- Lissu hajasoma ripoti husika, na hata angekuwa ameisoma;
- Lissu siyo mtaalam wa sayansi ya miamba wala madini; na kama bado hujaelewa,
- Hao unaosema kuwa ni 'wataalam' walioshangaa maudhui ya riporti ya Prof. Muruma, hujasema ni akina nani na walifanya uchunguzi gani kuthibitisha utaalam wao.
Kama hivyo basi, hitimisho lako unalosisitiza kwenye bandiko lako linabebwa na msingi (locus stand) gani? Unapaswa kuelewa kuwa Tanzania haijawahi (hakuna ushahidi wa takwimu) kufanya comparative study ya kiasi cha dhahabu tulichonacho dhidi ya mataifa mengine kama Canada, Australia, Afrika Kusini, Ghana, Chile, DR Congo wala Mali. Unachoelezwa kuwa Tanzania ni nchi ya nne kwa kuwa na wingi wa dhahabu Afrika ni tathmini zinazofanywa na wachimbaji wawekezaji wenyewe na kisha kusambaza takwimu hizo kulingana na mikakti yao ya kibiashara/uwekezaji. Miaka kabla ya 2009 walikuwa wakisema Tanzania ni nchi ya tatu Afrika (nyuma na Afrika Kusini na Ghana) kwa kuwa na dhahabu nyingi. Baadaye (2010 na kuendelea) wakasema Tanzania ni nchi ya nne nyuma ya Afrika Kusini, Ghana na Mali kwa kuwa na wingi wa dhahabu. Kwa hiyo, ni mtu mjinga tu asiyejua political economy za TNEs na beneficiaries wao ndie anaweza kusema eti, 'haiwezekani Tanzania ikwawa na madini kiasi kinachotajwa kwenye ripoti ya Prof. Mruma (mtaalam wa jiolojia/miamba ya madini) ka kuwa wataalam wa Acacia wamesema kuwa haiwezekani!