Lissu, wasomi duniani kote hawafanyi hivyo

Lissu, wasomi duniani kote hawafanyi hivyo

Anatatizo hilo huyo bwana mdogo tangu utoto wake. Nakumbuka wakati wa kuchunga ng'ombe. Tumemchapa sana ili abadilike lakini tumeshindwa.

Usipoteze muda sasa keshakuwa mtu mzima. Unataka kukunja samaki mkavu?
 
Ujue mara nyingi wapinzani wanakuwa na hoja nzuri tu kwenye mambo mbalimbali shida ni kutoa mawazo yao kwa jazba na lugha chafu. Mwishowe wanaharibu ladha yote ya hoja zao.

"Ripoti ya Mchanga it is Rubbish! Rubbish!" Lissu (2017).Ni mfano mmoja miongoni mwa mingi.

Hauwezi ukawakosoa wasomi wenzako kwa kutumia lugha za namna hii. Haikubaliki dunia nzima. Wasomi hukosoana kwa hoja lakini kwa lugha zenye staha. Mfano huwezi kumuambia mtafiti, mchunguzi, au mtoa ripoti kuwa "ripoti yako ni upuuzi mtupu" badala yake unatakiwa umuambie ripoti yako ina upungufu mkubwa n.k

Kwa hiyo ni vizuri kuwa makini na utumiaji wa lugha unapowakosoa wasomi wenzako, vinginevyo hata kama una hoja ya msingi utapuuzwa.
Sound good
 
Tundu Lissu tayari amekuwa msemaji wa Acacia.
Ni aibu kwa msomi kama huyu kutoa kauli za kejeli kwa Rais Magufuli katika masuala yanayohusu maslahi ya taifa.
Hata kama serikali inakosea kuna njia ya kusahihisha sio kwa lugha za kejeli.
Bora watuibie tu maslahi gani ya taifa ambayo wanafaidi wachache Na wataendelea kufaidi wachache
 
Ile report ni total rubbish kwa sababu ilipeawa jina la ripoti ya kitaalam japo haikukidhi vigezo vyovyote vya kitaalam. Minerla Analysis gani huwa haina QAQC report?
Nadhani ilisomwa summary ya report hatujui report kwa ujumla wake.

Mambo ya Quality Assurance na Quality Control report Nategemea yatakuwepo tu.
 
Mimi sina shida na content, hata kama ina kasoro kiasi gani, ishu lugha. Kuna aina ya lugha mtu ukishafikia hatua fulani haupaswi kuzitumia
Mkapa ulishamwambia naye kwa umri na hadhi yake hakupaswa kutumia lugha za makuli na wavuta bangi?
 
Sii kosa nikibashiri kuwa wewe "ndiwe"

Acacia wamesema hivii, laiti kama report ya mruma ingekuwa kweli basi wao acacia ndio wangekuwa wazalishaji/wachimbaji wenye kuuza/kuchimba/kuzalisha dhahabu kwa wingi zaidi duniani.

Taarifa/tamko la Acacia halijasema wala kupendekeza kuwa tanzania ingekuwa na dhahabu nyingi zaidi kuliko nchi zote duniani.

Pole mruma!!! Mmeiingiza nchi kwenye mgogoro mzito na mnaomba tuwaunge mkono kwenye ujinga wenu wa kisomi.
Umepungukiwa taarifa, maarifa na uwezo wa kuchambua sera/matamko. Kampuni ya Acacia imewekeza nchini Tanzania peke yake. Hauna nchi nyingine duniani utaweza kukuta kampuni inaitwa Acacia ambayo sehemu ya Acacia yetu inayoendesha migodi ya Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara. Kwa hiyo kampuni hiyo ikisema kuwa ndio ingekuwa kampuni pekee kubwa kuzalisha dhahabu duniani, maana yake ni kuwa Tanzania ndio ingekuwa nchi ya kwanza duniani kuzalisha dhahabu. Umeelewa?
 
Tundu ni mpuuzi na kichaa anaevaa suti, hana sifa ya kuwa mwanasheria kwa sababu hakuna mwanasheria anayejadili hoja kwa jazba labda awe mwehu tu kama Tundu
Kosa halirekebishwi kwa kosa,kama Tundu ametukama wewe usitukane maana anayemalizia hulipwa mara saba, mtoa hoja ametoa hoja nzuri kwa ajiri ya kurekebishana kwa upole,wewe umetumia lugha kali ambayo mtoa mada anasihi isitumike katika mijadala.
 
Too much words. Hata hakimu atakae hukumu hiyo kesi hatakuwa mtaalam wa miamba,

Ita hitaji mtaalamu wamiamba kuandaa, lakini kuisoma, kuelewa na kuihukumu si kazi ya wataalamu pekeyao,

Hata anaye kabidhiwa na kuisoma Kwa dakika5, kisha kuisemea na kuamua si mtaalamu wa miamba.

Mtaalamu Mkuu wa miamba mwenyewe kasha fukuzwa Kwa report hiyo.
Nani alikuongopea kwa majaji hawatakiwi kuwa wataalam katika maeneo ya kitaalam kuhusiana na kesi wanazozisikiliza na kisha kuzitolea hukumu?
 
Umepungukiwa taarifa, maarifa na uwezo wa kuchambua sera/matamko. Kampuni ya Acacia imewekeza nchini Tanzania peke yake. Hauna nchi nyingine duniani utaweza kukuta kampuni inaitwa Acacia ambayo sehemu ya Acacia yetu inayoendesha migodi ya Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara. Kwa hiyo kampuni hiyo ikisema kuwa ndio ingekuwa kampuni pekee kubwa kuzalisha dhahabu duniani, maana yake ni kuwa Tanzania ndio ingekuwa nchi ya kwanza duniani kuzalisha dhahabu. Umeelewa?
Usitumie akili za ccm kuelewa.

Rejea tamko la acacia, ni kwamba:-
Kama kiwango cha dhahabu anazodai professor mruma kipo kwenye ule mchanga, ingemaanisha jumla ya dhahabu wanayochimba wao hapa tanzania ingekuwa nyingi kuliko mchimbaji yeyote duniani.

Hakikisha hesabu hazikupigi chenga ndipo ushupaze mshipa kubishana.
 
Sophist,simuamini.kabisa Mruma kabisa to say the truth. Mruma alikuwa geologist Director wa Kampuni kubwa ya madini iliyowekeza pia hapa Bongo.Mruma alipewa na shares kulingana na sheria za wenzetu Board Directors wanapewa na shares kwenye kampuni husika,toka 1997 -2014 alikuwa wapi kusema jamani tunaibiwa??

Je si hawa walikuwa wanasafirosha madini yetu toka migodini na walikubaliana kabisa na wawekezaji,hivi baada ya miaka yote ya kuramba asali leo anakuwa na ngonjera ati kwenye mchanga kuna dhahabu nyingi mbona simuelewi??

Hivi uzalendo unaanzia pale unapokosa ulaji??Na zile shares ameshadeclare??Alishadeckare kwamba alikuwa muajiriwa.wa kampuni Mpinzani wa acacia?Hivi Acacia wakisema jamaa alikuwa wanatetea shares zake ili kuua kiuchumi acacia tuna hata cha kujitetea??

Ninachukia waongo mmoja wapo ni Mruma na Kalemani w atueleze kwamba kwanini walifanya walichofanya.

Lissu anasema ukweli hiimijitu ni miongo tu inataka tushtakiwe wakati kulikuwa na njia mbadala ya kupata hata kule kwenye minara ya dhahabu.
  1. Kampuni gani ambayo Prof. Mruma anamiliki hisa? Kampuni hiyo inahusana vipi na Acacia kwenye migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu?
  2. Unajuaje kwa Mruma hakuwahi kusema chochote kuhusiana na impropriety ya Acacia?
  3. Kazi ya kuongoza Kamatiya Rais ni jukumu alilokabidhiwa na Rais, sasa wewe unataka kupendekeza kuwa kabla ya kupewa jukumu hilo Prof. Mruma alikuwa na mandate gani ya kuunda kamati ya kuchunguza michanga ya dhahabu?
  4. Hivi unamaanisha kuwa Rais alielekezwa na Prof. Mruma kuunda kamati husika?
Haya tupatie majibu wenzako.
 
`pongezi kwa kazi nzuri iliyofanywa na tume'- lissu (kupitia account yake ya twitter). Wengine wakasema hakuwa ameisoma vizuri, kwa hiyo alikurupuka kupost? yeye ni msomi, anafahamu kwamba kabla ya kutoa `reply' kwenye utafiti wowote ni lazima u `read btn the lines' kwa mantiki hii huwezi ukamwamini lissu moja kwa moja.
 
Mimi sina shida na content, hata kama ina kasoro kiasi gani, ishu lugha. Kuna aina ya lugha mtu ukishafikia hatua fulani haupaswi kuzitumia
Mimi nina tatizo sana na watu wanaoshitushwa na lugha kali ya Lissu, wakati wanameza lugha kali na ya kuudhi sana inayotumiwa na viongozi wa serikali na wale wa CCM, dhidi ya wapinzani kwa ujumla. kwa miaka nenda miaka rudi, inaelekea imekubalika kwamba wapinzani ni waleta fujo, "tuwapigepige, tuwachanechane tuwatupe..." aliimba marehemu Komba, na hiyo ilikuwa moja tu ya nyimbo za kuudhi sana tu. imewahi kusemwa kwamba "Wapinzani wakipewa mamlaka ya kuunda serikali, wataleta vita". Mkapa aliwahi kutamka kwamba "Malofa hawa". lugha zinazotumika bungeni ndio usiseme. Rais Magufuli, wakati CHADEMA wanajiandaa kutekeleza kampeni ya UKUTA, ambayo ilikuwa ni watu kuandamana kutoa malalamiko yao, alitoa lugha kali na ya kuudhi na ya vitisho. Kuandamana ni jambo halali kabisa kwa mujibu wa katiba yetu, na ni halali kwa mujibu wa sheria ya vyama vingi. lugha kali ya Rais Magufuli, kitendo cha serikali kuamrisha vikosi vya polisi nchi nzima kufanya mazoezi na kuonesha silaha zao kali hadharani, yote hayo yalikuwa ni unyanyasaji wa wazi, na udhalilishaji wa kiwango cha juu. lakini hatukuona hawa wanaoona kuwa wapinzani wana lugha kali, wakijitokeza hadharani kulaani lugha na vitendo hivyo.

Rais, ambaye anapaswa kuwa juu ya wote, kuwa nje ya chama, alitoa vitisho na kusema "ole wao, na wajaribu waone... tena wasingoje mwezi ujao, waandamane hata kesho waone cha moto...". Hapa rais alikuwa tayari kuamrisha vyombo vya maguvu na vyenye silaha za moto, ambapo watu wanaweza kujeruhiwa vibaya na hata kuuawa, kisa wanatekeleza haki yao ya kikatiba. hatukuona maneno ya busara ya kuitaka serikali itende haki. sasa leo Tundu Lissu anatamka kwamba ripoti ya utafiti "ni rubbish" watu wanakuja juu, nywele zinasimama. hapo hajamtolea mtu bastola wala kumtishia maisha mtu yeyote. kwa taarifa yako ndugu yangu, hutokea mtu unapeleka ripoti yako kwa msimamizi wako, anaweza, baada ya kuisoma, hata kuichana chana na kusema kuwa hujaandika kitu hapo. alichosema Lissu ndio hicho, tusubiri hoja za kutetea kwamba ile siyo rubbish bali ni mali tupu
 
Usitumie akili za ccm kuelewa.

Rejea tamko la acacia, ni kwamba:-
Kama kiwango cha dhahabu anazodai professor mruma kipo kwenye ule mchanga, ingemaanisha jumla ya dhahabu wanayochimba wao hapa tanzania ingekuwa nyingi kuliko mchimbaji yeyote duniani.

Hakikisha hesabu hazikupigi chenga ndipo ushupaze mshipa kubishana.
Waombe wenzako wakufundishe kuelewa hesabu za elementary logic na one-to one functions utaweza kuelewa hoja husika.

Here you come
Kama Dhahabu yote ya Acacia huchimbwa nchini Tanzania pekee; kama Acacia ni kampuni kubwa kwa kuzalisha dhahabu kuliko kampuni yoyote duniani, basi Tanzania ni nchi ya kwanza kuzalisha dhahabu duniani. Umeelewa?
 
Hivi wewe Lissu anakupa shida gani wakati yule ni mwendawazimu wa kupuuzwa tu
Acha kumpuuza rais wa TLS ambaye rais kesho amepanga kumjibu.. wewe unampuuza rais wako anamtilia maanani,bilashaka watu watakupuuza wewe.
 
alichosema Lissu ndio hicho, tusubiri hoja za kutetea kwamba ile siyo rubbish bali ni mali tupu
who cares wasting time responding to such rubbish utterance of rubbish? You will learn a long way when you are already lost. And who said the report was about research? No research was conducted ever but scientific examination by of testing samples. atakiwa kujua tofauti kati ya utafiti na uchunguzi kisayansi.
 
Vipi kuwaita wanafunzi walodahiliwa na kuingizwa chuoni kwa mfumo sahihi kuwaita "vilaza?"
Hapana. Walikuwa wamedahiliwa kwa njia ya kukwepa mfumo sahihi, usitetee ujinga. Hawakuwa na viwango vya ufaulu viivyotakikana na ndio maana waliondolewa takriban wote na kupelekwa vyuo stahiki kwao, isipokuwa wachache wao.
 
Ujue mara nyingi wapinzani wanakuwa na hoja nzuri tu kwenye mambo mbalimbali shida ni kutoa mawazo yao kwa jazba na lugha chafu. Mwishowe wanaharibu ladha yote ya hoja zao.

"Ripoti ya Mchanga it is Rubbish! Rubbish!" Lissu (2017).Ni mfano mmoja miongoni mwa mingi.

Hauwezi ukawakosoa wasomi wenzako kwa kutumia lugha za namna hii. Haikubaliki dunia nzima. Wasomi hukosoana kwa hoja lakini kwa lugha zenye staha. Mfano huwezi kumuambia mtafiti, mchunguzi, au mtoa ripoti kuwa "ripoti yako ni upuuzi mtupu" badala yake unatakiwa umuambie ripoti yako ina upungufu mkubwa n.k

Kwa hiyo ni vizuri kuwa makini na utumiaji wa lugha unapowakosoa wasomi wenzako, vinginevyo hata kama una hoja ya msingi utapuuzwa.


Dunia ya tatu haina "tolerance" bro! Kumkosoa mwenzako inabidi utumie lugha hasi ili ku-capture attention wa watu! Tumekosa tu kustaarabika, sio TL tu bali wasomi wengi hawajui kubishana kwa hoja, zaidi ya kukejeliana! Labda vyuoni wanafundishwa namna hiyo, huwezijua!
 
Mimi sina shida na content, hata kama ina kasoro kiasi gani, ishu lugha. Kuna aina ya lugha mtu ukishafikia hatua fulani haupaswi kuzitumia
Una point, ula kwa aina ya siasa ya hapa hasa haina ustaarabu, zaidi ni dhihaka na lugha chafu, huwa haionekani wala kukemewa CCM wakiongea.
 
Kwa watu wenye ujuzi na fani ya miamba wanajua ukweli halisi na ndio maana wengi wao walishangaa hiyo report kama kweli hiyo copper concentrate ina madini kiasi kile!! Kwa dunia hii migodi ingekuwa iko nafasi ya juu sana!! Ndio maana lisu alitumia lugha kali kiasi kile kwani masuala ya kitaalam ni kosa kubwa kuweka siasa
kwa akili yako wale ma dr walidanganya?
 
Back
Top Bottom