Lissu Vs. Chikawe: Prosecute or Not to Prosecute Chenge in BAE Scandal

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,226
Hayo ni kwa mujibu bungeni leo,Lissu akasema iyo barua inayomtaja chenge na idrisa ilikuwa addressed kwa attorney general je mnaitaji ushaidi gani kuwaburuza mahakamani hawa jamaa.Nami nongezea kama hamna ushaidi kwa nini mnataka ela izo ziludi tz?shenzi kabsaa suala liko obvious
 
Nimeangalia bunge jioni hii, Tundu Lissu kaisoma barua bungeni inayoonyesha jinsi Andrew Chenge alivyonufaika na fedha za rada. Mathias Chikawe na Hawa Ghasia wanasema Lissu apeleke ushahidi. Akawajibu kuwa Serikali imepelekewa ushahidi. Ajabu wabunge wa CCM wamejibu sioooooooo.....kupinga hoja ya Lissu.Nimejiuliza sana,sipati jibu..... CCM wapo kwa ajili ya nani? Dhana ya kujivua gamba iko wapi? Nashauri Chadema wakishindwa bungeni warudi kwa wananchi, watueleze uhalisia wa hili jambo. Watanzania tuna akili za ajabu sana
 
Foolish gov't ever seen. INDEED LISSU SPEAKS FOR THE SILENT MAJORITY
 
Serikali ushahidi unao kwa Atorney General, unless kama barua iliandikwa wakati Chenge ndiyo AG. Tatizo mawaziri wetu wanajibu hoja kiushabiki wa kisiasa.
 
nimeshangaa sana. huku nje wanazungumzia kuwa chenge fisadi, bungeni wanakataa kuwa si fisadi. ni afadhali dhana ya kujivua gamba waiache tu ni ya kinafiki
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Serikali ushahidi unao kwa Atorney General, unless kama barua iliandikwa wakati Chenge ndiyo AG. Tatizo mawaziri wetu wanajibu hoja kiushabiki wa kisiasa.

Ni ushahidi wa bunge kubakwa na CCM kunufaisha serikali legelege.
 
Haingii akilini kuona jambo la wazi kama ushahidi anaotoa Tundu Lissu dhidi ya Andrew Chenge kwamba ni sawa kuipotezea kwa kura ya sio, bila kuona umuhimu wa kusaidia serikari kurudisha fedha iliyoibwa.
Kwa maneno mengine ni sawa wizi wa chenge utetewe na wabunge kwa vile tu huyo ni mwanachama wa chama chao kilicho madarakani. Haingii akilini!
 
Barua ilikuwa addressed kwa AG sasa serikali hata. Haijui kuwa kuna iyo barua nyambafu
 
Kazi tunayo, safari ya ukombozi ni ngumu kuliko chochote,mapambano yanahitajika ili kutoka katika dhuruma ya CCM na kupata UHUiRU wa dhati,watoto wetu,mama zetu,baba zetu,bibi zetu na babu zetu wanaishi maisha magumu hadi wanatamani kufa.Eee MUNGU tusaidie watanzania tuondokane na dhuruma hi ya CCM.
 
CCM wanafiki wakubwa.

Pia Lissu kawatega hao CCM bila CCM kujua hilo.
 
Tundu Lissu kajibiwa kuwa, kama unaushahidi leta tuupeleke mahakamani au upeleke takukuru au upeleke wewe mwenyewe Mahakamani.

Sasa anangoja nini?
 
sasa maana ya kujivua gamba manake nini.bora umeme umekatika huku kwetu,manake ningevunja hata ka tv kangu kwa hasira.
 
Nimeangalia bunge jioni hii, Tundu Lissu kaisoma barua bungeni inayoonyesha jinsi Andrew Chenge alivyonufaika na fedha za rada. Mathias Chikawe na Hawa Ghasia wanasema Lissu apeleke ushahidi. Akawajibu kuwa Serikali imepelekewa ushahidi. Ajabu wabunge wa CCM wamejibu sioooooooo.....kupinga hoja ya Lissu.Nimejiuliza sana,sipati jibu..... CCM wapo kwa ajili ya nani? Dhana ya kujivua gamba iko wapi? Nashauri Chadema wakishindwa bungeni warudi kwa wananchi, watueleze uhalisia wa hili jambo. Watanzania tuna akili za ajabu sana

Hichi ni kisiki kingine kwa Nape.....
 
Wabunge wote wa ccm ni watumwa kwa kiasi fulani. Wakiwa nje ya Bunge wanaonekana kuwa na akili timamu na hata kulalamika kuhusu utendaji wa serikali lakini bungeni hawathubutu kusema au kusimamia yale wanayoyalalamikia huku mtaani. Kama mbunge hayuko huru wananchi wa kawaida watakuwaje?
 
Back
Top Bottom