Chikwangara
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 685
- 942
Wenye akili za kununulika!? Mwambieni aruhusu mikutano ndo uje tena na unafiki wako.
Si mseme wanamfuata Maghufuli na siyo chama? Au pengine wananchi huwa hawafuati sera, bali personalities nk. Ndo maana hata midahalo hakuna wakati wa uchaguzi wa rais, na wananchi wanaona sawa kabisa!Hii dhana ya kusema Chama ni kile kile na itikadi ni ile ile haina mashiko katika uwanja wa siasa ambazo zinachagizwa na mazingira.
Kiongozi mkuu wa chama ndiye chachu katika mageuzi, mabadiliko na maendeleo ndani na nje ya chama.
Chama kile kile na itikadi ile ile lakini CCM ya wakati wa Mwl. Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete inatofautiana kulingana na uongozi wa kila mmojawapo.
Yes, Kiongozi Mkuu wa chama ni muhimu kama driver bila regardless una abiria wana uwezo gani. Driver akiwa mzuri hata kama gari linamatatizo anaweza kumudu kuliongoza kwa weledi
Kwa nini unadhani Mbowe anaweza kuongoza CHADEMA badala ya Prof. Safari kama chama ni kile kile na Itikadi ni ile ile!
Hata nchini Uingereza pamoja na kwamba chama chenye wabunge wengi ndichp huunda serikali lakini kama kiongozi wa chama hana uwezo hata chama hakiwezi kushinda uchaguzi hata kama wagombea wake wa ubunge watakuwa wana uwezo mkubwa kiuongozi.
Wao wanachoshindwa kuelewa kuanzia mwenyekiti hadi hawa kina jinga lao & co malumbano ni chachu ya maendeleo . Hata huko ulaya walilumbana wee mpaka wakapata maendeleo. Ni hatari sana kiongozi kufikiria ana akili nyingi na ni suluhisho la matatizo yoote kwenye taasisi? ukiona hivyo ujue huyo anataka kuabudiwa na kutukuzwa... lakini utukufu wa pekee huletwa na mungu wala hauji kwa hutuba za mazabahuniNinaendelea kushangazwa na sababu zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani pale wanaporudi ama kuhamia ccm.
Porojo ni nyingi, lakini kwa kifupi, ni kama wamemfuata mtu na si chama. Chama ni kile kile, sera ni zile zile. Lakini wanapotoa sababu zao, unaona kabisa ni kwasababu ya mtu, ni kwasababu ya Maghufuli, na si kwasababu ya chama.
Wengine ambao wako ccm, wanasema Maghufuli anafanya yale ambayo upinzani waliahidi kuyafanya, kwahiyo ndiyo maana wengi walioko upinzani wanarudi ccm.
Hii situation yote inatufanya tuonekane kama hamnazo! Ngoja nikusanye sababu zilizotajwa na baadhi ya viongozi wa upinzani kuhusu kuhamia ama kurudi ccm, halafu tuone kama akili zao hao watu si mbovu.
Kuna mmoja wa huko Siha mkoani Kilimanjaro, ambaye ni diwani, katoa sababu kuwa eti “ccm ni chama kinachofanya siasa za maendeleo na siyo za kulumbana na kupoteza muda”. Kuna ukweli gani hapo? Anafahamu alichoongea? Sababu iliyomfanya akajiunga na upinzani hapo mwanzoni, kwa maoni yake, hazipo tena kwasababu ccm inafanya siasa za maendeleo!
Nitaweka hizo sababu za wengine, halafu tujadili.