Live ITV mada: Bajeti ya 2012/2013 je imekidhi matarajio ya wengi??

Dr. Mwakyembe aunga mkono bajeti, awakebei wapinzani na awafananisha na mashabiki wasiojua wa mpira wanaopenda kukosoa wakiwa nje ya uwanja.
 
Hapa tunazungumzia uzalishaji kobello we mchumi wa wapi?
Mkulima wa mpunga kule kilombero, mbarali, pawaga, shinyanga na mkulima wa mahindi kule songea, sumbawanga na maeneo mengine anahitaji pembejeo bora za kilimo, anahitaji scheme za umwagiliaji ili asiendelee kulima kwa kutegemea kudra za mwenyezi Mungu, anahitaji mabwana shamba wa kumshauri ili alime kitaalamu. Huyu mkulima hata sasa analima kwa kutumia jembe la kukokotwa kwa ng'ombe na anavuna mazao mengi tu lakini yanashindwa kufika sokoni kwa sababu ya miundombinu mibovu ya barabara.

Element ya mafuta hapa ni ndogo sana katika mchakato mzima wa uzalishaji na hivyo haiwezi kamwe kuwa kikwazo katika uzalishaji wa chakula. Kinachotakiwa hapa kiko so obvious hata mtu asiye mchumi anaelewa tu kwamba tunahitaji kuwekeza vya kutosha katika kilimo, as simple as that. Hatuhitaji kununua mafuta mengi (bulk procuremnt) ili kuzalisha mazao ya chakula.

Kuwekeza kivipi?
Kilimo kinahitaji efficiency ya hali ya juu. Na huwezi kuongelea efficiency bila kuhusisha energy.
Umesema mazao yanakosa soko, si wakulima wangetembea na magunia yao mpaka sokoni? .... swala la energy linahusika hapa pia.
Kwa idadi ya watu wanaoshiriki kilimo, tunazalisha kidogo mno, wenzetu walioendelea (ahum! ahum!) ni asilimia chache tu ya wakulima wao wanaweza kuwalisha.
Kama mafuta yangekuwa nusu ya bei ya sasa, maisha yangekuwa ahueni kwa watu wengi tu na bei za bidhaa zingekuwa chini pia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom