Kumbe chenji ya radi CCM iliahatumia zamaaniii
Hapa tunazungumzia uzalishaji kobello we mchumi wa wapi?
Mkulima wa mpunga kule kilombero, mbarali, pawaga, shinyanga na mkulima wa mahindi kule songea, sumbawanga na maeneo mengine anahitaji pembejeo bora za kilimo, anahitaji scheme za umwagiliaji ili asiendelee kulima kwa kutegemea kudra za mwenyezi Mungu, anahitaji mabwana shamba wa kumshauri ili alime kitaalamu. Huyu mkulima hata sasa analima kwa kutumia jembe la kukokotwa kwa ng'ombe na anavuna mazao mengi tu lakini yanashindwa kufika sokoni kwa sababu ya miundombinu mibovu ya barabara.
Element ya mafuta hapa ni ndogo sana katika mchakato mzima wa uzalishaji na hivyo haiwezi kamwe kuwa kikwazo katika uzalishaji wa chakula. Kinachotakiwa hapa kiko so obvious hata mtu asiye mchumi anaelewa tu kwamba tunahitaji kuwekeza vya kutosha katika kilimo, as simple as that. Hatuhitaji kununua mafuta mengi (bulk procuremnt) ili kuzalisha mazao ya chakula.