Lissu tambua unaishi katika Taifa ambalo wengi wana mitazamo ya aina hii

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,850
Tundu Lissu, tambua unaishi katika Taifa la watu ambao wengi wao wanaamini uzalendo ni kusubiri Raisi aseme nini na wao kisha wamuunge mkono.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini kuhoji au kukosoa anachosema Raisi si uzalendo.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengu wanaamini ukiona jambo halija kaa sawa si busara kulisema au kulihoji mpaka kwanza Raisi wa nchi ahoji au alianzishe.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo,wengi wanaamini mawazo ya wapinzani si chochote mpaka mawazo hayo yatolewe na Raisi,CCM au kamati za kiuchunguzi zilizoundwa na Raisi.

Lisssu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini hata mapendekezo ya kamati za kiuchunguzi zinazoundwa na mtu mwenye wadhifa wa uraisi, mapendekezo hayo yanakuwa na maana tu iwapo Raisi atayakubali mapendekezo hayo.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo wengi wanaaamini ni uzalendo kusubiri Raisi tu aanzishe jambo na si wapinzani au mtu mwingne yoyote.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo wengi eana mtazamo kuwa si uzalendo kwa vyombo vya habari kutoa support kwa mawazo mazuri ya wapinzani ila ni uzalando tu kwa vyombo vya habari kutoa support kubwa kwa yale anayoyasema au kuyaanzisha Raisi.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini wapinzani hawajakomaa ila waliokomaa ni wale wanaondesha nchi inayoporwa na wawekezaji kila kukicha.

Lissu,tambua unaishi katika nchi ambayo watu wengi wanaamini kuhoji busara au maamuzi ya Raisi ni kukosa heshima.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini si uzalendo kutambua mchango wa wapinzani bali ni uzalendo tu kutambua mchango wa Raisi na chama chake.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini si uzalendo na pia ni kukosa adabu kuwakumbusha watawala kuwa ni wao wametufikisha hapa kama nchi bali ni uzalendo kuwapigia makofi pale wanapojaribu kujirekebisha hata kabla hawajaanza kujirekebisha.

Tundu Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini Raisi akitoa ahadi kila mtu anapaswa kushangilia hata kabla ahadi hiyo haijaanza kutekelezwa na usipofanya hivyo wewe si mzalendo.

Vile vie kila siku katika ukosoaji wako, unawapa ushauri/unaonyesha njia lakini tambua hakuna atakaekushukuru pale wanapochukua mawazo yako na kuyafanyika kazi bali tambua siku zote atapongezwa na kusifiwa yule tu aliebeba mawazo yako na kuyafanyia kazi.

Mwisho,tambua kuwa unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini chama tawala tu ndio chama chenye watu wastaarabu na wenye busara na ambao ndio wanaofaa kuongoza hii nchi na wapinzani ni watu wahuniwahuni tu,wapiga dili na wasio na uwezo wa kuongoza nchi.

Lissu,nakutahadharisha utambue mapema kabisa kuwa,katika Taifa la watu wa aina hii,usishangae zikaibuka hoja za kutaka kumtunukia Mkulu nishani ya kulinda za maliasili za nchi hii wakati wewe uliekaa jela ukipinga mikataba na sheria zilizotufikisha hapa ukipigwa vita na kuitwa msaliti.

Lissu,hata yale uliotuonya yakitokea yote au baadhi,tambue wote wataa kimya na badala yake watasema Mkulu alishauriwa vibaya na hakuna atakaeatmka hadharani kusema Lissu aliwahi kututahadharisha.

Hivyo,ndugu yangu Lissu, uelewe utapata shida sana kuishi katika nchi hii kwasababu huu ndio mtazamo wa wengi katika hii nchi japo si wa kila mtanzania.

Nina mashaka sana na IQ ya walio wengi katika hii nchi kuanzia wasomi na wasio wasomi.

Sometimes huwa nahisi huenda ulipaswa kuzaliwa katika nchi za wenzetu ambako huenda ungeweza kupata recognition lakini ni bahati mbaya umezaliwa katika nchi yetu.
 
Miaka ya nyuma chadema huku zitto, kule Slaa, mitandaoni vijana lukuki, kwingineko mnyika, ukigeuka kushoto mbowe...
Sikuhizi medulla oblangata ya chama kuachiwa lissu lazima....
Wengine wako katika hatia ya mabadiliko ya Gia angani...

749ce279e77703001d13b9d386e92a2b.jpg
 
Lisu namfananisha na Mbwana Samata, wanaishi katika taifa ambalo wanaoishi nao wapo mbali nao hawakustahili kuwa katika taifa kama hili ambalo hata wasomi wanaongozwa na mitizamo ya kisiasa, na hivyo kukosa dhana nzima ya kuwa wasaidizi wa jamii husika. Hayati legendari Deo Filikunjombe walimuondoa mapema sababu aliwaambia ukweli kuwa CCM sio waaminifu. Maneno yake na kivuli chake vinaishi. R.I.P DEO
 
Tundu Lissu, tambua unaishi katika Taifa la watu ambao wengi wao wanaamini uzalendo ni kusubiri Raisi aseme nini na wao kisha wamuunge mkono.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini kuhoji au kukosoa anachosema Raisi si uzalendo.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengu wanaamini ukiona jambo si busara kulisema au kulihoji mpaka Raisi wa nchi ahoji au alianzishe.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo,mawazo ya wapinzani si chochote mpaka mawazo hayo yatolewe na Raisi,CCM au kamati za kiuchunguzi zilizoundwa na Raisi.

Lisssu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini hata mapendekezo ya kamati za kiuchunguzi zinazoundwa na mtu mwenye wadhifa wa uraisi mapendekezo hayo yanakuwa na maana tu iwapo Raisi atayakubali mapendekezo hayo.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo ni uzalendo kusubiri Raisi tu aanzishe jambo na si wapinzani au mtu mwingne yoyote.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo si uzalendo kwa vyombo vya habari kutoa support kwa mawazo mazuri ya wapinzani ila ni uzalando tu kwa vyombo vya habari kutoa support kubwa kwa yale anayoyasema au kuyaanzisha Raisi.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini wapinzani hawajakomaa ila waliokomaa ni wale wanaondesha nchi inayoporwa na wawekezaji kila kukicha.

Lissu,tambua unaishi katika nchi ambayo watu wengi wanaamini kuhoji busara au maamuzi ya Raisi ni kukosa heshima.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini si uzalendo kutambua mchango wa wapinzani bali ni uzalendo tu kutambua mchango wa Raisi na chama chake.

Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wenhi wanaamini si uzalendo na pia ni kukosa adabu kuwakumbusha watawala kuwa ni wao wametufikisha hapa kama nchi bali ni uzalendo kuwapigia makofi pale wanapojaribu kujirekebisha hata kabla hawajaanza kujirekebisha.

Tundu Lissu,tambua unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini Raisi akitoa ahadhi kila mtu anapaswa kushangilia hata kabla ahadi hiyo haijaanza kutekelezwa na usipofanya hivyo wewe si mzalendo.

Mwisho,tambua kuwa unaishi katika Taifa ambalo watu wengi wanaamini chama tawala tu ndio chama chenye watu wastaarabu na wenye busara na ambao ndio wanaofaa kuongoza hii nchi na wapinzani ni watu wahuniwahuni tu,wapiga dili na wasio na uwezo wa kuongoza nchi.

Lissu,nakutahadharisha utambue mapema kabisa kuwa,katika Taifa la watu wa aina hii,usishangae zikaibuka hoja za kutaka kumtunukia Mkulu nishani ya kulinda za maliasili za nchi hii wakati wewe uliekaa jela ukipinga mikataba na sheria zilizotufikisha hapa ukipigwa vita na kuitwa msaliti.

Hivyo,ndugu yangu Lissu ueleww utapata shida sana kuishi katika nchi hii kwasababu huu ndio mtazamo wa wengi katika hii nchi japo si wa kila mtanzania.

Nina mashaka sana na IQ ya walio wengi katika hii nchi kuanzia wasomi na wasio wasomi.

Sometime huwa nahisi huenda ulipaswa kuzaliwa katika nchi za wenzetu ambako huenda ungeweza kupata recognition lakini ni bahati mbaya umezaliwa katika nchi yetu.
Kama kawaida yako unahangaika sana. Tatizo lake ni kuwa yeye alitakiwa kuangalia maslahi ya nchi kwa vile ni President wa TLS. Alisema ripoti ni RUBBISH umesahau?
 
Mbona chadema wakati wa kampeni huko kakola (buliankulu) hawakuongelea chochote, zaidi ya kukata viuno na kuzungusha mikono au walihongwa tofali la zahabu.
 
Miaka ya nyuma chadema huku zitto, kule Slaa, mitandaoni vijana lukuki, kwingineko mnyika, ukigeuka kushoto mbowe...
Sikuhizi medulla oblangata ya chama kaachiwa lissu ...
Wengine wako katika hatia ya mabadiliko ya Gia angani...
Mnahangaika sana ila yale ya miaka 20 ndo leo mnaamka. Hata miaka ile mlikejeli. Bado. Miaka 20 ijayo mtahangaika ..... AAAAH HAMTAKUWEPO!!!!!!!!!!
 
Mbona chadema wakati wa kampeni huko kakola (buliankulu) hawakuongelea chochote, zaidi ya kukata viuno na kuzungusha mikono au walihongwa tofali la zahabu.
Una matatizo wewe. Lowassa alisemea wapi kuhusu kuvunja mikataba hiyo?
 
Mbona chadema wakati wa kampeni huko kakola (buliankulu) hawakuongelea chochote, zaidi ya kukata viuno na kuzungusha mikono au walihongwa tofali la zahabu.
Tofali alipewa Mkapa. Usisahau. Karamagi alisaini mkataba London waliwa safarini nje na Kikwete. Rudi makala za nyuma JF.
 
Hili suala la migodi ni chama cha ACT chini ya zitto na Anna Mugwira ndio waliobebea bango,sio CDM.
 
Back
Top Bottom