Mambo tarajiwa bajeti ya serikali mwaka wa fedha 2023/24

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Serikali inasoma baieti vake ya mwaka wa fedha 2023/2024 leo. Bajeti hivo ni ya majumuisho itaonyesha makadirio ya jumla ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha ujao.

Majumuisho yanatokana bajeti za kisekta ambazo kwa kiasi kikubwa ndiyo zinabeba mipan-go inayotaraiiwa kutekelezwa na Serikali katika kipindi hicho cha mwaka mmoja wa fedha.

Kuna mambo kadhaa tunayoweza kuyatarajia kuwa yataakisi katika bajeti ya 2023/2024 na hapa nitagusia zaidi yanayoweza kujitokeza katika afya, elimu, kilimo, na udhibiti wa fedha katika programu za uwezeshaji.

Wengi tunatarajia kuwa bajeti itaakisi mwendelezo wa kutoa huduma za afya na uboreshaji, kulingana na vipaumbele vya Wizara ya Afya kwa mwaka ujao wa fedha; itaonyesha msisiti-Zo wa kutenga kiasi cha fedha kutoa huduma za kinga dhidi ya maradhi, ikiwamo huduma za chanjo.

Vile vile matarajio ni kuona bajeti inaimarisha upatikanaji na ubora wa huduma za afya zinazotolewa na vituo vya umma, upatikanaii na udhibiti wa dawa, vifaa, vifaa tiba, kuimarisha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto na mengine. Hivyo, kama bajeti itaweza kuakisi mambo hayo katika sekta ya afya wananchi wataona huduma imeboreshwa.
Katika elimu kuna mambo mawili makubwa tunaweza kuyatarajia kuwa bajeti itaelekeza nguvu zake ili
kuyafanikisha, ambayo yote msingi wake ni kuboresha ubora wa elimu, kukuza maarifa ya kujiajiri na ujuzi.

Kwanza
, kukamilisha mtalaa mpya wa elimu na mafunzo katika shule za msingi, sekondari na vyuo vya kati ambao mchakato wake tayari unaendelea. Utelekezaji wa jambo hilo unaweza kusadia kuongeza ubora wa elimu kwa kuimarisha maarifa na ujuzi miongoni mwa wahitimu wangazi mbalimbali na kupungu-za changamoto ya ukosefu wa ajira, hususani kwa kundi la vijana miongoni mwa Watanzania.
Pili, tunatarajia bajeti itaelekeza nguvu kwa kuweka mafungu katika utelekezaji wa miradi ya miundombinu ya kusomea, kama ukarabati wa shule za sekondari, kufufua vyuo vya ufundi; kuongeza vifaa vya kujifunzia na kufundishia, kuboresha vyuo vya ualimu, ujenzi wa karakana na kusimika vifaa na mitambo ya kujifunzia mafunzo ya ufundi stadi.

Upande wa kilimo bila shaka bajeti itaweka msisitizo na kuelekeza nguvu katika kufanikisha miradi ya maendeleo ya kilimo na hasa ili kuzalisha chakula, ajira na kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.
Hili linatokana па mambo mawili.

Kwanza, vipaumbele kwa mwaka wa fedha 2023/24 ambao Serikali imedhamiria kuongeza tija na uzalishaji kwa kuweke za katika utafiti wa mbegu bora na udongo, uzalishaji wa mbegu na miche bora, kuwekezaji katika huduma za ugani, utoaji wa ruzuku ya mbolea, na uwekezaji kwenye ukarabati wa miundom binu ya umwagiliaji.

Pili, ni bajeti inayokuja katika kipindi ambacho dunia inapitia changamoto zinazoathiri uzalishaji, kwa mfano mabadiliko ya tabianchi na vita vinavyoendelea kati ya Ukraine na Russia vinaathiri uzalishaji, upatikanaji na bei za vyakula sehemu mbalimbali duniani.

Hali hiyo inajenga msingi mzuri kwa bajeti ijao kutarajia inaweza kuonyesha msisitizo na kutenga mafungu ya kutelekeza miradi muhimu kwa sekta ya kilimo nchini.

Katika udhibiti wa mapato na matumizi ya fedha, bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/24 inaweza kuja na utaratibu mpya kuhusu utoaji na uhakiki wa mikopo inayotolewa na Serikali kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Kwa mwaka wa fedha ujao, Serikali inaweza kuanzisha utaratibu mpya wa utoaji wa mikopo hiyo kupitia benki ili kuongeza ufanisi na kuzuia mianya ya upotevu.
 
Back
Top Bottom