Lissu Vs. Chikawe: Prosecute or Not to Prosecute Chenge in BAE Scandal

Lissu Vs. Chikawe: Prosecute or Not to Prosecute Chenge in BAE Scandal

SAKATA LA RADA:Kina Ndugai wataka kina Chenge washitakiwe

TIMU ya wabunge walioenda nchini Uingereza kufuatilia malipo ya rada kwa Serikali ya Tanzania imekabidhi ripoti yake kwa Spika wa Bunge inayopendekeza mambo mawili, ikiwamo kushtakiwa kwa wahusika wa sakata hilo hapa nchini.Timu hiyo ya wabunge wanne ikiongozwa na Naibu Spika, Job Ndugai, ilimkabidhi ripoti hiyo kwa Spika Anne Makinda jana mchana.

Wajumbe wengine wa timu hiyo ni Angellah Kairuki (Viti Maalumu-CCM), Mussa Zungu (Ilala-CCM) na John Cheyo (Bariadi Mashariki-UDP).

Kwa nyakati tofauti, wabunge hao waliwaeleza waandishi wa habari mjini hapa jana kuwa imegundua madhambi ya kutisha katika sakata la ununuzi wa rada hiyo ya kijeshi yanayoweza kuwatia hatiani wahusika.

Ingawa wajumbe hao hawakuwataja watuhumiwa hao kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Andrew Chenge, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), ni mtuhumiwa namba moja na aliyekuwa Gavana wa BoT, Dk Idrisa Rashid.

Wakati wa uchunguzi wa sakata hilo, Kampuni ya SFO ilibaini zaidi ya Dola za Marekani 1.2milioni kwenye akaunti ya Chenge iliyoko katika kisiwa cha Jersey nchini Uingereza. Lakini alipohojiwa na waandishi wa habari, Chenge alisema 'hivi ni vijisenti tu'

"Miongoni mwa mapendekezo yake (ripoti) kwa Serikali ni kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote waliohusika kwenye ufisadi huo," alisema mmoja wa wajumbe wa timu hiyo.

Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa imeweza kufichua mlolongo wa kashfa na njama ambazo zilitengenezwa nchini Uingereza ili kufunika uovu huo ambao ni wizi dhidi ya fedha za Watanzania.

Wakizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, timu hiyo ilisema, mbali na kupendekeza wahusika katika sakata hilo washtakiwe, walitaka pia Bunge na Serikali kushirikiana kwa karibu hadi fedha ambazo Tanzania inazidai kutoka Kampuni ya BAE System, zipatikane.

Cheyo, mmoja wa wajumbe wa timu hiyo, hakuwapo katika mazungjmzo hayo na waandishi wa habari jana.

Wabunge hao walisema katika safari yao wamegundua mengi ikiwa ni pamoja na namna uovu huo wa kifisadi ulivyozimwa ili dunia isifahamu.

Angellah alisema kuwa timu hiyo ya wabunge ilibaini pia kuwa Serikali ya Tanzania ilikuwa imekatazwa na SFO isiwachukulie hatua watuhumiwa wa hapa nchini kwa sababu ingekuwa ni mwingiliano wa kesi mahakamani.

Alisema kwa sasa ambapo tayari mahakama ya Uingereza imetoa hukumu, Tanzania iko huru kuwachukulia hatua wahusika. Pamoja na hali hiyo, alisema nguvu kubwa kwa sasa ielekezwe katika kuiwezesha Tanzania kupata fedha hizo bila mizengwe.

Alisema kama Serikali ya Tanzania inataka kuwashtaki inapaswa kupata pia ushahidi wa SFO ambao waliutumia kuibana BAE hadi ikaamua irejeshe fedha zote.

Kuhusu uwezekano wa kuwaunganisha maofisa wa BAE kwenye kesi hiyo, Ndugai alisema kuwa tatizo ni kwamba waliohusika kwenye mpango huo tayari wameondolewa kwenye kampuni hiyo.

Zungu alisema mkakati wao ni kwamba iwapo kampuni ya BAE haitatoa fedha hizo hadi Desemba mwaka huu, Serikali ya Tanzania ifungue upya mashtaka nchini Uingereza.

Kwa upande wake, Ndugai alianza kwa kuelezea lilikoanzia sakata hilo, akisema: "kama mnavyojua Desemba 20 mwaka jana mahakama nchini Uingereza ilitoa hukumu ambayo iliiadhibu kampuni ya BAE kulipa fidia ya paundi 29 milioni kwa Tanzania."

Alisema Kampuni ya Kuchunguza Rushwa kubwa kubwa nchini Uingereza ya (SFO) ndiyo iliyofungua mahakamani kesi hiyo. Ndugai alisema kwa kuwa BAE ilibaini kuwa shtaka hilo lilikuwa ni zito na lingeweza kuharibu sifa ya kampuni hiyo duniani, walifanya mpango wa kesi hiyo kuzungumzwa nje ya mahakama na kufanikiwa.

Wakiwa nje ya mahakama, Ndugai alisema BAE walitengeneza mkataba na kusema kwamba watarejesha fedha zote ambazo Tanzania ilinunulia rada hiyo pamoja na fidia.

"Yaani walifanya kana kwamba rada hiyo Tanzania imepewa bure. Maana walinunua kwa pauni 28 milioni na sasa wanatoa pauni 29.3 milioni," alisema Ndugai. Alifafanua kuwa mkataba huo ulikuwa ni wa kufunika aibu na uliandikwa na mwanasheria wa BAE huku ukieleza kuwa fedha hizo zitatolewa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ili yatoe huduma za kijamii.

Alisema hata kabla kesi hiyo haijaenda mahakamani, walitoa mapendekezo ya fidia itakayopatikana iletwe nchini ili kununua madawati na kujenga nyumba za walimu kwa kuwa waathirika ni Watanzania.

Baada ya makubaliano hayo ya nje ya mahakama, Ndugai alisema SFO na BAE walikubaliana kesi iliyoko mahakamani ijulikane kuwa ni ya kosa la kushindwa kuweka vizuri kumbukumbu.

Alisema SFO na BAE wakaingia mkataba wa kufunga faili la uchunguzi kuhusu kashfa hiyo ikiwa na maana kwamba uozo uliofanyika hautatolewa kwa namna yoyote kwa chombo chochote.

Ndugai alizidi kueleza kuwa hii ni njama kati ya SFO na BAE ya kutotaka madhambi yaliyofanywa katika ununuzi huo wa rada yasiwekwe hadharani na dunia ikafahamu.

Hata hivyo, Ndugai alisema kamati yake imegundua ujanja huo na kwamba kitendo cha kusema fedha hizo ziende kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ya kuisaidia jamii, ni njia ya kuzitumia wao wenyewe.

"Wao wanataka ionekane BAE wametoa msaada halafu wafanye safari za kuja nchini kwa ndege na walipane posho halafu mwisho wa siku fedha nyingi watatumia wao," alilalamika Ndugai.

Ndugai alisema fedha hizo zitolewe kwa Serikali ya Tanzania na zisimamiwe na Bunge katika kutengeneza madawati na nyumba za walimu na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG) aweze kuzikagua.

"Zikitolewa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali, CAG hataweza kuzikagua na hata matumizi yake yakipindishwa hakuna namna ya kuwabana wahusika," alisema Ndugai.

Akizungumzia kuhusu safari yao ya Uingereza, Zungu alisema walichogundua ni kwamba BAE ilifanya mchezo mchafu kuanzia ununuzi wa rada hadi kuficha madhambi yake kwa kutaka kesi izungumzwe nje ya mahakama.

Taarifa zao kuvuja
Alilalamika kuwa hata baadhi ya wabunge wa upinzani waliozungumzia suala hilo juzi, ilitokana na kuvuja kwa taarifa za ripoti yao.

Hakumtaja mbunge huyo wa upinzani, lakini John Mnyika ndiye aliyeliambia Bunge kuwa fedha hizo zisipelekwe serikalini kwa sababu walishindwa kuzisimamia na wala hawakuomba washirikishwe kwenye kesi hiyo.

Zungu alilalamika kuwa miongoni mwa lawama dhidi ya SFO ni kutoshirikisha Tanzania kwenye kesi hiyo hasa ikizingatiwa kuwa iliwasiliana na Takukuru ili kupata ushahidi ambao uliisaidia kuibana BAE.


Lakini akamsifu Jaji aliyeamua kesi hiyo kwa sababu alisisitiza kuwa dhuluma hiyo ilikuwa ni dhidi ya wananchi wa Tanzania hivyo lazima fedha hizo zipelekwe moja kwa moja kwa manufaa ya waathirika hao.

Zungu alisema kuwa Jaji aliamua itozwe fidia ndogo ya paundi 500,000 katika fedha hizo ili zigharimie kesi hiyo.

Zungu alionya kuwa kama mshikamano hautakuwapo katika suala hilo, BAE itatumia fedha za Watanzania na kujigamba imetoa msaada.

Alisema katika Bunge la Uingereza, Tanzania inasifiwa kuwa imekuwa ikitumia vizuri fedha za misaada na wanaridhika iendelee kupewa misaada.

"Sasa kitendo cha kutoa fedha hizi, zilizotoka mikononi mwa Serikali ziende kwa asasi za kiraia kwa madai kwamba hazitatumika vizuri ni udhalilishaji mkubwa," alieleza Zungu.

Alisema kamati hiyo ilipanga kukutana na Mkurugenzi wa SFO, Richard Agaman, lakini alikataa huku akisema yuko tayari kuwasiliana na balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Zungu alisema balozi huyo alisema mkurugenzi huyo wa SFO aliomba radhi kwa kutoshirikisha Serikali ya Tanzania kwenye kesi hiyo.

Chanzo: Mwananchi


Hawa Wabunge wapuuzi kabisa! yaaani wanaongea nini hapa na wanampinga nini Lissu?
 
We lazima utakuwa mwana sio riziki, kwa jinsi unavyoargue. Ina maana unafurahia taifa linavyotafunwa na wajanja wachache?
 
Mh Chikawe ushahidi dhidi ya Chenge ni huu hapa, na Mwanasheria Mkuu anafahamu!!!

nimeamua ku-copy kipande kidogo kutoka katika ukurasa wa 5, lakini naomba u-download report yote hapo chini.

------------------------------------------------------------------------------------
... It is apparent from documents obtained from BAE and from interviews conducted by the SFO that Vithlani was acting as SPS agent from the earliest stages of the proposed sale, as far back as 1992 - 1993. However there is no written product from Vithlani of note for the sums he was paid and persons familiar with the commercial negotiations state that Vithlani neither was a technical nor commercial specialist playing an apparently nominal role as the contract progressed to finality.

The SFO investigation has good grounds now to believe it was generally known that Vithlani's role involved making payments to Tanzanian public officials in positions of influence in the Radar contract negotiations. The SFO believes on reasonable grounds that the Attorney-General, Andrew John Chenge ("Chenge") was one of the most important persons whom it was believed Vithlani would have had to make payments...

------------------------------------------------------------------------------------

Naomba utimize kauli yako ya kumshtaki Andrew John Chenge, akifuatiwa na Dr Idriss Rashidi

Mungu ibariki Tanzania!!

Hakika hapo ndio msingi wa hoja ya Chenge and Rashid wote wafikishwe mahakamani. Chama Cha Magamba na TAKURURU acheni utani! Kama mnataka Ushahidi zaidi hao SFO watauleta. Msituletee hadithi za kijinga. Hawa watashitakiwa kwa sheria za Jamhuri ya Tanzania - hivyo kesi yao haijafungwa.
 
Viongozi wetu wengi ni vituko vitupu yaani wanakataa maelezo ya Lissu kisa ni Chadema
 
Tundu Lissu kajibiwa kuwa, kama unaushahidi leta tuupeleke mahakamani au upeleke takukuru au upeleke wewe mwenyewe Mahakamani.

Sasa anangoja nini?

Ma CCM na kutumia sijui harufu kuwaza na wewe ni kitu gani sijui.Mnatia aibu na hasira .But wananchi si wajinga .Mtaona wenyewe kwenye uchaguzi ujao .
 
Sasa hao waliotajwa ni akina nani?????na wameshakamatwa????
 
Tundu karusha mbegu ya hindi kumbe ndani kaweka ndoano sasa kwa vile majinga mengi ya amagamba yanagangana nani ale yamenaswe yote ole wenu mrudi huku majimboni mtaona dhahama yake kama hamjui hilo muulizeni Nyambari Nyangwine kilichowahi mtokea huko nyuma
 
Wabunge wa CCM wanakili za matope sana,yani wanawaza kwa kutumia makamasi badala ya ubongo,akili wamezifungia kabatini,wameiamua kuiuza nchi,wanabadilisha ukweli kuwa uwongo,mahakama ya wananchi itaamua hatma yao.
 
If Min. of good governance thinks after reading the SFO report that the AG who was obviously responsible for financing of the deal and of course who gave the green light to this radar deal, that Mzee Vijisenti is "cleared" of all wrongdoing than there is seriously something wrong concerning the Min. of good governance's stance on this highly sensitive matter. In fact, his stance on this matter could be viewed as a total failure of a whole government! A government devoid of all moral/ethical compass! Devoid of all and absolute responsibility for officials working for the country. His stance in trying to "clear" his "friend" from ultimately being prosecuted is truly shameful for the whole country, and for himself, his stance is nothing but an insult to good governance. Instead his stance on "cleansing" his friend sends a message to the world, that TZ gvt. is all about "goon" governance! In fact, he should be fired from his Min. position because he ultimately cannot do his job in a honest/truthful/objective/ professional manner as he is too busy trying to protect his friends and incapable of serving or looking after the well being of his country. & by the way he is getting paid for "protecting" his "friend-Mzee Vijisenti" (this friend who compares a million dollars to some cents), the money for his salary is coming from the TZ taxpayer.
 
Tundu Lissu kajibiwa kuwa, kama unaushahidi leta tuupeleke mahakamani au upeleke takukuru au upeleke wewe mwenyewe Mahakamani.

Sasa anangoja nini?
Umeshalala?
Takukuru nao wameshutumiwa na unajua tume hiyo ya kupamba na kuremba rusha itamuukumu vipi mtuhumiwa wa rushwa? Nakushangaa uzijui mahakama za tanzania? mwenye haki ndani mwizi huru?
usijichanganye mrembo, nakuja nikuelekeze vizuri, usifunge mlango. LOL
 
SIKU moja baada ya Serikali kumkingia kifua Mbunge wa Bariadi Mashariki (CCM), Andrew Chenge ili asishtakiwe kwa rushwa katika mchakato wa ununuzi ya rada, Chadema imeweka hadharani kurasa 11 za ushahidi inaodai kuwa unaweza kumtia hatiani Mwanasheria Mkuu huyo wa zamani wa Serikali kama atashtakiwa.

Ushahidi huo uliotolewa jana na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, ni ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Shirika la Upelelezi la Makosa Makubwa ya Jinai la Nchini Uingereza (SFO).

Dk Slaa aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa amefikia hatua hiyo baada ya kusikitishwa na majibu ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe kuhusu suala hilo alipokuwa akijibu hoja za wabunge.

Kwa mujibu wa Dk Slaa, ukurasa wa tano wa ripoti hiyo, unaeleza jinsi Chenge alivyoshinikiza utekelezwaji wa mkataba huo na namna alivyofaidika kwa malipo ya kitita cha Dola 1.5 milioni kupitia akaunti ya Benki ya Barclays iliyoko katika kisiwa cha Jersey nchini Uingereza.

"Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kati ya mwaka 1995 na 2006. Katika kipindi hicho, BAE na SPS walikuwa wakifanya majadiliano ya ununuzi wa rada kwa ajili ya Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam na Chenge alihusika moja kwa moja katika mchakato huo hasa kushinikiza ununuzi huo," alisema Dk Slaa akinukuu waraka huo alioutoa pia kwa waandishi wa habari.

Aliendelea,"Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilitakiwa kutoa maoni na kuthibitisha malipo hayo na bila Chenge kukubali, kusingeweza kufanyika chochote."

Kwa mujibu wa Dk Slaa, kauli ya Waziri Chikawe kuwa serikali haina ushahidi unaowataja watuhumiwa wa kashfa ya rada moja kwa moja na kutaka mwenye ushahidi wauwasilishe kwake, ni hatari kwa kuwa inaonyesha kuwa haina dhamira ya kweli ya kushughulikia rushwa na ufisadi huo.

Alisema ripoti hiyo ya SFO, ambayo anaamini Serikali inayo, ni ushahidi tosha unaoweza kumtia hatiani Chenge ambaye pia angeweza kusaidia kutaja wahusika wengine katika sakata hilo.

Alisema ushahidi huo huo ambao hata Mbunge wa sasa kupitia Chadema Tundu Lisu aliyeibua hoja hiyo upo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kusisitiza kuwa kama Serikali haina taarifa hiyo, ilipaswa kumwajibisha Mwanasheria wake na si kusafisha watuhumiwa wa ufisadi.

"Kinachofanywa sasa ni mpango wa makusudi wa Serikali ya CCM ambayo imeanza taratibu ya kuwasafisha watuhumiwa wa ufisadi kabla ya kufanyika kwa vikao vya chama hicho,"alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alikemea hilo na kusisitiza kuwa chama chake hakitalala bali kitatoka nje ya Bunge na kuendelea na maandamano ya kuelimisha Watanzania kuhusu suala hilo hadi hapo mafisadi wote watakapofikishwa mahakamani.

Kuhusu uhusika wa Chenge, alisema uchunguzi wa SFO umemwingiza moja kwa moja katika sakata hilo kwa sababu katika kipindi hicho, yeye (Chenge), alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

"Katika sakata hilo, Chenge anaingia moja kwa moja kwa sababu makubaliano yoyote katika mkataba huo, alikuwa ndiye mwenye uamuzi wa mwisho,"alisema Dk Slaa huku akinukuu ripoti ya SFO.

"Wakati suala la uuzwaji wa rada kutoka BAE kwa Serikali ya Tanzania likifikia ukingoni kati ya mwaka 1996/7, Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ni katika kipindi hiki ndipo Kampuni ya Franton Investment Ltd inayomilikiwa na Chenge ilipoingiziwa Sh1.5 milioni katika Benki ya Barclays katika visiwa vya Jersey,"alisema Dk Slaa.


Lissu: Chenge akishtakiwa hatoki

Kutoka Dodoma, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Tindu Lissu amesema iwapo Watanzania wataamua kumshitaki Chenge, atatiwa hatiani mara moja kwa sababu ushahidi uliopo hawezi kuukabili.

Lakini akasema tatizo ni Serikali kumkingia kifua ili asishtakiwe ingawa wao kama wabunge wa upinzani, wataendelea kupambana naye nje ya Bunge kwa kutumia majukwaa ya kisiasa ili umma wa Watanzania utoe hukumu.

Mbunge wa CCM achukizwa kauli ya Chikawe

Wakati Lissu akisema hayo, Ally Mohamed (Nkasi Kaskazini-CCM), alisema juzi hakupata usingizi kutokana na hasira alizopata baada ya kuchukizwa na kauli ya Chikawe kuwa Serikali haina ushahidi wa kumshtaki Chenge.

Wakati akifanya majumuisho wa bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mahusiano na Uratibu, Chikawe alisema uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru) unaonyesha hakuna Mtanzania aliyehusika na ufisadi wa ununuzi wa rada isipokuwa Waingereza watatu.

Licha ya Lissu kusema kuwa SFO iliwasilisha serikalini ushahidi kuwa Chenge alihusika na ufisadi huo, Chikawe alisema wao hawana na kumtaka apeleke ushahidi huo ili wautumie kumshitaki.

Lakini jana Lissu alisema hana haja ya kuwapelekea ushahidi alio nao kwa sababu anatambua wazi hicho ni kiini macho.

Alisema kwamba anatambua wazi kuwa barua hiyo ya SFO, Serikali inayo.

"Barua hiyo mimi nimeipata kutoka huko serikalini, wao wanasema niwapelekee, siwezi kufanya upumbavu wa namna hiyo," alisema Lissu akisisitiza:

"Limeshindikana hapa bungeni kwa sababu Serikali inamkingia kifua. Sisi hatuna haja ya kuendelea kujisumbua. Sasa tumeamua tutaingia mitaani maana huko ndiko waliko walioumia kutokana na ufisadi huo," alisema Lissu.

"Lakini kwa hakika leo hii Chenge akifikishwa mahakamani ni kitanzi tu," alidai Lissu ambaye ana taaluma ya sheria akimanisha kuwa ushahidi wa SFO unaweza kumtia hatiani.

Kuhusu kuwepo kwa ushahidi unaotosheleza, Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki alisema kuwa barua hiyo iliyoandikwa na SFO kwenda kwa Mwanasheria wa Serikali Machi 21, 2008, inaonyesha wazi jinsi fedha zilivyolipwa kwenye akaunti ya Chenge iliyopo katika kisiwa cha Jessy.

Alidai pia kuwa barua hiyo iliyosainiwa na Msimamizi wa Kesi za SFO, Mathew Cowie ilieleza jinsi sehemu ya fedha hizo zilivyotolewa na kupewa mtu mwingine anayefahamika kwa jina la Idriss Rashid.

Alifafanua kuwa kwa sheria za sasa za Takukuru, zinaweza kumtia hatiani Chenge kwa sababu zinasema kuwa uamuzi wowote uliofanywa na kiongozi wa Serikali wenye dalili inayoashiria kutokuwepo kwa maslahi ya umma, ni kosa litakalohesabika kuwa ni rushwa.

Akasema barua ya SFO inaonyesha kuwa kulikuwapo na mkakati ambao ulifanywa na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati huo wa kuingia mkataba na benki iliyotoa fedha hizo kuwa tatizo lolote litalakalotokea, halipaswi kushughulikiwa kwa namna yoyote na Serikali ya Tanzania bali ya Uingereza.


Chikawe alimkingia kifua Chenge muda mfupi tu baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kukabidhiwa ripoti inayolitaka Bunge kuishauri Serikali iwashitaki wote waliohusika na kashfa hiyo ya rada.

Ripoti hiyo ilitolewa na timu maalumu ya wabunge wanne, iliyoongozwa na Naibu Spika, Job Ndugai ikitoa pendekezo hilo baada ya kubaini kuwa kwenye sakata hilo kuna ufisadi wa kutisha.

Chenge asema apelekwe kwa Takukuru, DPP

Alipotafutwa na gazeti hili ili azungumzie tuhuma hizo jana, Chenge alihoji "kwanini watu wazunguuke? Kama wana ushahidi ni vema wakaupeleka Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa) halafu wao wataniita."

Chenge maarufu kama mzee wa vijisenti, alisema anashangazwa na watu ambao wamekuwa wakizunguka huku na kule kushikia bango jambo ambalo tayari limekwishafanyiwa uchunguzi na kutolewa maamuzi.

"DPP pia yupo na Takukuru, wakipeleka huko mimi si nitaitwa? Wapeleke tu nyaraka zao. Maana mimi napenda watu wenye uwezo wa kuthubutu..., hilo jambo limekwishaelezwa jana (juzi) na Waziri Chikawe, sasa hizo nyaraka mpya sijaziona na kama zipo wazipelekea mamlaka husika," alisisitiza.

Akionyesha msisitizo, Chenge alisema kama nyaraka hizo zinazoonyeshwa sasa ni zile za mwaka 2007, itakuwa sawa na kuwafanya Watanzania watu wasiojua kufikiri vema kwani nyaraka hizo ndizo zilizochunguzwa na kubainika hakuna kitu chochote kuhusu yeye.

"Tujielekeze katika mambo ya msingi tuache kuwahadaa Watanzania. Kama nyaraka zenyewe unazosema wanazo hao waliozitoa ni za mwaka 2007, basi huko ni kuhadaa Watanzania," alisema Chenge na kuongeza:

Uchunguzi una msingi wake, na ukishafanyika majibu yake huambatana na msingi wa jambo lenyewe..., nasema tena, hili jambo limekwishachunguzwa na hao SFO."
 
Watuhumiwa wengine wa rushwa ya rada ni kina nani? Naamini kuna zaidi ya Chenge. Chenge kama mwanasheria kazi yake ilikuwa ni nini katika mchakato mzima wa ununuzi wa rada? kuna kitu hakiko wazi hapa. Walio andaa specification na hatimaye kuona kuwa hiyo rada ya BAE inafaa na kuanza mazungumzo ya ununuzi ni kina nani?
 
sasa unadhani serikali italifuatilia suala hili chenge yeye wamamuonea lakini fedha hizi zilienda kwenye chama cha mapinduzi account no 2092500xxx
sasa kutaka kumshitaki chenge mwenyewe ni mchezo wa kuigiza
 
Hongera Chadema, Pigeni kazi kwenda mbele watanzania si tunaona nani anatutetea na nani anatumaliza mwisho wa siku tutafanya maamuzi. na maamuzi tutakayo yafanya hatutakubali yayumbishe! na kama ikitokea mtu anataka kupindisha sisi (umma) tutapambana nae
 
Back
Top Bottom