Lissu; Nia njema ya Magufuli inatupeleka pabaya

Sometimes when an intelligent man speaks,it is not alyways easy for everybody to understand the message behind untill the intelligent people discuss the message behind.Then from that discussion, the unintelligent ones can have a chance to understand.
Mkuu msg yako ungekuwa umeandika kwa kiswahili likes zingekuua, lakini kwa vile wengi wanaipita bila kuisoma ndiyo hivyo tena.
 
Msome tena anasema tunaibiwa kwasababu ya makubaliano yetu wenyewe na hatuibiwi zaidi kwenye mchanga bali kwenye dhahabu yenyewe. Pia sio uchawi wala uganga kwamba ukivunja makubaliano utalipa na tumeshalipa sana kesi ya Richmond n.k . ANASEMA Tume hizi kwenye suala hili sio za kwanza hivyo kujifanya ndio zinleta majibu leo yanayofanana na majibu yatume zilizopita na kuibuka kama wajinga kuvunja makubaliano sio Akili. Anasema njia sahihi ni kutibu ugonjwa aka mikataba mibovu inayonuka sio kurukia makapi aka mchanga. Sijui hii itakufanya umuelewe Wakili?
 
Mh. Rais hili andiko nilmsaada sana kwako najua kama rais inaweza ikakuwia vigumu kuukubali ukweli,fanya kama vile we mwanafunzi isome itakuingia tu Mkuu wetu
 
Tangu tumeanza kuwakaribisha wawekezaji hawa, hatujawahi kufikisha 10% ya mapato ya kikodi kutokana na mauzo ya dhahabu yote iliyochimbwa na kuuzwa nje. Sio kwa sababu wawekezaji walikuwa wana-underdeclare mchanga wa dhahabu, bali ni kwa sababu sheria zetu zinawaruhusu kutokulipa kodi kama hawajatangaza faida.
Ni sheria, sheria, sheria. Sio mchanga wa dhahabu. Hilo ni changa la macho tu la kufumbia wasioelewa.
Kama Magufuli ana nia njema angeanza na sheria.

Nadhani kuna pendekezo hapo
Sijui mtu aseme vipi ndiyo aeleweke
Keshesema mara elfu moja kidogo. Tubadili sheria na tujitoe hiyo mifungamano ya kimataifa inayotubana.
Sasa kama sio Ufumbuzi au mawazo mbadala ni nini?
 
Tundu Lissu anaongea ukweli mtupu, lakini ni " Misplaced truth", Sisi Wananchi tunataka tuone Serikali na Wapinzani wanaongea kwa sauti moja katika hili, Tunataka huku nje watume meseji ya kuikataa mikataba ya Kilaghai, lakini ndani kwenye vikao vya kutafuta muafaka waelezane huo " Ukweli wa Lissu".
Ni mfano wa vita, haiwezekani majeshi yetu yameshafika Mutukula, Amiri jeshi Mkuu anatoa Amri yasonge mbele yakamng'oe Nduli Kampala, halafu wanasheria na Wasomi wanaanza kupaza sauti ya " Ni kinyume cha International Law", " Sijui ni kinyume cha OAU" , Japo kisheria wanaweza kuwa Sahihi lakini " Kimkakati hawako sahihi".

Lissu alishakiri tunaibiwa!
Lissu alishakiri mikataba ni mibovu.
Lakini Lissu hajaweka appointment na Raisi kumueleza one to one what is the way forward.
Lissu hasemi tunafanyaje sasa!
Lissu anazungumzia historia ya tatizo lakini hatoi solution ya Tatizo!, hapo ndo sisi wengine hatumuelewi kabisa!
 
Sijui mtu aseme vipi ndiyo aeleweke
Keshesema mara elfu moja kidogo. Tubadili sheria na tujitoe hiyo mifungamano ya kimataifa inayotubana.
Sasa kama sio Ufumbuzi au mawazo mbadala ni nini?

Sheria haiact kwenda nyuma, ukiitunga leo, haizuii dili zilizowekwa mikataba zamani kuendelea.

Je huyo Lissu keshakwambia athari za kujitoa katika mafungamano ya Kimataifa juu ya uwekezaji?, Wawekezaji hawaji!!. Approach ya Lissu haiwork!

Kitakachowork ni kuipiga mashimo mikataba ya zamani kwa kuprove kuwa hakukuwa na good faith kwa upande wa mwekezaji na hivyo kukaa mezani kurenogiate better deal!. Lakini hili haliwezi kufanyika mpaka uje na ushahidi kwenye meza ya mazungumzo kuwa data mlizokuwa mnatumia kumbe siyo sahihi!
 
Tundu Lissu anaongea ukweli mtupu, lakini ni " Misplaced truth", Sisi Wananchi tunataka tuone Serikali na Wapinzani wanaongea kwa sauti moja katika hili, Tunataka huku nje watume meseji ya kuikataa mikataba ya Kilaghai, lakini ndani kwenye vikao vya kutafuta muafaka waelezane huo " Ukweli wa Lissu".
Ni mfano wa vita, haiwezekani majeshi yetu yameshafika Mutukula, Amiri jeshi Mkuu anatoa Amri yasonge mbele yakamng'oe Nduli Kampala, halafu wanasheria na Wasomi wanaanza kupaza sauti ya " Ni kinyume cha International Law", " Sijui ni kinyume cha OAU" , Japo kisheria wanaweza kuwa Sahihi lakini " Kimkakati hawako sahihi".

Lissu alishakiri tunaibiwa!
Lissu alishakiri mikataba ni mibovu.
Lakini Lissu hajaweka appointment na Raisi kumueleza one to one what is the way forward.
Lissu hasemi tunafanyaje sasa!
Lissu anazungumzia historia ya tatizo lakini hatoi solution ya Tatizo!, hapo ndo sisi wengine hatumuelewi kabisa!



mkuu kaa usome tena walau mara tatu akichoandikaTL,nazungumzia comments yako ya mwisho,bashite mkubwa wewe
 
Hivi TUNAOGOPA NINI KUANZA NA SHERIA,au kubadili sheria,au kupindisha makusudi ni sehemu nyingine ya kipigo cha CCM kwa watanzania?
Au CCM inakula ganji kwenye haya malipo?mbona hawataki ushauri kutoka kwa watu competent kwenye sheria?
Wakiharibu kitu wanasema DENI LETU TANZANIA,wakipatia wanasema SERIKALI YA CCM na wala si ya Tanzania.
Aaaaaahhhh watuache bana,chama kimechoka kinatoa moshi tu.
 
Naona Lisu analialia tu lakini hatoi mapendekezo mahsusi ya nini kifanywe.

Mimi ningekuwa ndo Magufuli ningemwomba huyo Lisu atoe mapendekezo halafu niyafuate hayo mapendekezo yake tuone tutakapofika.

Maana kupiga mayowe kama mwendawazimu na kusubiri wenzio watende na wewe ndiyo ujitokeze uanze kuwakosoa ni kazi rahisi sana.
Mapendekezo gani tena makontena yapo withheld ndio anachosema sheria mkononi
 
Tatizo la nchi limeshakuwa kubwa,sasa kwa sababu tu ya chakula cha siku moja,hata SHERIA haziangaliwi tena eti kwa sababi ya n8a njema.
 
Kwa hiyo unaamini kila upuuzi unaofanyika CDM ? Usilinganishe CCM na hiyo saccoss yenu ya mtaa wa ufipa. CCM ni habari nyingine
Endelea kuwaza hivyo hivyo ungejua nnavyotamani lowassa na Sumaye wahusishw moja kwa moja na hii mikataba ya hovyohovyo waliyosaini wakati wapo madarakani sidhani kama ungeniita CDM moja kwa moja.

This a matter of National bro kama wewe umeshikwa akili na CCM usifikirie wote tupo hivyo wengine tunasimama kwa ajili ya Taifa.

Sidhani kama utapingana na mimi kwamba yote haya kiini ni hicho chama chenu ambacho kimetumikiwa na huyo mnayemuona leo ni kaka Malaika kashushwa msitambue kama na yeye alihusika kupiga makofi kupitisha hiyo mikataba.
 
Pia anasema hata hiyo kamati iliyoundwa,hakuna kipengele cha kimkataba kinachohalalisha uundwaji wake! Hata walichoandika mahakamani hakitapokelewa kama ushahidi,vitabu vyao vimejaa magwangala (maandishi)tu yasiyo na thamani kimahakama

Mkataba umeonyesha jinsi ya kushughulikia mgogoro baina ya pande mbili endapo utajitokeza,sisi hatujafata utaratibu,na juu ya yote,kutofata kwetu utaratibu kumewatia hasara ya matrilioni, Acacia wanaweza kwenda mahakamani na hoja moja tu,utaratibu haukufatwa,na wakaomba walipwe fidia!

Mkataba haukusainiwa jukwaani,huwezi kuuzuia jukwaani

Kimahakama hii ni kesi fupi,na itatugharimu,na Mimi naomba iishe kabla ya 2020
Lakini hawa hawa wakina Lisu huwa wanatuambia hawajawahi ona hiyo mikataba hata wewe najua hujawahi ona hiyo mikataba sasa hivyo vifungu vya mikataba umeviona wapi?Kuhusu 2020 unadhani itasaidia kitu?Magu tabia yake sio kama unavyofikiri wewe huwa hafanyi kitu anatarajia kupigiwa kura nenda waulize wana chato watakueleza vizuri jinsi alivyokuwa anawapa makavu na bado wanamchagua,lakini tubaki kwenye hoja hivi kuvunja hiyo mikataba au kubadilisha hizo sheria hakutawaogopesha hao wawekezaji anaowapigia kelele kuwatetea pale bungeni
 
ANAANDIKA TUNDU LISU...

Suala sio nia njema ya Rais. Suala ni consequences za hiyo nia njema. The road to hell is paved with good intentions.

Mugabe most likely alikuwa na nia njema. The consequences za nia njema hiyo ni kwamba Zimbabwe ya leo haina hata sarafu yake na imegeuka kuwa ya kuomba chakula wakati ilikuwa a major food exporter.

Kama kweli Rais Magufuli ana nia njema angeanza na mfumo mzima wa kisheria, sio kuhangaika na magwangala.

100% ya uzalishaji wa dhahabu ya Geita unafanyikia mgodini na Geita Gold Mine ni mgodi mkubwa kuliko yote nchini.

Kwa logic ya Magufuli ni kwamba GGM hawatuiibii kwa sababu tu smelting yote inafanyikia Geita.

Acacia wanayeyushia dhahabu yote ya Nyamongo mgodini Nyamongo.

Kwa logic hiyo hiyo, hawa wezi wa mchanga wa Bulyanhulu na Buzwagi hawaibi Nyamongo kwa sababu tu wanafanya kila kitu Nyamongo.

Resolute walisafisha 100% ya dhahabu yao Nzega mpaka walipokomba kila kitu na kuacha mashimo na maji ya sumu tu.

Kwa logic ya wazalendo wetu, hatukuibiwa Nzega kwa sababu wawekezaji hao hawakusafirisha mchanga wa dhahabu.

Acacia walishakomba kila kitu Tulawaka na kuacha mashimo na maji ya sumu. Kwa sababu tu hawakusafirisha mchanga, basi hawakuwa wezi.

Hii ni logic ya mtu asiyeelewa biashara ya uchimbaji dhahabu katika nchi hii kabisa.

Tangu tumeanza kuwakaribisha wawekezaji hawa, hatujawahi kufikisha 10% ya mapato ya kikodi kutokana na mauzo ya dhahabu yote iliyochimbwa na kuuzwa nje.

Sio kwa sababu wawekezaji walikuwa wana-underdeclare mchanga wa dhahabu, bali ni kwa sababu sheria zetu zinawaruhusu kutokulipa kodi kama hawajatangaza faida.

Ni sheria, sheria, sheria. Sio mchanga wa dhahabu. Hilo ni changa la macho tu la kufumbia wasioelewa.

Kama Magufuli ana nia njema angeanza na sheria. Hajaanza na sheria, hana nia njema.

Mnaambiwa tusiogope kushtakiwa. ******* ujinga na hao hao waliowaruhusu wageni kuchota mali zetu: akina Magufuli na CCM yao.

Tumeshalipishwa na tunaendelea kulipishwa mabilioni mengi kutokana na kesi za Richmond/Dowans, IPTL/Tegeta Escrow, City Water, Samaki wa Magufuli, n.k. kwa sababu tumekuwa tunakiuka mikataba 'kwa nia njema.'

Tumekuwa tunaingia hasara kubwa kama taifa kwa sababu za kijinga. Badala ya kukataa ujinga huu tunaushabikia kwa sababu tu umefanywa 'kwa nia njema.'

Magufuli atauachia huo mchanga wa dhahabu kwa wenyewe. Mark my words.

Hana jinsi.

Sheria yetu ya madini inasema huo mchanga ni mali yao. Na imesema hivyo tangu mwaka '98.

Mkataba wao unasema ni mali yao. Na umesema hivyo tangu mwaka 2000.

Mikataba ya kimataifa tuliyosainishwa na wenye nia njema hawa inasema mchanga ni mali ya Acacia.

Mchanga huo umehakikiwa na TRA, TMAA, GST na SGS. Zote hizi ni taasisi za Serikali hii hii na zimepewa mamlaka kisheria na kimkataba na Serikali hii hii kuhakiki mchanga huo.

Kamati ya Prof. Mruma haina mamlaka hayo. Ripoti yake haina maana yoyote kiushahidi.

Sio kupiga ramli au kuagua kusema kwamba tutapigwa asubuhi kwenye arbitral tribunals za kimataifa.

Tutawarudishia mchanga na tutawalipa hasara yote waliyopata kwa sababu ya matendo yenye nia njema lakini yasiyozingatia sheria wala busara katika mambo haya.

Tunarushiwa changa la macho lingine. Tunaambiwa kuna Kamati ya wachumi na wanasheria inaleta ripoti nyingine. Hii itakuwa Kamati ya nne tangu mwaka 2004. Tulikuwa na Kamati ya Dr. Jonas Kipokola (2004); Lau Masha (2006) na Jaji Mark Bomani (2008). Tumekuwa na taarifa lukuki za watafiti binafsi na kwa muda mrefu. Ni kitu gani hasa cha kiuchumi au kisheria ambacho hatukijui hadi sasa na ambacho kinahitaji kuundiwa Kamati nyingine??? Wajinga ndio waliwao. Mimi sio mjinga. Na sijahongwa kama hawa wanajiita wazalendo. Ninapinga na nitaendelea kupinga ujinga huu unaotupeleka kuzimu.....

Tundu Lisu
Huyu Mwanasheria uchwara anazidi kubore.
 
Halafu ni upuzi wa hili jamaa kufananisha Tanzania na Zimbabwe. Mugabe ni life president tokea mwaka 1982.

Na anachofanya Mugabe ni sawa. Nchi yake inapata shida kwa sababu mijitu kama huyu Lissu iko mingi inayomchimba ashindwe ili ichukue madaraka.
Mugabe ametengwa na wazungu kama North Korea. North Korea inapigwa tafu na China. Mugabe hana wa kumpa tafu. Mijitu kama Lissu inaona Mugabe ni
ubao wa kufundushia political failure.

Mugabe yuko right na anahitaji kuungwa mkono na nchi nyingine za kiafrika. It doesn't make sense nchi kupata uhuru ardhi iendelee kuwa mali ya wazungu.


Anachofanya Mugabe ni sawa na alichofanya Nyerere. Ila Nyerere alipoona kazidiwa kubanwa na wazungu aliamua kuachia ngazi. "He who fights and run away, lives to fight another day" - Bob Marley".
 
Back
Top Bottom