Lissu tambua unaishi katika Taifa ambalo wengi wana mitazamo ya aina hii

Tundu Lissu, tambua unaishi katika Taifa la watu ambao wengi wao wanaamini uzalendo ni kusubiri Raisi aseme nini na wao kisha wamuunge mkono.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini kuhoji au kukosoa anachosema Raisi si uzalendo.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengu wanaamini ukiona jambo halija kaa sawa si busara kulisema au kulihoji mpaka kwanza Raisi wa nchi ahoji au alianzishe.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo,mawazo ya wapinzani si chochote mpaka mawazo hayo yatolewe na Raisi,CCM au kamati za kiuchunguzi zilizoundwa na Raisi.

Lisssu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini hata mapendekezo ya kamati za kiuchunguzi zinazoundwa na mtu mwenye wadhifa wa uraisi, mapendekezo hayo yanakuwa na maana tu iwapo Raisi atayakubali mapendekezo hayo.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo ni uzalendo kusubiri Raisi tu aanzishe jambo na si wapinzani au mtu mwingne yoyote.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo si uzalendo kwa vyombo vya habari kutoa support kwa mawazo mazuri ya wapinzani ila ni uzalando tu kwa vyombo vya habari kutoa support kubwa kwa yale anayoyasema au kuyaanzisha Raisi.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini wapinzani hawajakomaa ila waliokomaa ni wale wanaondesha nchi inayoporwa na wawekezaji kila kukicha.

Lissu,tambua unaishi katika nchi ambayo watu wengi wanaamini kuhoji busara au maamuzi ya Raisi ni kukosa heshima.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini si uzalendo kutambua mchango wa wapinzani bali ni uzalendo tu kutambua mchango wa Raisi na chama chake.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wenhi wanaamini si uzalendo na pia ni kukosa adabu kuwakumbusha watawala kuwa ni wao wametufikisha hapa kama nchi bali ni uzalendo kuwapigia makofi pale wanapojaribu kujirekebisha hata kabla hawajaanza kujirekebisha.

Tundu Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini Raisi akitoa ahadhi kila mtu anapaswa kushangilia hata kabla ahadi hiyo haijaanza kutekelezwa na usipofanya hivyo wewe si mzalendo.

Mwisho,tambua kuwa unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini chama tawala tu ndio chama chenye watu wastaarabu na wenye busara na ambao ndio wanaofaa kuongoza hii nchi na wapinzani ni watu wahuniwahuni tu,wapiga dili na wasio na uwezo wa kuongoza nchi.

Lissu,nakutahadharisha utambue mapema kabisa kuwa,katika Taifa la watu wa aina hii,usishangae zikaibuka hoja za kutaka kumtunukia Mkulu nishani ya kulinda za maliasili za nchi hii wakati wewe uliekaa jela ukipinga mikataba na sheria zilizotufikisha hapa ukipigwa vita na kuitwa msaliti.

Hivyo,ndugu yangu Lissu ueleww utapata shida sana kuishi katika nchi hii kwasababu huu ndio mtazamo wa wengi katika hii nchi japo si wa kila mtanzania.

Nina mashaka sana na IQ ya walio wengi katika hii nchi kuanzia wasomi na wasio wasomi.

Sometime huwa nahisi huenda ulipaswa kuzaliwa katika nchi za wenzetu ambako huenda ungeweza kupata recognition lakini ni bahati mbaya umezaliwa katika nchi yetu.
Kwa hiyo?
 
Lisu siku hivi ukijitokeza maeneo kama kakola au kahama sijui kama hutapigwa nawe na wanachi na wachimbaji walisha sahau utetezi wako wamabadili gia angani kikuona ni mshitiki wa acacia. Tambua na hilo
 
Mimi pongezi zangu ziwaendee Anna Mughwira mkuu wa mkoa wa kilimanjaro,na Zitto kabwa Mb kigoma mjini,lissu na genge lake wamedandia tu kama wanavyodandiaga misiba na kuzurura nayo mitaani
 
Tundu Lissu, tambua unaishi katika Taifa la watu ambao wengi wao wanaamini uzalendo ni kusubiri Raisi aseme nini na wao kisha wamuunge mkono.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini kuhoji au kukosoa anachosema Raisi si uzalendo.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengu wanaamini ukiona jambo halija kaa sawa si busara kulisema au kulihoji mpaka kwanza Raisi wa nchi ahoji au alianzishe.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo,mawazo ya wapinzani si chochote mpaka mawazo hayo yatolewe na Raisi,CCM au kamati za kiuchunguzi zilizoundwa na Raisi.

Lisssu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini hata mapendekezo ya kamati za kiuchunguzi zinazoundwa na mtu mwenye wadhifa wa uraisi, mapendekezo hayo yanakuwa na maana tu iwapo Raisi atayakubali mapendekezo hayo.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo ni uzalendo kusubiri Raisi tu aanzishe jambo na si wapinzani au mtu mwingne yoyote.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo si uzalendo kwa vyombo vya habari kutoa support kwa mawazo mazuri ya wapinzani ila ni uzalando tu kwa vyombo vya habari kutoa support kubwa kwa yale anayoyasema au kuyaanzisha Raisi.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini wapinzani hawajakomaa ila waliokomaa ni wale wanaondesha nchi inayoporwa na wawekezaji kila kukicha.

Lissu,tambua unaishi katika nchi ambayo watu wengi wanaamini kuhoji busara au maamuzi ya Raisi ni kukosa heshima.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini si uzalendo kutambua mchango wa wapinzani bali ni uzalendo tu kutambua mchango wa Raisi na chama chake.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wenhi wanaamini si uzalendo na pia ni kukosa adabu kuwakumbusha watawala kuwa ni wao wametufikisha hapa kama nchi bali ni uzalendo kuwapigia makofi pale wanapojaribu kujirekebisha hata kabla hawajaanza kujirekebisha.

Tundu Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini Raisi akitoa ahadhi kila mtu anapaswa kushangilia hata kabla ahadi hiyo haijaanza kutekelezwa na usipofanya hivyo wewe si mzalendo.

Mwisho,tambua kuwa unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini chama tawala tu ndio chama chenye watu wastaarabu na wenye busara na ambao ndio wanaofaa kuongoza hii nchi na wapinzani ni watu wahuniwahuni tu,wapiga dili na wasio na uwezo wa kuongoza nchi.

Lissu,nakutahadharisha utambue mapema kabisa kuwa,katika Taifa la watu wa aina hii,usishangae zikaibuka hoja za kutaka kumtunukia Mkulu nishani ya kulinda za maliasili za nchi hii wakati wewe uliekaa jela ukipinga mikataba na sheria zilizotufikisha hapa ukipigwa vita na kuitwa msaliti.

Hivyo,ndugu yangu Lissu ueleww utapata shida sana kuishi katika nchi hii kwasababu huu ndio mtazamo wa wengi katika hii nchi japo si wa kila mtanzania.

Nina mashaka sana na IQ ya walio wengi katika hii nchi kuanzia wasomi na wasio wasomi.

Sometime huwa nahisi huenda ulipaswa kuzaliwa katika nchi za wenzetu ambako huenda ungeweza kupata recognition lakini ni bahati mbaya umezaliwa katika nchi yetu.
Maneno machache tu yanakutosha SS kuwa. Unaweza ukawa na point lakini ukakosema approach. Mfano wa muhubiri atoke kuwa anaenda kuhubiri mahali, kisha wale anaotaka kuwahubiri aanze kuwatukana kuwadharau na kuwafanyia kejeri, je unadhani mhubiri huyo atafanikiwa katika mahubiri yake?

Issue ya Mchanga yeye hakupaswa kuanza kutukana na kutuogopesha kama taifa, yeye alipaswa kutambua kuwa kile kilio chetu sasa kimesikilizwa na huu ndio wakati muafaka wa kutumia ujuzi wangu wa sheria kuhakikisha tunawashikisha adabu wezi na wale watanzania waliopewa dhamana wakatuingiza ktk majanga.

Ss mwambie Lisu anapotaka kuongea awe anaanza kwa kumlaani shetani kwani huwa anampanda kichwani na kumtia hasira nyingi na kiburi, kiburi kinachompelekea hata kutowaheshimu watu ambao hata kiumri hawalingani.
 
Miaka ya nyuma chadema huku zitto, kule Slaa, mitandaoni vijana lukuki, kwingineko mnyika, ukigeuka kushoto mbowe...
Sikuhizi medulla oblangata ya chama kaachiwa lissu ...
Wengine wako katika hatia ya mabadiliko ya Gia angani...
ndio ulichobakiza kwenye medulla oblangata yako
 
Kama kawaida yako unahangaika sana. Tatizo lake ni kuwa yeye alitakiwa kuangalia maslahi ya nchi kwa vile ni President wa TLS. Alisema ripoti ni RUBBISH umesahau?
Tundu lissu sio msalati tofauti tu ninamuna ya kuaproach hii inshu.
Alichokisema lissu ni kwamba mikataba ndo mibovu kupindukia na tunapigwa kweli na kasema tulireview hiyo mikataba au kukaa meza moja nao lakini Leo Rais Wetu amesema hayo hayo baada ya kamati zote mbili kuwasilia ripoti zao.
Tusichukie watu bila sababu sema nachoona kuwa Tundu Lissu huwa anatumiaga lugha Kali lakini ukweli utabaki vilevile kilichoibiwa kupitia mikataba ni kikubwa kuliko kwenye Mchanga(geology point of view).
Unajaza server bure. Umaarufu wa kulazimisha mwisho Singida
 
Lissu tambua kwamba unaishi ktk taifa linalofikili Raisi hakosei akiwa madarakani lkn akitoka ndiyo anakosea
Tambua kuwa unaishi ktk Taifa ambalo muda wa jpm ukiisha ndio watakuwa wa kwanza kumponda na kumsifia aliyepo kama mzalendo
 
Back
Top Bottom