Lissu, wasomi duniani kote hawafanyi hivyo

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,784
2,000
Ujue mara nyingi wapinzani wanakuwa na hoja nzuri tu kwenye mambo mbalimbali shida ni kutoa mawazo yao kwa jazba na lugha chafu. Mwishowe wanaharibu ladha yote ya hoja zao.

"Ripoti ya Mchanga it is Rubbish! Rubbish!" Lissu (2017).Ni mfano mmoja miongoni mwa mingi.

Hauwezi ukawakosoa wasomi wenzako kwa kutumia lugha za namna hii. Haikubaliki dunia nzima. Wasomi hukosoana kwa hoja lakini kwa lugha zenye staha. Mfano huwezi kumuambia mtafiti, mchunguzi, au mtoa ripoti kuwa "ripoti yako ni upuuzi mtupu" badala yake unatakiwa umuambie ripoti yako ina upungufu mkubwa n.k

Kwa hiyo ni vizuri kuwa makini na utumiaji wa lugha unapowakosoa wasomi wenzako, vinginevyo hata kama una hoja ya msingi utapuuzwa.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,784
2,000
Sasa kama ni rubbish ulitaka asemeje? yaani ma CCM yanapenda kusifiana ujinga
Sijasema usifu kitu kama unaona kina kasoro, nimesema ubakosoa kwa lugha ya staha. Hebu fikiri mfano wewe umefanya kazi yako kwa kutumia muda akili na resources nyingine, halafu unamaliza na kuwasilisha halafu anaibuka mtu mmoja anayeaminika kuwa msomi anakuambia what you did is total rubbish! Hahahaha, hatuendi hivyo aiseee, Lisu yuko vizuri ila kwa lugha hizi sio aisee, ajirekebishe
 
MAKOSHNELI

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
908
1,000

Mkapa aliwaita wapinzani woote Malofa Huyu wasasa ana lugha za kejeli na za kuudhi pia kunaubaya gani Lissu kuiita riport ya CCM kuwa ni Rubbish kama kweli ipo hivyo? usipende ku-"SUGARCOAT" mambo kama ni nyekundu sema ni "NYEKUNDU"
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
5,184
2,000
Ujue mara nyingi wapinzani wanakuwa na hoja nzuri tu kwenye mambo mbalimbali shida ni kutoa mawazo yao kwa jazba na lugha chafu. Mwishowe wanaharibu ladha yote ya hoja zao.

"Ripoti ya Mchanga it is Rubbish! Rubbish!" Lissu (2017).Ni mfano mmoja miongoni mwa mingi.

Hauwezi ukawakosoa wasomi wenzako kwa kutumia lugha za namna hii. Haikubaliki dunia nzima. Wasomi hukosoana kwa hoja lakini kwa lugha zenye staha. Mfano huwezi kumuambia mtafiti, mchunguzi, au mtoa ripoti kuwa "ripoti yako ni upuuzi mtupu" badala yake unatakiwa umuambie ripoti yako ina upungufu mkubwa n.k

Kwa hiyo ni vizuri kuwa makini na utumiaji wa lugha unapowakosoa wasomi wenzako, vinginevyo hata kama una hoja ya msingi utapuuzwa.
Kwa watu wenye ujuzi na fani ya miamba wanajua ukweli halisi na ndio maana wengi wao walishangaa hiyo report kama kweli hiyo copper concentrate ina madini kiasi kile!! Kwa dunia hii migodi ingekuwa iko nafasi ya juu sana!! Ndio maana lisu alitumia lugha kali kiasi kile kwani masuala ya kitaalam ni kosa kubwa kuweka siasa
 
tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,388

Hakuna siasa ktk ile report ya wanasayansi na ule ndiyo ukweli wa report yenyewe.

Uiite rubbish au sijui uiite takataka ndiyo report iliyofanyiwa kazi na wataalam
 
nanjinji

Senior Member
Mar 23, 2017
151
250
Kwa watu wenye ujuzi na fani ya miamba wanajua ukweli halisi na ndio maana wengi wao walishangaa hiyo report kama kweli hiyo copper concentrate ina madini kiasi kile!! Kwa dunia hii migodi ingekuwa iko nafasi ya juu sana!! Ndio maana lisu alitumia lugha kali kiasi kile kwani masuala ya kitaalam ni kosa kubwa kuweka siasa
Kwa hiyo Lissu na yeye ni mjuvi wa mambo ya Miamba..?
 
Msengapavi

JF-Expert Member
Oct 23, 2008
8,499
2,000
Sijasema usifu kitu kama unaona kina kasoro, nimesema ubakosoa kwa lugha ya staha. Hebu fikiri mfano wewe umefanya kazi yako kwa kutumia muda akili na resources nyingine, halafu unamaliza na kuwasilisha halafu anaibuka mtu mmoja anayeaminika kuwa msomi anakuambia what you did is total rubbish! Hahahaha, hatuendi hivyo aiseee, Lisu yuko vizuri ila kwa lugha hizi sio aisee, ajirekebishe
Oya! Rubbish ni Rubbish tu aisee!
 
shululu

JF-Expert Member
Jan 26, 2015
28,124
2,000
Kwa watu wenye ujuzi na fani ya miamba wanajua ukweli halisi na ndio maana wengi wao walishangaa hiyo report kama kweli hiyo copper concentrate ina madini kiasi kile!! Kwa dunia hii migodi ingekuwa iko nafasi ya juu sana!! Ndio maana lisu alitumia lugha kali kiasi kile kwani masuala ya kitaalam ni kosa kubwa kuweka siasa
Hawaelewi hawa watu hata uwaeleweshe vip, Lissu alikuwa sahihi kabisa
 
mangelengele

JF-Expert Member
Nov 4, 2014
1,295
2,000
Unajua Ukisha Tengeneza Mazngira Ya Watu Kufanya Kaz Kwa Uwoga Unategemea Ukiwaasign Kaz Watafanyaje, Lazma Wakupe Majibu Unayo yataka Wewe. Ndivyo Wanavofanya Akina Mugabe, Kagame, Nk Wa Namna Hyo. Mf. Unaenda Mahala Unasema Hapa Lazma Kuna Wizi, Af Unatuma Watu Waende Kuchunguza, Unategemea Jb Gan?
 
Zakaria Lang'o

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
2,595
2,000
Hakuna siasa ktk ile report ya wanasayansi na ule ndiyo ukweli wa report yenyewe.

Uiite rubbish au sijui uiite takataka ndiyo report iliyofanyiwa kazi na wataalam
Kama ni wataalam basi kuna mahali walifungwa pingu kiasi kwamba wakawa hawana namna ila kumfurahisha aliyewatuma. Si unajua tabia ya viongozi wa kiafrika bwana, wanapenda kusikia kile walichokwisha kuamua!!
 
Sophist

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
4,396
2,000
Kwa watu wenye ujuzi na fani ya miamba wanajua ukweli halisi na ndio maana wengi wao walishangaa hiyo report kama kweli hiyo copper concentrate ina madini kiasi kile!! Kwa dunia hii migodi ingekuwa iko nafasi ya juu sana!! Ndio maana lisu alitumia lugha kali kiasi kile kwani masuala ya kitaalam ni kosa kubwa kuweka siasa
  1. Lissu hajasoma ripoti husika, na hata angekuwa ameisoma;
  2. Lissu siyo mtaalam wa sayansi ya miamba wala madini; na kama bado hujaelewa,
  3. Hao unaosema kuwa ni 'wataalam' walioshangaa maudhui ya riporti ya Prof. Muruma, hujasema ni akina nani na walifanya uchunguzi gani kuthibitisha utaalam wao.
Kama hivyo basi, hitimisho lako unalosisitiza kwenye bandiko lako linabebwa na msingi (locus stand) gani? Unapaswa kuelewa kuwa Tanzania haijawahi (hakuna ushahidi wa takwimu) kufanya comparative study ya kiasi cha dhahabu tulichonacho dhidi ya mataifa mengine kama Canada, Australia, Afrika Kusini, Ghana, Chile, DR Congo wala Mali. Unachoelezwa kuwa Tanzania ni nchi ya nne kwa kuwa na wingi wa dhahabu Afrika ni tathmini zinazofanywa na wachimbaji wawekezaji wenyewe na kisha kusambaza takwimu hizo kulingana na mikakti yao ya kibiashara/uwekezaji. Miaka kabla ya 2009 walikuwa wakisema Tanzania ni nchi ya tatu Afrika (nyuma na Afrika Kusini na Ghana) kwa kuwa na dhahabu nyingi. Baadaye (2010 na kuendelea) wakasema Tanzania ni nchi ya nne nyuma ya Afrika Kusini, Ghana na Mali kwa kuwa na wingi wa dhahabu. Kwa hiyo, ni mtu mjinga tu asiyejua political economy za TNEs na beneficiaries wao ndie anaweza kusema eti, 'haiwezekani Tanzania ikwawa na madini kiasi kinachotajwa kwenye ripoti ya Prof. Mruma (mtaalam wa jiolojia/miamba ya madini) ka kuwa wataalam wa Acacia wamesema kuwa haiwezekani!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom