Lissu; Nia njema ya Magufuli inatupeleka pabaya

Kumbe unazungumzia social media?? Be serious brother
We kiazi, huko social media mimi ndio niliowaandikia hao? Unadharau social media huku nawewe uko hapa hapa unatoa maoni yako na unataka yathaminiwe?
 
Ni kweli wengi tulikuwa carried away na findings za tume na tukaanza kupongeza kabla ya kuitafakari kwanza. Hata Mh. Rais alikuwa carried away na kujikuta anachukua maamuzi ya kutumbua watu instantly.
Baadae wengi tulipoanza kupiga yale mahesabu ya tume ya tani 7.8 za dhahabu ndio tukaelewa tumelishwa tango pori. Yani tani 7.8 ni sawa na troy ounce 250,755. Hiki ni kiwango kikubwa sana cha dhahabu kuweza kupatikana kwa MWAKA. Itakuwaje kipatikane kwenye makontena 277 ambayo ni uzalishaji wa MWEZI mmoja.
Kama unakumbuka kesho yake Tundu Lissu aligeuka na kuiponda ripoti ya tume kwa kuiita rubbish.
Kama ingekuwa findings za tume zina figure zenye uhalisia basi wala tusingekuwa tunabishana juu ya kama tutashindwa au kushinda tukienda mahakamani, japo bado utata ungejitokeza kuwa TMAA na TRA walikuwa wapi, but at least tungesema tumeibiwa. Ila kwa sasa hakuna hiyo chance. Ndio maana Acacia wanayaka tume huru...wanajua hakuna makosa ya kiwango kile kwenye data zao ambazo zilithibitishwa naTMAA na TRA na mnunuzi wa mchanga huo...
Hapo sasa ndipo inakuja concern ya Lissu kuwa as long as hatutaweza kuonyesha kuwa data zinazotumika ni za uongo then tutashindwa kesi asubuhi na mapema na kitakachofata ni kulipa mifidia maana kimkataba hakuna mahala mwekezaji amekiuka hata kipengele kimoja....

Kinachonichekesha kwenye hili sakata, watu mmeanza kurukia sheria sijui mikataba wakati tume iliyotumwa kushughulikia athari za kiuchumi na kisheria bado haijawasilisha ripoti yake. Mnawahi wapi?
 
Ala kumbe tungeanza na SHERIA - kama ni kweli basi hili ni kosa la kiufundi ingawa lina njema kabisa.
 
Lissu ni moja ya watu wanaotakiwa kuombewa sana sana sana kuliko hao wanaolazimisha kuombewa kila siku!!
 
Hatuwezi kuendesha nchi kwa misingi ya NIA NJEMA bali ni misingi ya SHERIA SAFI, MIKATABA SAFI NA KATIBA NZURI.Ni hao hao waliokataa katiba nzuri na sheria safi. Ni hao hao waliopitisha sheria za gesi haraka haraka wakipuuza madai ya wapinzani. Watanzania tuamke la sivyo tutabaki mifupa tu hao jamaa wakiendelea kutawala. Mbona hawataki kuwachukulia hatua walioandika na kusaini mikataba mibovu? Hayo ni makelele ya kutuzubaisha tu hayana nia njema ni ubabaishaji tu ambao utatuletea hasara kubwa taifa.
 
Kinachonichekesha kwenye hili sakata, watu mmeanza kurukia sheria sijui mikataba wakati tume iliyotumwa kushughulikia athari za kiuchumi na kisheria bado haijawasilisha ripoti yake. Mnawahi wapi?
Nisome na kunielewa vizuri. Katika michango yangu yote kuhusiana na suala hili hakuna sehemu nimezungumzia sheria na mikataba....sio eneo langu hilo. Nawasikiliza wenye uelewa huo. Mimi toka day one nilikataa hizo figures za Mruma kuwa haziwezekaniki kiuhalisia na kwa logic tu. Walikosea big time. Na ndio wametuletea taharuki zaidi. Huhitaji kuwa geologist au mining engineer au metallurgist kuliona hilo.
Kifupi, hakuna mgodi hapa Tanzania unaoweza kuzalisha ounce 250,000 kwa mwezi. Hata kwa mwaka haiwezekani.
 
Yale mazuzu yana laana mkuu angalia TULAWAKA ilipewa STAMICO juzi wametangaza kufunga Mgodi wakiwa na deni la zaidi ya bil 56!!

Aisee. Hii ni kweli? Kama ni kweli inabidi wananchi tuungane tusimamishe shughuli zote mpaka haya mazuzu yatoke madarakani. Hovyo sana. Yaani wenzao wameacha mgodi baada ya kuona haulipi. Wao ndio kwanza wanakwenda kuanza kujifanya wanachimba kwa hela za mkopo? Shenzi kabisa. Watu hawa wanapaswa kupigwa mawe hadharani wafie mbali. Tufike mahali kama wananchi tuanze kuwatambua hao wafanya maamuzi na kuwafuata majumbani kwao, kuwatenga makanisani na misikitini, mashuleni, na sokoni. Kila mahali. Make life miserable for them.
 
Nia njema inayokiuka mikataba tukiosaini wenyewe,hiyo mwanasheria gani atasapoti ujinga huo,tumevunja sheria kwa kukata michanga ya watu
 
Namwelewaga Sana huyu Jamaa anayeitwa Tundu Antipas Lissu. Msomeni hapa wenyewe

"ANAANDIKA TUNDU LISU...

....Suala sio nia njema ya Rais. Suala ni consequences za hiyo nia njema. The road to hell is paved with good intentions.

Mugabe most likely alikuwa na nia njema. The consequences za nia njema hiyo ni kwamba Zimbabwe ya leo haina hata sarafu yake na imegeuka kuwa ya kuomba chakula wakati ilikuwa a major food exporter.

Kama kweli Rais Magufuli ana nia njema angeanza na mfumo mzima wa kisheria, sio kuhangaika na magwangala.

100% ya uzalishaji wa dhahabu ya Geita unafanyikia mgodini na Geita Gold Mine ni mgodi mkubwa kuliko yote nchini.

Kwa logic ya Magufuli ni kwamba GGM hawatuiibii kwa sababu tu smelting yote inafanyikia Geita.

Acacia wanayeyushia dhahabu yote ya Nyamongo mgodini Nyamongo.

Kwa logic hiyo hiyo, hawa wezi wa mchanga wa Bulyanhulu na Buzwagi hawaibi Nyamongo kwa sababu tu wanafanya kila kitu Nyamongo.

Resolute walisafisha 100% ya dhahabu yao Nzega mpaka walipokomba kila kitu na kuacha mashimo na maji ya sumu tu.

Kwa logic ya wazalendo wetu, hatukuibiwa Nzega kwa sababu wawekezaji hao hawakusafirisha mchanga wa dhahabu.

Acacia walishakomba kila kitu Tulawaka na kuacha mashimo na maji ya sumu. Kwa sababu tu hawakusafirisha mchanga, basi hawakuwa wezi.

Hii ni logic ya mtu asiyeelewa biashara ya uchimbaji dhahabu katika nchi hii kabisa.

Tangu tumeanza kuwakaribisha wawekezaji hawa, hatujawahi kufikisha 10% ya mapato ya kikodi kutokana na mauzo ya dhahabu yote iliyochimbwa na kuuzwa nje.

Sio kwa sababu wawekezaji walikuwa wana-underdeclare mchanga wa dhahabu, bali ni kwa sababu sheria zetu zinawaruhusu kutokulipa kodi kama hawajatangaza faida.

Ni sheria, sheria, sheria. Sio mchanga wa dhahabu. Hilo ni changa la macho tu la kufumbia wasioelewa.

Kama Magufuli ana nia njema angeanza na sheria. Hajaanza na sheria, hana nia njema.

Mnaambiwa tusiogope kushtakiwa. Munatiwa ujinga na hao hao waliowaruhusu wageni kuchota mali zetu: akina Magufuli na CCM yao.

Tumeshalipishwa na tunaendelea kulipishwa mabilioni mengi kutokana na kesi za Richmond/Dowans, IPTL/Tegeta Escrow, City Water, Samaki wa Magufuli, n.k. kwa sababu tumekuwa tunakiuka mikataba 'kwa nia njema.'

Tumekuwa tunaingia hasara kubwa kama taifa kwa sababu za kijinga. Badala ya kukataa ujinga huu tunaushabikia kwa sababu tu umefanywa 'kwa nia njema.'

Magufuli atauachia huo mchanga wa dhahabu kwa wenyewe. Mark my words.

Hana jinsi.

Sheria yetu ya madini inasema huo mchanga ni mali yao. Na imesema hivyo tangu mwaka '98.

Mkataba wao unasema ni mali yao. Na umesema hivyo tangu mwaka 2000.

Mikataba ya kimataifa tuliyosainishwa na wenye nia njema hawa inasema mchanga ni mali ya Acacia.

Mchanga huo umehakikiwa na TRA, TMAA, GST na SGS. Zote hizi ni taasisi za Serikali hii hii na zimepewa mamlaka kisheria na kimkataba na Serikali hii hii kuhakiki mchanga huo.

Kamati ya Prof. Mruma haina mamlaka hayo. Ripoti yake haina maana yoyote kiushahidi.

Sio kupiga ramli au kuagua kusema kwamba tutapigwa asubuhi kwenye arbitral tribunals za kimataifa.

Tutawarudishia mchanga na tutawalipa hasara yote waliyopata kwa sababu ya matendo yenye nia njema lakini yasiyozingatia sheria wala busara katika mambo haya.

Tunarushiwa changa la macho lingine. Tunaambiwa kuna Kamati ya wachumi na wanasheria inaleta ripoti nyingine. Hii itakuwa Kamati ya nne tangu mwaka 2004. Tulikuwa na Kamati ya Dr. Jonas Kipokola (2004); Lau Masha (2006) na Jaji Mark Bomani (2008). Tumekuwa na taarifa lukuki za watafiti binafsi na kwa muda mrefu. Ni kitu gani hasa cha kiuchumi au kisheria ambacho hatukijui hadi sasa na ambacho kinahitaji kuundiwa Kamati nyingine??? Wajinga ndio waliwao. Mimi sio mjinga. Na sijahongwa kama hawa wanajiita wazalendo. Ninapinga na nitaendelea kupinga ujinga huu unaotupeleka kuzimu......".

Tundu Lisu
wenye akili hawapewi kuongoza nchi mamburura ndio yanayopewa kuongoza nchi,hasara hii
 
Namwelewaga Sana huyu Jamaa anayeitwa Tundu Antipas Lissu. Msomeni hapa wenyewe

"ANAANDIKA TUNDU LISU...
emoji116.png


....Suala sio nia njema ya Rais. Suala ni consequences za hiyo nia njema. The road to hell is paved with good intentions.

Mugabe most likely alikuwa na nia njema. The consequences za nia njema hiyo ni kwamba Zimbabwe ya leo haina hata sarafu yake na imegeuka kuwa ya kuomba chakula wakati ilikuwa a major food exporter.

Kama kweli Rais Magufuli ana nia njema angeanza na mfumo mzima wa kisheria, sio kuhangaika na magwangala.

100% ya uzalishaji wa dhahabu ya Geita unafanyikia mgodini na Geita Gold Mine ni mgodi mkubwa kuliko yote nchini.

Kwa logic ya Magufuli ni kwamba GGM hawatuiibii kwa sababu tu smelting yote inafanyikia Geita.

Acacia wanayeyushia dhahabu yote ya Nyamongo mgodini Nyamongo.

Kwa logic hiyo hiyo, hawa wezi wa mchanga wa Bulyanhulu na Buzwagi hawaibi Nyamongo kwa sababu tu wanafanya kila kitu Nyamongo.

Nadhani kuna mahali hoja ya Lissu ilikuwa haijaeleweka na bado haijaeleweka.
Kwa maana zimwi hili hatuwezi kulishinda bila kushikilia mpini kwa maana ya review ya Mkataba ambao ndiyo hawa mabwana wanautumia kufanikisha uwizi.
Ila kwa Raisi kukubali mapendekezo ya Kamati ya kufanyia marekebisho sheria ni hatua moja kuelekea ushindi wa kadhia hii.
 
Back
Top Bottom