m niko nyuma siwezi sogea mbele niko na baiskel yangu haina kufuli naogopa kuiacha ila watu n wengi mbaya
 
CHADEMA hakuna kulala mpaka watu waelewe ubovu wa serikali iliyoko madarakani. CCM imetufikisha pabaya jamani..
 
Kamanda wa Anga kaanza kumwaga sera uwanja wa nguzo 8 umejaa anaanza kwa kushukuru wananchi kwa kuja na pia anawapa Waislamu hongera kwa swaumu
 
Ngoja nikukaushie,nitapigwa ban bure





QUOTE=Apolonary;6876585]Kazi njema, na ulinzi uimarishwe. Mwenyekiti wa cdm ni zaid ya mwenyekiti[/QUOTE]
 
Baada ya hapo kesho mnatoa tamko makamanda la kususia katiba si ndiyo eee.
 
Anahimiza uhusiano mzuri baina ya Watanzania bila kujali itikadi zetu.... Tunatakiwa tutafakari mambo ysnayoligusa Taifa. Mtu wa chama kingine sio adui bali mwanaCDM fanya kazi atuelewe tunahitaji kura yake. Tusijadili itikadi bali tujadili mustakabali wa nchi yetu
 
Mbona picha hamna au leo mnahutubia watoto wa shule wekeni hata za mwaka 2010 make hii aibu wakuu.
 
Kamanda wa Anga kaanza kumwaga sera uwanja wa nguzo 8 umejaa anaanza kwa kushukuru wananchi kwa kuja na pia anawapa Waislamu hongera kwa swaumu
Mafunzo ya jeshi letu kasema yataanza lini wakuu ile red bregad.
 
Anaongelea shambulio la Arusha anasema mlipuko ulikuwa mchana kweupe na walishambuliwa kwa silaha nne, mabomu, risasi za moto smg, bastola na mabomu ya machozi je kosa lao ni lipi?
 
Back
Top Bottom