Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,320
- 18,599
Nilishasema humu na ninaendelea kusema, Hakuna chama pinzani kilicho serious wala hakuna chama pinzani kinachofanya kazi kikidhamiria kushika dola.Hivi chadema nyie ndio mmekuwa mboga kiasi hiki? [emoji28][emoji28][emoji28] yani kwamba sasa na ninyi mnafika bei? Alafu sasa mnakuja kulilia hapa kwamba mnafika bei bila aibu?
Najiuliza tu, mngepewa nchi ingekuwaje? Maana hao mnaosema wamenunuliwa ndio wamgekuwa mawaziri wenu hao! Ndio ambao wangekuwa wawakilishi wa rasilimali zetu dhidi ya mabepari, sasa ingekuwaje?
Wanaume wazima mnalia kununuliwa kweli bila aibu?
CCM sio chama imara, wala CCM haipendwi, wananchi hawashindwi kuiacha CCM ila sasa wakiacha CCM watamchagua nani?
Ni bora CCM mara 10 kuliko kuchagua chama pinzani, huko vyama pinzani kuna wanafiki sana, mtu yuko upinzani anahamia chama tawala kirahisi tu alafu tukiamini chama?
Mtu wa chama pinzani anateuliwa kua RC alafu tuamini kwamba kuna chama pinzani?
CCM ni hovyo sana lakini vyama pinzani ndio hovyo zaidi, sio Chadema wala CUF wala ACT wote hovyo tu hakuna mwenye unafuu.
Muendelee kununuliwa na mngepewa nchi mngeiuza kwa wazungu mchana kweupe.