Lissu Vs. Chikawe: Prosecute or Not to Prosecute Chenge in BAE Scandal

Lissu Vs. Chikawe: Prosecute or Not to Prosecute Chenge in BAE Scandal

Serikali ushahidi unao kwa Atorney General, unless kama barua iliandikwa wakati Chenge ndiyo AG. Tatizo mawaziri wetu wanajibu hoja kiushabiki wa kisiasa.

Kazi tunayo, safari ya ukombozi ni ngumu kuliko chochote,mapambano yanahitajika ili kutoka katika dhuruma ya CCM na kupata UHUiRU wa dhati,watoto wetu,mama zetu,baba zetu,bibi zetu na babu zetu wanaishi maisha magumu hadi wanatamani kufa.Eee MUNGU tusaidie watanzania tuondokane na dhuruma hi ya CCM.

Tundu Lissu kajibiwa kuwa, kama unaushahidi leta tuupeleke mahakamani au upeleke takukuru au upeleke wewe mwenyewe Mahakamani.

Sasa anangoja nini?

Oh! My God! U-CCM unaiua nchi. Inakera unapoona watu wazima(ccm) wanakuwa wanafiki hata kwa nafsi zao! Laana iwafuate makaburini siku wakifa!

waziri chikawe alipomaliza hotuba yake nilijiuliza kama nape na mukama wamemsikiliza ama walikua ktk mikutano ya chama chao kujivua gamba!
  1. Assume Lissu ni muongo, kalidanganya Bunde, Mbona Makinda hakumwabia kuwa kalidanganya Bunge alete ushahidi kama Zitto na Lema walivyowai kuambiwa?
  2. Assume Spika kabadili tabia yake, then jiulize kama CCM na Serikali yake hawana ushahidi huo hivi kwanini wanamuita Chenge Gamba na walimpa 90days yeye na wenzake wakidai watamfukuza ni Fisadi?
Hizi assuption mbili ni ushahidi tosha kuwa CCM walivyosema kuwa watawachukulia hatua Mafisadi walikuwa wanajaribu kuchezea akili za Watanzania na huu ni Ushahidi kuwa Nape anaimba wimbo wake binafsi wa kitoto ambao wazazi wake CCM hata hamwelewi kabisa na yamkini wanamshangaa anavyopiga kelele mitaani, au Nape anazunguka zunguka kutafuta Posho tu!
 
Nimeangalia bunge jioni hii, Tundu Lissu kaisoma barua bungeni inayoonyesha jinsi Andrew Chenge alivyonufaika na fedha za rada. Mathias Chikawe na Hawa Ghasia wanasema Lissu apeleke ushahidi. Akawajibu kuwa Serikali imepelekewa ushahidi. Ajabu wabunge wa CCM wamejibu sioooooooo.....kupinga hoja ya Lissu.Nimejiuliza sana,sipati jibu..... CCM wapo kwa ajili ya nani? Dhana ya kujivua gamba iko wapi? Nashauri Chadema wakishindwa bungeni warudi kwa wananchi, watueleze uhalisia wa hili jambo. Watanzania tuna akili za ajabu sana
da mkuu wangekua Tundu Lisu 100 bungeni kazi ingekuwepo kwa magamba
 
Sio kwamba srikali haina ushaidi inashindwa kumshitaki sbabu ya cheo alichokuwa nacho. Ni katika veyoe nyeti sana na ndio maana hata rais akiapishwa teuzi za mwanzoni pamoja na AJ.

Kumshtaki AG maana yake hapo nyuma yake kuna lundo la watu.pia wanatakiwa kushtakiwa naye. Who are they???

But ile NGO yake yenye vijisenti new jersey ambayo alisema yeye ni mlezi
  • Ofisi zake ziko wapi
  • Inashughulisha na na shughuli gani
Hivi waandishi wetu toka issue izimwe wameshindwa kufuatilia ka kuchimba data zaidi........
 
Na wapa hii wana JF,

Chenge still ana jeuri na dharau kwa watanzania amini usiamni nilishudia mahali alirudishiwa chenji akajibu kwa kejeri hivyo vijiela ndio mwanirudishai mwanionaje mie? kaeni navyo, huyu mtu ana maana gani mbele ya jamii ni kuwa dhahili nchi wameishikilia mikononi mwao change ya shilling elfu 4 anaidharau kiasi hicho ingali ananajua vyombo vya habari na wananchi wana mtizama kwa jicho tofauti khaaaaa nchi hii kweli ina wenyewe
 
Pole tanzania. Chenge chenge halafu ccm wamtetetee, wala bangi hao
 
TIMU ya wabunge walioenda nchini Uingereza kufuatilia malipo ya rada kwa Serikali ya Tanzania imekabidhi ripoti yake kwa Spika wa Bunge inayopendekeza mambo mawili, ikiwamo kushtakiwa kwa wahusika wa sakata hilo hapa nchini.Timu hiyo ya wabunge wanne ikiongozwa na Naibu Spika, Job Ndugai, ilimkabidhi ripoti hiyo kwa Spika Anne Makinda jana mchana.

Wajumbe wengine wa timu hiyo ni Angellah Kairuki (Viti Maalumu-CCM), Mussa Zungu (Ilala-CCM) na John Cheyo (Bariadi Mashariki-UDP).

Kwa nyakati tofauti, wabunge hao waliwaeleza waandishi wa habari mjini hapa jana kuwa imegundua madhambi ya kutisha katika sakata la ununuzi wa rada hiyo ya kijeshi yanayoweza kuwatia hatiani wahusika.

Ingawa wajumbe hao hawakuwataja watuhumiwa hao kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Andrew Chenge, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), ni mtuhumiwa namba moja na aliyekuwa Gavana wa BoT, Dk Idrisa Rashid.

Wakati wa uchunguzi wa sakata hilo, Kampuni ya SFO ilibaini zaidi ya Dola za Marekani 1.2milioni kwenye akaunti ya Chenge iliyoko katika kisiwa cha Jersey nchini Uingereza. Lakini alipohojiwa na waandishi wa habari, Chenge alisema 'hivi ni vijisenti tu'

"Miongoni mwa mapendekezo yake (ripoti) kwa Serikali ni kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote waliohusika kwenye ufisadi huo," alisema mmoja wa wajumbe wa timu hiyo.

Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa imeweza kufichua mlolongo wa kashfa na njama ambazo zilitengenezwa nchini Uingereza ili kufunika uovu huo ambao ni wizi dhidi ya fedha za Watanzania.

Wakizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, timu hiyo ilisema, mbali na kupendekeza wahusika katika sakata hilo washtakiwe, walitaka pia Bunge na Serikali kushirikiana kwa karibu hadi fedha ambazo Tanzania inazidai kutoka Kampuni ya BAE System, zipatikane.

Cheyo, mmoja wa wajumbe wa timu hiyo, hakuwapo katika mazungjmzo hayo na waandishi wa habari jana.

Wabunge hao walisema katika safari yao wamegundua mengi ikiwa ni pamoja na namna uovu huo wa kifisadi ulivyozimwa ili dunia isifahamu.
 
Leo ndio wanaona hivyo???hawakujua toka mwanzo kama wamefanya makosa???mbona hao hao wabunge wa CCM wanawatetea hao mafisadi kwamba wasichukuliwe hatua????inatia huruma sana kwa kweli......
 
Wasituletee za kuletwa wamegonga mwamba ndipo wanajifanya kusema ukweli
kwanza waturudishie pesa zetu walizotumia huko wasifikiri tumesahau wanafiki wakubwa.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hii inaonyesha wazi kwamba wabunge wa CCM ni wabinafsi, wako pale bungeni kwa ajili ya kutetea maslahi ya watanzania wanyonge bali kwa maslahi yao binafsi.Hilo liko wazi.kila mtu analijua,lakini utakuta bado leo hii kuna watu wanaishabikia CCM.Ningependa kuona CDM wanakwenda na sehemu za vijini kufanya mikutanano yao ya hadhara ili kuwajulisha wananchi wa kule vijijini uovu na unyonyaji wa CCM.Imefika wakati sasa watanzania tuamkeni tutete taifa letu linaangamia.Hakuna asiyejua kwamba Tanzania ina utajiri.
 
Hii habari inawaweka wabunge wa ccm (wote) hatiani kwa kupinga hoja za msingi toka Lissu na hasa Mh Chikawe aliyesema serikali haina ushahidi.
Nadhani serikali na hata wabunge wa ccm kupitia kwa MSAADA mkubwa wa Spika Makinda wamedhihirisha madhara ya kuongoza nchi kwa MAZOEA. Kwa wabunge wa bunge la Tanzania kwenda kudai hela London only to be shown evidence ya 'mchongo' wa hii chenji ni aibu kwa bunge, serikali na hata Taifa. Na pengine hili linatupa mwanga ni kwa nini hukumu iliyotelewa iliweka 'kipengele' cha kuzuia Serikali kushika hizi hela. Judge atakuwa amejiridhisha kuwa Serikali itatumia hizi hela vibaya.

Mimi ningeshukuru kama mbunge mmoja angeuliza (hasa wakati wa bajeti ya Foreign) nani aliwatuma hawa wabunge wanne London? Kwa mamlaka gani? na walikuwa wanaimwakilisha nani? Na hawa wabunge wanne walikuwa na taarifa gani kuhusu wahusika kwa upande wa Tanzania?
Hapa hawawezi kusema hawana taarifa kwa sababu cheque iliandikwa na mtu hai (a human being) kwa niaba ya serikali ya Tanzania, na huyo mtu lazima atakuwa ameandika cheque baada ya mchakato wa makubaliano ya bei na BAE Systems. Sasa nani alihusika kwenye mchakato wa kujua bei?

Hii issue inaweza kuwapa shida ccm kuliko wanavyodhani. Na kwa majibu ya Mh. Chikawe bungeni nadhani atakuwa amewasha moto kwa raia kufuatilia kwa karibu hii kashfa.
 
Kama mnatetea fedha ziende serikalini ili BAE wasijisfu wametoa msaada, mbona naona kamaa hoja hiyo ni dhaifu sana! Sisi tunataka fedha zetu watanzania zitufikie salama. Kama BAE walikubali makosa wakatubu wakarudisha fedha zote, mbona sisi tunaona hili ni jambo jema kuliko nyie CCM mmekazana kuficha ujambazi huu kwa kumsafisha Chenge na kujitetea kuwa hapakua na kosa lakini chenji mnataka! Anzeni na mafisdi wenu kwanza! Wakirudisha zote ndio tuwaamini kwa hizo za BAE
 
Jamani... Makala ndefe wana JF zifupisheni ..andika walau hata haya( paragraph) moja harafu weka chanzo cha hiyo makala kwa mfuatiliaji au atakaependa kuisoma kwa kirefu kuifuata huko kuliko kuifanya saver yetu kubeba vitu visivyo vya lazima.... Maoni binafsi lakini...
 
Their sin will find them out. Vichaa wakikutana kama hiyo mi-abnormal political animals. They shud be screwed afterall.
 
Malaria sugu na wale vijana wa nepi aliowapandza wajtoze hapa na dhamiri zao mfu dhidi ya nchi yao.
Wameanza mgomo baridi wanataka nyongeza ya mshahara na posho ya mazingira magumu maana wengine wanakesha kwenye key bodi.
Kama unafikiri utani tafuta kuna thread alianzisha Maralia Sugu akiomba msaada kwa viongozi wa CCM kuwa wamezidiwa humu JF.
 
Kutegemea chochote kutoka kwa mwenye kichaaa kama hawa wabunge wa ccm ni kutegema inzi aongee na kukana anakula uchafu.
ccm sio chama ni genge la mafia
 
hivi serikali iantaka ushahidi kutoka source gani ndio ione inafaa? au kwa kuwa kila ushahidi unaotolewa unatoka upande wa wapinzani? sidhani kama kwa style hii tutafika
 
SAKATA LA RADA:Kina Ndugai wataka kina Chenge washitakiwe

TIMU ya wabunge walioenda nchini Uingereza kufuatilia malipo ya rada kwa Serikali ya Tanzania imekabidhi ripoti yake kwa Spika wa Bunge inayopendekeza mambo mawili, ikiwamo kushtakiwa kwa wahusika wa sakata hilo hapa nchini.Timu hiyo ya wabunge wanne ikiongozwa na Naibu Spika, Job Ndugai, ilimkabidhi ripoti hiyo kwa Spika Anne Makinda jana mchana.

Wajumbe wengine wa timu hiyo ni Angellah Kairuki (Viti Maalumu-CCM), Mussa Zungu (Ilala-CCM) na John Cheyo (Bariadi Mashariki-UDP).

Kwa nyakati tofauti, wabunge hao waliwaeleza waandishi wa habari mjini hapa jana kuwa imegundua madhambi ya kutisha katika sakata la ununuzi wa rada hiyo ya kijeshi yanayoweza kuwatia hatiani wahusika.

Ingawa wajumbe hao hawakuwataja watuhumiwa hao kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Andrew Chenge, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), ni mtuhumiwa namba moja na aliyekuwa Gavana wa BoT, Dk Idrisa Rashid.

Wakati wa uchunguzi wa sakata hilo, Kampuni ya SFO ilibaini zaidi ya Dola za Marekani 1.2milioni kwenye akaunti ya Chenge iliyoko katika kisiwa cha Jersey nchini Uingereza. Lakini alipohojiwa na waandishi wa habari, Chenge alisema 'hivi ni vijisenti tu'

"Miongoni mwa mapendekezo yake (ripoti) kwa Serikali ni kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote waliohusika kwenye ufisadi huo," alisema mmoja wa wajumbe wa timu hiyo.

Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa imeweza kufichua mlolongo wa kashfa na njama ambazo zilitengenezwa nchini Uingereza ili kufunika uovu huo ambao ni wizi dhidi ya fedha za Watanzania.

Wakizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, timu hiyo ilisema, mbali na kupendekeza wahusika katika sakata hilo washtakiwe, walitaka pia Bunge na Serikali kushirikiana kwa karibu hadi fedha ambazo Tanzania inazidai kutoka Kampuni ya BAE System, zipatikane.

Cheyo, mmoja wa wajumbe wa timu hiyo, hakuwapo katika mazungjmzo hayo na waandishi wa habari jana.

Wabunge hao walisema katika safari yao wamegundua mengi ikiwa ni pamoja na namna uovu huo wa kifisadi ulivyozimwa ili dunia isifahamu.

Angellah alisema kuwa timu hiyo ya wabunge ilibaini pia kuwa Serikali ya Tanzania ilikuwa imekatazwa na SFO isiwachukulie hatua watuhumiwa wa hapa nchini kwa sababu ingekuwa ni mwingiliano wa kesi mahakamani.

Alisema kwa sasa ambapo tayari mahakama ya Uingereza imetoa hukumu, Tanzania iko huru kuwachukulia hatua wahusika. Pamoja na hali hiyo, alisema nguvu kubwa kwa sasa ielekezwe katika kuiwezesha Tanzania kupata fedha hizo bila mizengwe.

Alisema kama Serikali ya Tanzania inataka kuwashtaki inapaswa kupata pia ushahidi wa SFO ambao waliutumia kuibana BAE hadi ikaamua irejeshe fedha zote.

Kuhusu uwezekano wa kuwaunganisha maofisa wa BAE kwenye kesi hiyo, Ndugai alisema kuwa tatizo ni kwamba waliohusika kwenye mpango huo tayari wameondolewa kwenye kampuni hiyo.

Zungu alisema mkakati wao ni kwamba iwapo kampuni ya BAE haitatoa fedha hizo hadi Desemba mwaka huu, Serikali ya Tanzania ifungue upya mashtaka nchini Uingereza.

Kwa upande wake, Ndugai alianza kwa kuelezea lilikoanzia sakata hilo, akisema: "kama mnavyojua Desemba 20 mwaka jana mahakama nchini Uingereza ilitoa hukumu ambayo iliiadhibu kampuni ya BAE kulipa fidia ya paundi 29 milioni kwa Tanzania."

Alisema Kampuni ya Kuchunguza Rushwa kubwa kubwa nchini Uingereza ya (SFO) ndiyo iliyofungua mahakamani kesi hiyo. Ndugai alisema kwa kuwa BAE ilibaini kuwa shtaka hilo lilikuwa ni zito na lingeweza kuharibu sifa ya kampuni hiyo duniani, walifanya mpango wa kesi hiyo kuzungumzwa nje ya mahakama na kufanikiwa.

Wakiwa nje ya mahakama, Ndugai alisema BAE walitengeneza mkataba na kusema kwamba watarejesha fedha zote ambazo Tanzania ilinunulia rada hiyo pamoja na fidia.

"Yaani walifanya kana kwamba rada hiyo Tanzania imepewa bure. Maana walinunua kwa pauni 28 milioni na sasa wanatoa pauni 29.3 milioni," alisema Ndugai. Alifafanua kuwa mkataba huo ulikuwa ni wa kufunika aibu na uliandikwa na mwanasheria wa BAE huku ukieleza kuwa fedha hizo zitatolewa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ili yatoe huduma za kijamii.

Alisema hata kabla kesi hiyo haijaenda mahakamani, walitoa mapendekezo ya fidia itakayopatikana iletwe nchini ili kununua madawati na kujenga nyumba za walimu kwa kuwa waathirika ni Watanzania.

Baada ya makubaliano hayo ya nje ya mahakama, Ndugai alisema SFO na BAE walikubaliana kesi iliyoko mahakamani ijulikane kuwa ni ya kosa la kushindwa kuweka vizuri kumbukumbu.

Alisema SFO na BAE wakaingia mkataba wa kufunga faili la uchunguzi kuhusu kashfa hiyo ikiwa na maana kwamba uozo uliofanyika hautatolewa kwa namna yoyote kwa chombo chochote.

Ndugai alizidi kueleza kuwa hii ni njama kati ya SFO na BAE ya kutotaka madhambi yaliyofanywa katika ununuzi huo wa rada yasiwekwe hadharani na dunia ikafahamu.

Hata hivyo, Ndugai alisema kamati yake imegundua ujanja huo na kwamba kitendo cha kusema fedha hizo ziende kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ya kuisaidia jamii, ni njia ya kuzitumia wao wenyewe.

"Wao wanataka ionekane BAE wametoa msaada halafu wafanye safari za kuja nchini kwa ndege na walipane posho halafu mwisho wa siku fedha nyingi watatumia wao," alilalamika Ndugai.

Ndugai alisema fedha hizo zitolewe kwa Serikali ya Tanzania na zisimamiwe na Bunge katika kutengeneza madawati na nyumba za walimu na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG) aweze kuzikagua.

"Zikitolewa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali, CAG hataweza kuzikagua na hata matumizi yake yakipindishwa hakuna namna ya kuwabana wahusika," alisema Ndugai.

Akizungumzia kuhusu safari yao ya Uingereza, Zungu alisema walichogundua ni kwamba BAE ilifanya mchezo mchafu kuanzia ununuzi wa rada hadi kuficha madhambi yake kwa kutaka kesi izungumzwe nje ya mahakama.

Taarifa zao kuvuja
Alilalamika kuwa hata baadhi ya wabunge wa upinzani waliozungumzia suala hilo juzi, ilitokana na kuvuja kwa taarifa za ripoti yao.

Hakumtaja mbunge huyo wa upinzani, lakini John Mnyika ndiye aliyeliambia Bunge kuwa fedha hizo zisipelekwe serikalini kwa sababu walishindwa kuzisimamia na wala hawakuomba washirikishwe kwenye kesi hiyo.

Zungu alilalamika kuwa miongoni mwa lawama dhidi ya SFO ni kutoshirikisha Tanzania kwenye kesi hiyo hasa ikizingatiwa kuwa iliwasiliana na Takukuru ili kupata ushahidi ambao uliisaidia kuibana BAE.


Lakini akamsifu Jaji aliyeamua kesi hiyo kwa sababu alisisitiza kuwa dhuluma hiyo ilikuwa ni dhidi ya wananchi wa Tanzania hivyo lazima fedha hizo zipelekwe moja kwa moja kwa manufaa ya waathirika hao.

Zungu alisema kuwa Jaji aliamua itozwe fidia ndogo ya paundi 500,000 katika fedha hizo ili zigharimie kesi hiyo.

Zungu alionya kuwa kama mshikamano hautakuwapo katika suala hilo, BAE itatumia fedha za Watanzania na kujigamba imetoa msaada.

Alisema katika Bunge la Uingereza, Tanzania inasifiwa kuwa imekuwa ikitumia vizuri fedha za misaada na wanaridhika iendelee kupewa misaada.

"Sasa kitendo cha kutoa fedha hizi, zilizotoka mikononi mwa Serikali ziende kwa asasi za kiraia kwa madai kwamba hazitatumika vizuri ni udhalilishaji mkubwa," alieleza Zungu.

Alisema kamati hiyo ilipanga kukutana na Mkurugenzi wa SFO, Richard Agaman, lakini alikataa huku akisema yuko tayari kuwasiliana na balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Zungu alisema balozi huyo alisema mkurugenzi huyo wa SFO aliomba radhi kwa kutoshirikisha Serikali ya Tanzania kwenye kesi hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom