Lissu; Nia njema ya Magufuli inatupeleka pabaya

Je aliwahi kuwashawishi wabunge wenzio wa CCM wakati akiwa mbunge katika kuikataa hii mikataba wakati wanaipitisha kisheria?
Mkuu unajua unapokuwa kwenye serikali nafasi kama mbunge/waziri ukaikosoa serikali unakuwa adui yao, alichaofanya Rais Magufuli ni kuwa mkimya na kutafuta nafasi ya juu ili ashughulikia suala hili kikamilifu.
 
wingi wa wabunge wa CCM bungeni ndiyo Sumu ya kupitisha mikataba mibovu na kutunga sheria mbaya.sasa wanajidai kuwahadaa watanzania kwa kufukua makaburi ya marehemu waliouawa na CCM wenyewe lakini wanataka wasaidiwe na watanzania wote.
Wakati wanaingia kwenye mikataba waliomba wapi msaada?msaada tuombane mambo yameharibika??
 
Mkuu unajua unapokuwa kwenye serikali nafasi kama mbunge/waziri ukaikosoa serikali unakuwa adui yao, alichaofanya Rais Magufuli ni kuwa mkimya na kutafuta nafasi ya juu ili ashughulikia suala hili kikamilifu.
Kwa hiyo hapo unamaanisha Akili pembeni, Udokta pembeni, Uprofesa pembeni, na Sifa zote za kiongozi mzalendo pembeni inabaki ''Ndioooooo" ndio Uzalendo?

Kumbuka unafiki ni kitu kibaya sana na ndio jambo ambalo wengi wetu tunalo.
 
Naona Lisu analialia tu lakini hatoi mapendekezo mahsusi ya nini kifanywe.

Mimi ningekuwa ndo Magufuli ningemwomba huyo Lisu atoe mapendekezo halafu niyafuate hayo mapendekezo yake tuone tutakapofika.

Maana kupiga mayowe kama mwendawazimu na kusubiri wenzio watende na wewe ndiyo ujitokeze uanze kuwakosoa ni kazi rahisi sana.
Mkuu mbona mapendekezo ameyatoa kwamba kila kitu lazima kianzie kwenye kuzibadilisha sheria zilizowekwa na serikali za CCM wenyewe kuwa favour hawa wawekezaji.
 
Hili jamaa halina mpango wowote. Rais katumia power yake kustopisha hujuma ya nchi lenyewe linapiga kelele sheria, sheria, ina maana rais abadili sheria ndio aje kuzuia wizi?

Nyama inaungua jikoni badala ya kuepua chungu unataka uende dukani ukanunue jiko jipya? Kama si ufala ni nini?

Hili jamaa halina credibility. Limemlaani Lowassa likamsafisha. Limechukua kesi ya Wema ya bangi. Lenyewe mradi tu lipinge serikali. Hapo linajistukia ooh mimi sijahongwa kuwatetea Acacia. Nani kakuuliza? Mwizi wa kuku usiku hukamatwa kwa kuwa na manyoya kichwani.
 
Huyu jamaa hajiamini na sijui anataka nini kila siku anarudia maneno yale yale. Huyu jamaa na genge lake wamewahi kusema hawamtambui Magufuli kama Rais, kwao Rais ni Lowasa (mamvi). Genge hili la mafisadi halijawahi kupongeza kazi inayofanywa na Magufuli. Tundu (tobo) Lissu kama hukuwahi kupongeza japo kwa unafiki kazi inayofanywa na Magufuli, hupaswi kusema nia yake inatupeleka pabaya kwa maana unaonekana huna msimamo mzee na maslahi yako yameguswa kaa pembeni tuache wanaume tupambane, tumeamua na haturudi nyuma!
Ndioooooo Mkuu endeleeni kuamua, lakini tusifichane kwenye malipo ya fidia na muandae press kama hii ya makanikia
 
Mkuu mbona mapendekezo ameyatoa kwamba kila kitu lazima kianzie kwenye kuzibadilisha sheria zilizowekwa na serikali za CCM wenyewe kuwa favour hawa wawekezaji.

nashindwa kuelewa hapa msichoelewa ni nini?kaonea three tymes SHERIA SHERIA SHERIA,akimanisha mkulu aanze na kubadili sheria,iko siku mtamuelewa TL,ambapo itakuwa too late
 
nashindwa kuelewa hapa msichoelewa ni nini?kaonea three tymes SHERIA SHERIA SHERIA,akimanisha mkulu aanze na kubadili sheria,iko siku mtamuelewa TL,ambapo itakuwa too late
Hawa watu hawawezi kutuelewa ila ipo siku wataelewa japo hawatadhihirisha.
Tusichoke kuwaelimisha
 
Huyu naye si wa kumwamini sana hata ikatokea kesho Lowasa na Sumaye wanapelekwa mahakamani huyo ndo atakuwa wa kwanza kuwatetea.
Na nina uhakika huenda hata huyo Lissu hajui anataka nini, anatumia na taaluma yake ya sheria kufanyia harakati kwa vile tu harakati zipo kwenye damu yake..!!!!
 
Ndioooooo Mkuu endeleeni kuamua, lakini tusifichane kwenye malipo ya fidia na muandae press kama hii ya makanikia

teh teh teh umenena mkuu hope na bashite kwenye press conference atakuepo ,lol
 
Huyu naye si wa kumwamini sana hata ikatokea kesho Lowasa na Sumaye wanapelekwa mahakamani huyo ndo atakuwa wa kwanza kuwatetea.
Na nina uhakika huenda hata huyo Lissu hajui anataka nini, anatumia na taaluma yake ya sheria kufanyia harakati kwa vile tu harakati zipo kwenye damu yake..!!!!

huenda una shida sehem au hutak kbs kusoma ,jitahidi kusoma,huenda ht huelewi ZIMBABWE wapo vipi kiuchumi na nia njema yao ya kutaka mali zao zimilikiwe na wazawa leo kiko wapi
 
hivi kila siku vizuri vitakuwa vya wanyonyaji na vibaya vyetu tu.tundu nakutazama kama mwanasheria mzuri wa kukingia kifua kesi hii.kwani we si mtanzania
 
Back
Top Bottom