Lissu, wasomi duniani kote hawafanyi hivyo

Lissu, wasomi duniani kote hawafanyi hivyo

Ndo kawaida yenu... haya embu cheki kauli hizi..!!



1. Mtakula nyasi lakini ndege ya Rais lazima inunuliwe (MRAMBA)
2. Ukitaka kula inabidi ukubali na wewe kuliwa (J Kikwete)
3. Foleni Dar ni ishara ya maisha bora (J Kikwete)
4. Hata mimi sielewi kwa nini Tanzania ni maskini! (J Kikwete)
5. Ningekuwa mvua ningenyeshea mabwawa (J Kikwete)
6. Wafanyakazi hata wakigoma miaka 100 ila mshahara kima cha chini 350,000 haiwezkani (J Kikwete)
7. Wanafunzi kupata mimba ni viherehere vyao (J Kikwete)
8. Acheni wivu wa kike (MSEKWA)
9. Asiyeweza nauli mpya kwenda kigamboni apige mbizi (MAGUFULI)
10. Baada ya kutumia helikopta ya jeshi kwenda kwetu urambo mlitaka nipande punda(KAPUYA)
11. Wabunge wa Dar wanafikiri kwa kutumia makalio(Dr Didas Ma------)
12. Mnaniuliza mvua kwani mimi waziri wa mvua?(WASIRA
13. Posho za wabunge lazima zipande kwa sababu maisha ya Dodoma yapo juu (Spika Makinda)
14. Wakati huu ambapo nchi inakabiliwa na janga la njaa nawashauri wakulima wahifadhi hata pumba maana zinaweza kusaidia (John Malecela)
15. Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe - Cleopa Msuya
26. Wapinzani wanapenda mambo ya ovyoovyo wanafiki hawa wataendelea kuwa wapinzani tu (Samwel Sita)
17. Graduates msio na kazi fugeni kuku biashara hiyo inalipa sana (Mwantumu MAHIZA)
18. Tanzania ni muungano wa visiwa viwili, Tanganyika na Zimbabwe (Philip Mulugo)
19. Siongei na mbwa mi naongea na mwenye mbwa (Juma Ngamia)
20. Hakuna Rais atakayetoka Kaskazini (Ridhiwan Kikwete)
21. Mbowe amekuja hapa kajamba-jamba halafu kaondoka (Seif Khatib)
22. (Billioni 1.2) - Hivyo ni vijisenti tu (Andrew Chenge)

Haya ewe Nyumbum, hizo nazo Ripoti za Tume?
 
Kuna mwanasheria mmoja msomi alipokuwa akijibu hoja bungeni alimwita mbunge mwenzange tumbili nitamkata kichwa,humohumo bungeni wengine wanawaita wenzao wezi na wengine walishawahi kujibu hoja za bajeti ya wapinzani kwa kutupa kitabu cha wapinzani chini na kuita takataka,kwa Lugha kama hizi na vitendo kama hivi sijui wanataka upande wa pili watumia lugha gani kujibu lugha kama hizi zisizokuwa na sitaha.
 
Misukule kamwe hawatakaa wa mwelewe Lissu msomiii
 
....Kuna kiongozi mmoja yeye aliwaita watanzania wenzake karibia milioni 6 MALOFA....
Sasa ndio umeandika nn hapa??
kwa hivyo kama huyo kiongozi ni msengerema na lisu nae atakuwa msengerema?!
alafu huoni kwamba huyo kiongozi aliyewaita wa tz malofa enzi zake zishapita tofauti na akina lisu ambao bado wanasaka dola?!
 
Ujue mara nyingi wapinzani wanakuwa na hoja nzuri tu kwenye mambo mbalimbali shida ni kutoa mawazo yao kwa jazba na lugha chafu. Mwishowe wanaharibu ladha yote ya hoja zao.

"Ripoti ya Mchanga it is Rubbish! Rubbish!" Lissu (2017).Ni mfano mmoja miongoni mwa mingi.

Hauwezi ukawakosoa wasomi wenzako kwa kutumia lugha za namna hii. Haikubaliki dunia nzima. Wasomi hukosoana kwa hoja lakini kwa lugha zenye staha. Mfano huwezi kumuambia mtafiti, mchunguzi, au mtoa ripoti kuwa "ripoti yako ni upuuzi mtupu" badala yake unatakiwa umuambie ripoti yako ina upungufu mkubwa n.k

Kwa hiyo ni vizuri kuwa makini na utumiaji wa lugha unapowakosoa wasomi wenzako, vinginevyo hata kama una hoja ya msingi utapuuzwa.
Kulemba lugha!
 
Una hoja nzuri sana, sasa naomba uniambie kama kweli rais amejua kila kinachoendelea mbona wote tunajua hiyo mikataba ni mibovu kwanini asisimashe na hiyo mikataba kabisa? Ni kweki kuzuia michanga ni vizuri ila mbona ni kama anazuia risasi kwa debe. Una mikataba mibovu kisha unakomaa tu na mchanga huoni hapo hata hao wazungu wanatuchora? Ni kipi kinamshinda rais kuiweka hiyo mikataba wazi ikajadiliwe bungeni kama ana nia njema?
Swali lako litajibiwa na ripoti ya pili ya kisheria hapo kesho........
 
Ujue mara nyingi wapinzani wanakuwa na hoja nzuri tu kwenye mambo mbalimbali shida ni kutoa mawazo yao kwa jazba na lugha chafu. Mwishowe wanaharibu ladha yote ya hoja zao.

"Ripoti ya Mchanga it is Rubbish! Rubbish!" Lissu (2017).Ni mfano mmoja miongoni mwa mingi.

Hauwezi ukawakosoa wasomi wenzako kwa kutumia lugha za namna hii. Haikubaliki dunia nzima. Wasomi hukosoana kwa hoja lakini kwa lugha zenye staha. Mfano huwezi kumuambia mtafiti, mchunguzi, au mtoa ripoti kuwa "ripoti yako ni upuuzi mtupu" badala yake unatakiwa umuambie ripoti yako ina upungufu mkubwa n.k

Kwa hiyo ni vizuri kuwa makini na utumiaji wa lugha unapowakosoa wasomi wenzako, vinginevyo hata kama una hoja ya msingi utapuuzwa.

Lissu siku ya kwanza alisema anamponheza Rais kwa at least kuliona la mchanga, lakini tatizo siyo Mchanga,kwenye mchanga wamemdanganya tunaibiwa kwenye sheria na mikataba Mibovu.

Wakamponda.ndipo akasema.hata hiyo report ya Mchanga ni rubbish kwa.kuwa tunaibiwa minara ndani ya Migodi yenyewe, hao wajina Mruma wanajua tunaibiwa wpaimHao walipiandika hiyo report specifically Mruma alikuwa muajiriwa wa Kampuni kubwa ya Madini kama Geologist Director, na kwa kawaida ya wazungu board directors wanapewa na shares za Kampuni husika.

Kampuni aliyekuwa ameajiriwa ni Kampuni Mpinzani wa Acacia, tuna uhakika gani analindwa shares za kampuni aliyoajiriwa.nayo toka 1997-2014?

Hivi tumeshajiuliza kwanini iwe.mchanga usiwe dhahabu??Hivi tumeshajiuliza kwanini mpaka Leo Kalemani hajatumbuliwa ilihali alikuwa State Attorney wa Nishati na Madini na ndiye muandishi wa Mikataba hiyo mibovu??Na yeye pia kama Mruma walikuwa directors kwenye the same company,hivi tumeshindwa kuoanisha.number hapa??

I wonder siku tukienda Mahakamani tukapigwa mtamlaumu Lissu kwanini hakuwashauri.
 
Kweli ni Rubbish wala hakukosea..Lisu kiboko ya mabashite yote!,wapi profesa wa karatasi..
Subiri Jtatu Raisi anasema usicheze mbali na TV yako ili unyanyue makwapa ya kumshangilia vizuri
rubbish
 
  1. Lissu hajasoma ripoti husika, na hata angekuwa ameisoma;
  2. Lissu siyo mtaalam wa sayansi ya miamba wala madini; na kama bado hujaelewa,
  3. Hao unaosema kuwa ni 'wataalam' walioshangaa maudhui ya riporti ya Prof. Muruma, hujasema ni akina nani na walifanya uchunguzi gani kuthibitisha utaalam wao.
Kama hivyo basi, hitimisho lako unalosisitiza kwenye bandiko lako linabebwa na msingi (locus stand) gani? Unapaswa kuelewa kuwa Tanzania haijawahi (hakuna ushahidi wa takwimu) kufanya comparative study ya kiasi cha dhahabu tulichonacho dhidi ya mataifa mengine kama Canada, Australia, Afrika Kusini, Ghana, Chile, DR Congo wala Mali. Unachoelezwa kuwa Tanzania ni nchi ya nne kwa kuwa na wingi wa dhahabu Afrika ni tathmini zinazofanywa na wachimbaji wawekezaji wenyewe na kisha kusambaza takwimu hizo kulingana na mikakti yao ya kibiashara/uwekezaji. Miaka kabla ya 2009 walikuwa wakisema Tanzania ni nchi ya tatu Afrika (nyuma na Afrika Kusini na Ghana) kwa kuwa na dhahabu nyingi. Baadaye (2010 na kuendelea) wakasema Tanzania ni nchi ya nne nyuma ya Afrika Kusini, Ghana na Mali kwa kuwa na wingi wa dhahabu. Kwa hiyo, ni mtu mjinga tu asiyejua political economy za TNEs na beneficiaries wao ndie anaweza kusema eti, 'haiwezekani Tanzania ikwawa na madini kiasi kinachotajwa kwenye ripoti ya Prof. Mruma (mtaalam wa jiolojia/miamba ya madini) ka kuwa wataalam wa Acacia wamesema kuwa haiwezekani!

Sophist,simuamini.kabisa Mruma kabisa to say the truth. Mruma alikuwa geologist Director wa Kampuni kubwa ya madini iliyowekeza pia hapa Bongo.Mruma alipewa na shares kulingana na sheria za wenzetu Board Directors wanapewa na shares kwenye kampuni husika,toka 1997 -2014 alikuwa wapi kusema jamani tunaibiwa??

Je si hawa walikuwa wanasafirosha madini yetu toka migodini na walikubaliana kabisa na wawekezaji,hivi baada ya miaka yote ya kuramba asali leo anakuwa na ngonjera ati kwenye mchanga kuna dhahabu nyingi mbona simuelewi??

Hivi uzalendo unaanzia pale unapokosa ulaji??Na zile shares ameshadeclare??Alishadeckare kwamba alikuwa muajiriwa.wa kampuni Mpinzani wa acacia?Hivi Acacia wakisema jamaa alikuwa wanatetea shares zake ili kuua kiuchumi acacia tuna hata cha kujitetea??

Ninachukia waongo mmoja wapo ni Mruma na Kalemani w atueleze kwamba kwanini walifanya walichofanya.

Lissu anasema ukweli hiimijitu ni miongo tu inataka tushtakiwe wakati kulikuwa na njia mbadala ya kupata hata kule kwenye minara ya dhahabu.
 

Waberoya hata hao akina Mruma na Kalemani ni rubbish walitakiwa kuwa jela by now.

Hao wote walikuwa madirectors 1997-2014,leo wanatueleza kitu gani??Hivi Kalemani si alikuwa State Attorney huko wizara ya Nishati na Madini?Ilikuwa je akapewa u director kwenye makampuni ya madini baada tu ya kusaini Mikataba??

Kaka yangu tumeshajiuliza hayo??Ni wakati Watanzania kuacha uvyama kujiuliza maswali mengi zaidi.Mpaka Leo Kalemani ni Waziri kuna nini huko??
 
Lissu saying it as it is. Calling a spade a spade. Safi sana ripoti bila shaka yeyeto ni takataka kabisa.
 
Kwa watu wenye ujuzi na fani ya miamba wanajua ukweli halisi na ndio maana wengi wao walishangaa hiyo report kama kweli hiyo copper concentrate ina madini kiasi kile!! Kwa dunia hii migodi ingekuwa iko nafasi ya juu sana!! Ndio maana lisu alitumia lugha kali kiasi kile kwani masuala ya kitaalam ni kosa kubwa kuweka siasa
Kumbuka sampling ilifanywa ndani ya makontena ... Yaaani kilichomo mule wataalamu Wã analytical chemistry walikuwepo pia... Lisu hajui hata kuandika equation anakwambia rubish ..??


Sampling haukifanywa huko kwenye miamba bali ndani ya Yale makontena .. Na ndicho wanachosafirisha
 
Ujue mara nyingi wapinzani wanakuwa na hoja nzuri tu kwenye mambo mbalimbali shida ni kutoa mawazo yao kwa jazba na lugha chafu. Mwishowe wanaharibu ladha yote ya hoja zao.

"Ripoti ya Mchanga it is Rubbish! Rubbish!" Lissu (2017).Ni mfano mmoja miongoni mwa mingi.

Hauwezi ukawakosoa wasomi wenzako kwa kutumia lugha za namna hii. Haikubaliki dunia nzima. Wasomi hukosoana kwa hoja lakini kwa lugha zenye staha. Mfano huwezi kumuambia mtafiti, mchunguzi, au mtoa ripoti kuwa "ripoti yako ni upuuzi mtupu" badala yake unatakiwa umuambie ripoti yako ina upungufu mkubwa n.k

Kwa hiyo ni vizuri kuwa makini na utumiaji wa lugha unapowakosoa wasomi wenzako, vinginevyo hata kama una hoja ya msingi utapuuzwa.
Sasa kakosea nin lisu kweli ni Rubbish Rubbish kweli kweli kama raisi anania njema na nchi hii atoe mwelekeo na msimamo wa serikali kuhusu mikataba ya madini na waliosaini wachukuliwe hatua Kali ili iwe fundisho vingine ni upuuzi tu unaoendelea kutafuta kiki sababu ashajua udhaifu wa watanzania.
 
Wale ni maprofesa kwel ila kwa sabab mkulu yupo nyuma yao hawatumii akili yao na hivyo wanakuwa leproffeselee
 
Back
Top Bottom