Lissu; Nia njema ya Magufuli inatupeleka pabaya

Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
10,554
2,000
Sasa hivi umekuwa Nyani hasa!! Mbona lissu alishatoa mapendekezo yaliyojaa akili na mbinu? Hukumsikia akimshauri uncle wako ajichomoe kwenye hizo platfoms zinazohalalisha Wao kutuibia sisi kisheria!! Tena sheria tuliyoisaini wenyewe?
 

Wateule

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
390
500
Duh! Leo Lissu kakubali Magufuli ana nia njema!!?

Ndio, lakini kama umemuelewa vizuri, maana yake ni kwamba "nia njema" haihalalishi unafiki. Huu ni unafiki mwingine unaofanywa na Magufuli na kundi lake la CCM. Hii mikataba ya madini na sheria zake wameingia wao na kutunga wao CCM. Kwahiyo, wanajua kinachoendelea. Sasa anachosema Lissu ni kwamba tuanze kurekebisha kwanza sheria hizi na mikataba hii ili kujiweka sehemu salama kisheria na kimikataba. Lakini, anachofanya Magu ni kujitafutia umaarufu rahisi (cheap political fame) kama anavyotafuta kwenye mambo mengine mbalimbali mbele za wananchi, kitu ambacho kitatugharimu sana huko mbele ya safari.
 

smallvile

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
493
250
Wasiellewa wakija utasikia wanataja vyama HIVI KUNA CHAMA KWENYE MAMBO YA MSINGI NA KIUCHUMI YANAYOHUSU SERIKALI YETU
WAJINGA
 

Zeni2017

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
1,247
2,000
Well done Magufuli hapa kazi tu. Hayo madebe matupu hayaachi kupiga kelele. Nani kasema rais hawezi kuvunja mkataba. Trump anafumua mikataba yote ya biashara ya Obama na maraisi waliopita.
Hoja yake ni sawa na ya Magufuli. Mikataba isiyo na maslahi kwa nchi.
 

ikipendaroho

JF-Expert Member
Jul 26, 2015
3,678
2,000
Naona Tundu Lisssu ametumia Lugha ya kidemokrasia zaidi katika Maelezo yake, lakini kwa kumlaumu Mheshimiwa Rais Magufuli ni mmoja wa wahusika wa mikataba hiyo sio kweli kwani Rais Magufuli hakuwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini. Rais Magufuli kabla kuwa Rais wa JMT alishawahi kutamka kuwa mikataba hii ya madini ni mibovu.
Acacia waliwahi kushitakiwa mahakamani na TRA kwa kutoa taarifa za uongo kwenye mapato wanayoyapata kutoka kwenye migodi wanayomiliki na mahakama ilihukumu Acacia wailiipe TRA. Sasa linapokuja suala la mikataba unayodai imevunjwa na Rais Magufuli si kweli, hapa ni Acacia akishirikiana na Watanzania wachache wasio waaminifu kujaribu kuiibia serikali ya Tanzania kwa kutoa taarifa ya uongo kwa kiasi cha madini kilichopo kwenye mchanga kusafirishwa, rekodi hii inaonyesha kampuni ya Acacia sio kampuni ya kuaminiwa. Mheshimiwa Tundu Lissu kama kweli ni mzalendo unatakiwa uiunge mkono serikali kwa hili badala ya kuiponda.
Maneno yale alikuwa ayaseme bungeni kuweka rekodi sawa. Hata Riz1 aliwahi kusema anamiliki toyota corolla 1 tu
 

charndams

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
437
225
Naona Lisu analialia tu lakini hatoi mapendekezo mahsusi ya nini kifanywe.

Mimi ningekuwa ndo Magufuli ningemwomba huyo Lisu atoe mapendekezo halafu niyafuate hayo mapendekezo yake tuone tutakapofika.

Maana kupiga mayowe kama mwendawazimu na kusubiri wenzio watende na wewe ndiyo ujitokeze uanze kuwakosoa ni kazi rahisi sana.
nyani ngabu rudia tena kusoma, Lissu kasema magufuli angeanza kwa sheria, its such simple. you don't treat the symptoms but the root cause!
 

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
12,877
2,000
Wanaojua kusoma na kuandika ni kazi sana kuwaelimisha.....na hawa ndio wanasaini mikataba,kama hapa JF tunapata shida kuwapa elimu,huko kwenye mikataba si ndio watakuwa wanachekacheka tu?

Sasa moto wameuwasha,ngoja Acacia wawachezeshe

Lissu anasema hata ripoti ya kamati ya mchanga hahakamani haitapokelewa kama ushahidi,haikidhi vigezo vya kisheria kupokelewa kama ushahidi,mahakama itaitupilia mbali na kuikanyagakanyaga !

Kamati ya mchanga si moja kati ya Taasisi zinazotambulika kimkataba,imeibuliwa juzijuzi tu,eti TRA na uwezo wao mkubwa kabisa wasione tatizo miaka yote? TRA wanajua kipi chetu na kipi sio chetu! Wakakaa kimya!

Kumbe ripoti ya mchanga mahakamani si mali kitu,ni sawa tu na gazeti la mwaka jana,
Hiyo ripoti ya kina Mruma ni sawa na kagazeti cha uhuru cha mwaka juzi
 

mjukuum

JF-Expert Member
Dec 8, 2014
5,155
2,000
Umenifanya nicheeeeeeeeeeke lkn kumbuka bashite na Lumumba kitu kimoja
Huyo wala siyo Lumumba product, bali ni Bashite product!
Wanajitoa akili hata za kuvukia tu
Hivi TUNAOGOPA NINI KUANZA NA SHERIA,au kubadili sheria,au kupindisha makusudi ni sehemu nyingine ya kipigo cha CCM kwa watanzania?
Au CCM inakula ganji kwenye haya malipo?mbona hawataki ushauri kutoka kwa watu competent kwenye sheria?
Wakiharibu kitu wanasema DENI LETU TANZANIA,wakipatia wanasema SERIKALI YA CCM na wala si ya Tanzania.
Aaaaaahhhh watuache bana,chama kimechoka kinatoa moshi tu.
 

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
12,877
2,000
Naona Lisu analialia tu lakini hatoi mapendekezo mahsusi ya nini kifanywe.

Mimi ningekuwa ndo Magufuli ningemwomba huyo Lisu atoe mapendekezo halafu niyafuate hayo mapendekezo yake tuone tutakapofika.

Maana kupiga mayowe kama mwendawazimu na kusubiri wenzio watende na wewe ndiyo ujitokeze uanze kuwakosoa ni kazi rahisi sana.
Umelemazwa na kuosha vikongwe hata kusoma na kuelewa huwezi tena
 

mjukuum

JF-Expert Member
Dec 8, 2014
5,155
2,000
Hivi TUNAOGOPA NINI KUANZA NA SHERIA,au kubadili sheria,au kupindisha makusudi ni sehemu nyingine ya kipigo cha CCM kwa watanzania?
Au CCM inakula ganji kwenye haya malipo?mbona hawataki ushauri kutoka kwa watu competent kwenye sheria?
Wakiharibu kitu wanasema DENI LETU TANZANIA,wakipatia wanasema SERIKALI YA CCM na wala si ya Tanzania.
Aaaaaahhhh watuache bana,chama kimechoka kinatoa moshi tu.
Mungu aliwafanya wachache wenye akili ili wawashauri kama viongozi

Pombe na team werk yake hawezi kushaurika watapotea hakika
 

mjukuum

JF-Expert Member
Dec 8, 2014
5,155
2,000
Endelea kuwaza hivyo hivyo ungejua nnavyotamani lowassa na Sumaye wahusishw moja kwa moja na hii mikataba ya hovyohovyo waliyosaini wakati wapo madarakani sidhani kama ungeniita CDM moja kwa moja.

This a matter of National bro kama wewe umeshikwa akili na CCM usifikirie wote tupo hivyo wengine tunasimama kwa ajili ya Taifa.

Sidhani kama utapingana na mimi kwamba yote haya kiini ni hicho chama chenu ambacho kimetumikiwa na huyo mnayemuona leo ni kaka Malaika kashushwa msitambue kama na yeye alihusika kupiga makofi kupitisha hiyo mikataba.
Kwenye nchi zenye maana ya demokrasia ile isue ya kuuza nyumba za serikali ingetosha kumtambua akili na ufahamu wake kuwa hafai sio kuwa waziri tu hata ubunge Wa kuteuliwa
Samaki za mchina watu wana mikataba wanafanya kutokana na kile mlichokisaini huku mkiwa mnajua kuwa hamjui kimeandikwa nn ingekuwa hoja ya pili kuwa huyu hafai
Oooooooh ccm waliishiwa mtu sahihi na huku hukijidhania hii nchi ni yao wakaona pamoja ja kukosa vigezo vyoooote hivyo lakini kuliko wampe mpinzani bora apewe asiyekuwa na sifa ila maadam anatoka ccm

Huu ni mwaka Wa ameliandalia taifa hasara kubwa mikataba waliyokuwa wanaipinga wapinzani Leo ndio inawaumiza

Kama mlivyosema wakati Wa mikataba ndio mnavyofanya kwenye mchanga mwisho mkiwa mmejua hasara ndio mtakumbuka kuwa ,,,,,,

Hakika Yesu alitambuliwa na waliomtesa baada ya kumuua
 

Nyaru

JF-Expert Member
Oct 14, 2016
289
250
Wanaojua kusoma na kuandika ni kazi sana kuwaelimisha.....na hawa ndio wanasaini mikataba,kama hapa JF tunapata shida kuwapa elimu,huko kwenye mikataba si ndio watakuwa wanachekacheka tu?

Sasa moto wameuwasha,ngoja Acacia wawachezeshe

Lissu anasema hata ripoti ya kamati ya mchanga hahakamani haitapokelewa kama ushahidi,haikidhi vigezo vya kisheria kupokelewa kama ushahidi,mahakama itaitupilia mbali na kuikanyagakanyaga !

Kamati ya mchanga si moja kati ya Taasisi zinazotambulika kimkataba,imeibuliwa juzijuzi tu,eti TRA na uwezo wao mkubwa kabisa wasione tatizo miaka yote? TRA wanajua kipi chetu na kipi sio chetu! Wakakaa kimya!

Kumbe ripoti ya mchanga mahakamani si mali kitu,ni sawa tu na gazeti la mwaka jana,
Tena gazeti lile la LUMUMBA lililopambwa na rangi za kijani.
 

mjukuum

JF-Expert Member
Dec 8, 2014
5,155
2,000
Halafu ni upuzi wa hili jamaa kufananisha Tanzania na Zimbabwe. Mugabe ni life president tokea mwaka 1982.

Na anachofanya Mugabe ni sawa. Nchi yake inapata shida kwa sababu mijitu kama huyu Lissu iko mingi inayomchimba ashindwe ili ichukue madaraka.
Mugabe ametengwa na wazungu kama North Korea. North Korea inapigwa tafu na China. Mugabe hana wa kumpa tafu. Mijitu kama Lissu inaona Mugabe ni
ubao wa kufundushia political failure.

Mugabe yuko right na anahitaji kuungwa mkono na nchi nyingine za kiafrika. It doesn't make sense nchi kupata uhuru ardhi iendelee kuwa mali ya wazungu.


Anachofanya Mugabe ni sawa na alichofanya Nyerere. Ila Nyerere alipoona kazidiwa kubanwa na wazungu aliamua kuachia ngazi. "He who fights and run away, lives to fight another day" - Bob Marley".
Kama hutajali punguza mhemuko soma ulichoandika mkuu nina uhakika utaedit

Kama yuko sahihi mwambie pombe afanye kama yeye basi

Makosa kaumbiwa binadamu dogo kuwa na uelewa pombe kakosea kama alivyokosea kwenye kuuza nyumba na wale samaki

Kama hutaki labda pia mafuta ya akili yameisha kichwani mwako utajua siku moja ukinunua
 

Mdudu halisi

JF-Expert Member
May 7, 2014
2,735
2,000
Nimemwelewa sana Lissu. Anapendekeza yafanyike marekebisho ya sheria za madini kwanza na siyo kukimbilia kuzuia makontena ya mchanga pale bandarini. Eti mwekezaji hapaswi kulipa kodi mpaka atangaze faida! Hivi kweli sheria hii ilitungwa na watu wenye akili timamu? CCM ndiyo MAWAKALA wa hawa wanyonyaji. Wameshiriki kutunga sheria mbovu na kusaini mikataba ya kipuuzi, leo wanatulilia watanzania na kujifanya wao ni wazalendo.
 

mtx2006

JF-Expert Member
Feb 1, 2008
276
225
Hiyo ripoti ya kina Mruma ni sawa na kagazeti cha uhuru cha mwaka juzi
Ripoti ya Mruma ni ya rais ili kujibu swali la kiasi gani kimo kwenye mchanga baada ya vyombo vilivyopo kisheria kutotimiza wajibu wake. Tundu anakili kwamba TRA TMAA etc ndizo zipo kisheria kutoa report. Kitu anachojisahulisha ni mamlaka ya rais ya kuteua hizo taasisi. Hata leo akitaka prof mruma anaweza akawa ndio TRA au TMAA na automatically akatoa ripoti ikawa ushahidi unaokubalika.

Tundu siasa za kukaa kwenye kukosoa tu kuna mfanya sasa awe kama gwajima. Sentensi zake zina mkanganyiko kibao. Ukichukua tu anayoyasema kwa mapovu mengi kwa wiki moja tu yanapingana vibaya mno. Ukiwasikia wawekezaji wenyewe wameanza kukiri baadhi ya mambo mfano kuuza huu mchanga juu kwa juu. Je waliwahi ku declare mauzo haya au wao hata wauze bei yoyote sisi wanatueleza tu ile thamani ya kilo 3. Je wakishauza wanaonunua wakechenjua uwa wana declare dhahabu inatoka Tanzania?. Je hii hawezi kuwa sababu ya Tanzania kutokuwa one of the biggest producer?

Hatua ya Magufuli hata kama sio sahihi ni muhimu kuwajengea hofu ili hiyo mikataba ijadilike kwa faida ya nchi.
 

KMANGA

JF-Expert Member
Jan 30, 2014
674
500
Maskini Tanzania nchi ya MAPANKI, MAGWANGALA, MAKINIKIA na mengineyo. Hivi baada ya mheshimiwa kutoa amri kuwa wananchi wapewe yale MAGWANGALA, mpaka sasa wananchi na taifa kwa ujumla wamenufaika vipi.

Ni vema haya mambo yasiwe yanaachwa hewani bila ya kuyafuatilia kwa undani na wananchi kupewa mrejesho kwa kila hatua.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom