Lissu; Nia njema ya Magufuli inatupeleka pabaya

BAKOI

JF-Expert Member
Jan 31, 2016
1,213
2,325
Namwelewaga Sana huyu Jamaa anayeitwa Tundu Antipas Lissu. Msomeni hapa wenyewe

"ANAANDIKA TUNDU LISU...

....Suala sio nia njema ya Rais. Suala ni consequences za hiyo nia njema. The road to hell is paved with good intentions.

Mugabe most likely alikuwa na nia njema. The consequences za nia njema hiyo ni kwamba Zimbabwe ya leo haina hata sarafu yake na imegeuka kuwa ya kuomba chakula wakati ilikuwa a major food exporter.

Kama kweli Rais Magufuli ana nia njema angeanza na mfumo mzima wa kisheria, sio kuhangaika na magwangala.

100% ya uzalishaji wa dhahabu ya Geita unafanyikia mgodini na Geita Gold Mine ni mgodi mkubwa kuliko yote nchini.

Kwa logic ya Magufuli ni kwamba GGM hawatuiibii kwa sababu tu smelting yote inafanyikia Geita.

Acacia wanayeyushia dhahabu yote ya Nyamongo mgodini Nyamongo.

Kwa logic hiyo hiyo, hawa wezi wa mchanga wa Bulyanhulu na Buzwagi hawaibi Nyamongo kwa sababu tu wanafanya kila kitu Nyamongo.

Resolute walisafisha 100% ya dhahabu yao Nzega mpaka walipokomba kila kitu na kuacha mashimo na maji ya sumu tu.

Kwa logic ya wazalendo wetu, hatukuibiwa Nzega kwa sababu wawekezaji hao hawakusafirisha mchanga wa dhahabu.

Acacia walishakomba kila kitu Tulawaka na kuacha mashimo na maji ya sumu. Kwa sababu tu hawakusafirisha mchanga, basi hawakuwa wezi.

Hii ni logic ya mtu asiyeelewa biashara ya uchimbaji dhahabu katika nchi hii kabisa.

Tangu tumeanza kuwakaribisha wawekezaji hawa, hatujawahi kufikisha 10% ya mapato ya kikodi kutokana na mauzo ya dhahabu yote iliyochimbwa na kuuzwa nje.

Sio kwa sababu wawekezaji walikuwa wana-underdeclare mchanga wa dhahabu, bali ni kwa sababu sheria zetu zinawaruhusu kutokulipa kodi kama hawajatangaza faida.

Ni sheria, sheria, sheria. Sio mchanga wa dhahabu. Hilo ni changa la macho tu la kufumbia wasioelewa.

Kama Magufuli ana nia njema angeanza na sheria. Hajaanza na sheria, hana nia njema.

Mnaambiwa tusiogope kushtakiwa. Munatiwa ujinga na hao hao waliowaruhusu wageni kuchota mali zetu: akina Magufuli na CCM yao.

Tumeshalipishwa na tunaendelea kulipishwa mabilioni mengi kutokana na kesi za Richmond/Dowans, IPTL/Tegeta Escrow, City Water, Samaki wa Magufuli, n.k. kwa sababu tumekuwa tunakiuka mikataba 'kwa nia njema.'

Tumekuwa tunaingia hasara kubwa kama taifa kwa sababu za kijinga. Badala ya kukataa ujinga huu tunaushabikia kwa sababu tu umefanywa 'kwa nia njema.'

Magufuli atauachia huo mchanga wa dhahabu kwa wenyewe. Mark my words.

Hana jinsi.

Sheria yetu ya madini inasema huo mchanga ni mali yao. Na imesema hivyo tangu mwaka '98.

Mkataba wao unasema ni mali yao. Na umesema hivyo tangu mwaka 2000.

Mikataba ya kimataifa tuliyosainishwa na wenye nia njema hawa inasema mchanga ni mali ya Acacia.

Mchanga huo umehakikiwa na TRA, TMAA, GST na SGS. Zote hizi ni taasisi za Serikali hii hii na zimepewa mamlaka kisheria na kimkataba na Serikali hii hii kuhakiki mchanga huo.

Kamati ya Prof. Mruma haina mamlaka hayo. Ripoti yake haina maana yoyote kiushahidi.

Sio kupiga ramli au kuagua kusema kwamba tutapigwa asubuhi kwenye arbitral tribunals za kimataifa.

Tutawarudishia mchanga na tutawalipa hasara yote waliyopata kwa sababu ya matendo yenye nia njema lakini yasiyozingatia sheria wala busara katika mambo haya.

Tunarushiwa changa la macho lingine. Tunaambiwa kuna Kamati ya wachumi na wanasheria inaleta ripoti nyingine. Hii itakuwa Kamati ya nne tangu mwaka 2004. Tulikuwa na Kamati ya Dr. Jonas Kipokola (2004); Lau Masha (2006) na Jaji Mark Bomani (2008). Tumekuwa na taarifa lukuki za watafiti binafsi na kwa muda mrefu. Ni kitu gani hasa cha kiuchumi au kisheria ambacho hatukijui hadi sasa na ambacho kinahitaji kuundiwa Kamati nyingine??? Wajinga ndio waliwao. Mimi sio mjinga. Na sijahongwa kama hawa wanajiita wazalendo. Ninapinga na nitaendelea kupinga ujinga huu unaotupeleka kuzimu......".

Tundu Lisu
 
Tumeshalipishwa na tunaendelea kulipishwa mabilioni mengi kutokana na kesi za Richmond/Dowans, IPTL/Tegeta Escrow, City Water, Samaki wa Magufuli, n.k. kwa sababu tumekuwa tunakiuka mikataba 'kwa nia njema wahusika wanashauriwa wanapuuzia .Mwanasheria Msomi Mhe.
Tundu Lissu anampa msaada mkubwa wa kisheria Raisi yetu ndo hivyo huwa wanadharau ushauri ambayo hutolewa na upinzani baadaye tunakuja kulipa gharama sisi za wananchi kwa maamuzi ya mtu mmoja !
 
Anajitahidi sana kupigania maslahi ya nchi yetu lakini mafisadi, wezi, watoa/wapokea rushwa wamekusudia kupotosha kile anachokipigania kwa manufaa ya Tanzania na Watanzania.
That's y siachi kumuombea maisha marefu. Japokuwa vizuri havidumu,lakini Mungu ajaribu kutusamehe na atuwachie mtu huyu kwa muda mrefu. Kwa Maana Naona kama tuna adhibiwa,kwanini Mungu anaruhusu mabaradhuli Haya kila siku yatuonee na kututesa? Basi atuwachie mtetezi huyu aliyetuletea.
Live long Tundu Lissu na wapigania haki wote,akiwemo BAK wangu. Maisha marefu kwako kaka angu.
 
Ahsante sana Maserati Mwenyezi Mungu atupe wote afya njema na maisha marefu. Huyu na Lema Serikali imewaonea sana kwa kuwatia rumande bila kuwa na hatia yoyote ile.

Kuna siku alikuwa anatoka rumande alipowaona viongozi wenzake wa Chadema, ndugu, jamaa na marafiki akaanza kulia. Nilisikia uchungu mkubwa sana kumuona mtu mzima ananyanyaswa kiasi kile hata kufikia kulia kama mtoto.

Zama hizi kupigania maslahi ya nchi yetu inataka moyo sana. Mwezi wa nane huu hatujui alipo Ben Saanane na kama yuko hao au kishauwawa. Yericko naye ndiyo wameshambeba jana usiku wa manane. Kumbuka pia yaliyompata Roma Mkatoliki na jamaa zake kisa wimbo tu!

Shukrani sana Maserati

That's y siachi kumuombea maisha marefu. Japokuwa vizuri havidumu,lakini Mungu ajaribu kutusehe na atuwachie mtu huyu kwa muda mrefu. Kwa Maana Naona kama tuna adhibiwa,kwanini Mungu anaruhusu mabaradhuli Haya kila siku yatuonee na kututesa? Basi atuwachie mtetezi huyu aliyetuletea.
Live long Tundu Lissu na wapigania haki wote,akiwemo BAK wangu. Maisha marefu kwako kaka angu.
 
80 Reactions
Reply
Back
Top Bottom