live: Mkutano wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga

live: Mkutano wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga

ukombozi unagarama yake, cdm na mboye tupo nyuma yenu
 
Leo kuna mkutano wa hadhara wa chadema mkoa wa shinyanga katika viwanja vya mahakama nguzo 8 majengo. Mgeni rasmi ni mwenyekiti wa CDM Taifa mh. Freeman Mbowe... Sasa tunasubiri mkutano uanze huku tukiburudishwa na gwaride la red brigade
shukran kwa taarifa kiongozi.
vipi hawa hapa chini wakoje huko?
avatar44815_4.gif
 
Mbona kimya mkuu? Ukiona tumetulia ujue tunakusikiliza,ukisikia minongono ujue tunachoka kusubiri.
 
Kweli mwaka huu CHADEMA mmeamua kila siku ni harakati tu, sijui mnapata wapi muda wa kuweza kupumzika?
Hivi majimbo yenu huwa mnayahudumia saa ngapi, maana kila siku mpo na mikutano, mijadala, maandamano, mahakamani, midahalo nk?
 
Watanzania wanaitaji kusikia chadema mnalipi jipya la kuwaambia sio kelele ya uchochezi na kuwagombanisha watanzania.
 
Leo kuna mkutano wa injili mkoani shinyanga mgenj rasmi Mch freeman mbowe asanteni.
 
Mbona wengine wanasema yupo Mbeya. Nyie Magwanda mbona mnajichanganya sana.
 
Kweli mwaka huu CHADEMA mmeamua kila siku ni harakati tu, sijui mnapata wapi muda wa kuweza kupumzika?
Hivi majimbo yenu huwa mnayahudumia saa ngapi, maana kila siku mpo na mikutano, mijadala, maandamano, mahakamani, midahalo nk?

Hao wenye muda mbona nao hawaishi kulalama? Si umesikia huko kwa Mngoshi Makamba nako kumenuka licha ya kwamba hafanyi maandamano? Au hujasikia pia timua timua ya wa-Masai Korogwe na Handani licha ya kwamba huko porini hayajui maandamano?

Muulize Wasira CHADEMA itakufa lini?
 
Mmechokwa mmesuswa na mmedharauliwa. Watz hawadanganyiki, wanakiamini chama kilichowajengea barabara, shule, vyuo vikuu na hospitali kila kijiji
 
Watanzania wanaitaji kusikia chadema mnalipi jipya la kuwaambia sio kelele ya uchochezi na kuwagombanisha watanzania.
Mkuu CHAMVIGA inaonekana wananchi wengi wanapenda kuwasikiliza hao CHADEMA haijalishi ni nini wanakisema, maana kila kukicha watu wanazidi kujaa kwenye hiyo mikutano yao.
 
Last edited by a moderator:
Benson Kigaila ndo anaongea kufungua mkutano anatambulisha makamanda. Red brigade wamejipanga kikazi zaidi hadi sasa sijaona polisi
 
Back
Top Bottom