Lissu; Nia njema ya Magufuli inatupeleka pabaya

Ahsante sana Maserati Mwenyezi Mungu atupe wote afya njema na maisha marefu. Huyu na Lema Serikali imewaonea sana kwa kuwatia rumande bila kuwa na hatia yoyote ile.

Kuna siku alikuwa anatoka rumande alipowaona viongozi wenzake wa Chadema, ndugu, jamaa na marafiki akaanza kulia. Nilisikia uchungu mkubwa sana kumuona mtu mzima ananyanyaswa kiasi kile hata kufikia kulia kama mtoto.

Zama hizi kupigania maslahi ya nchi yetu inataka moyo sana. Mwezi wa nane huu hatujui alipo Ben Saanane na kama yuko hao au kishauwawa. Yericko naye ndiyo wameshambeba jana usiku wa manane. Kumbuka pia yaliyompata Roma Mkatoliki na jamaa zake kisa wimbo tu!

Shukrani sana Maserati
Nayaona mkuu,roho inaniumaga sana.
Lakini nashukuru Mungu hawaachani,wanapeana ushirikiano mwanzo mwisho. Wanabana mwisho wanaachia,that's y siachi kuwaombea maisha mrefu na ulinzi kwa Mwenyezi Mungu.
Ipo siku,yatakwisha.
Hata Mzungu hakujua kama waafrika watainua vichwa na kupinga komandi zao.
 
Kuna upumbavu na wizi mkubwa unaendelea nchini kwetu. Hawa wachukuaji wanadai wanapata hasara miaka chungu nzima sasa. Cha kushangaza pamoja na hasara zao bado wameng'ang'ana nchini tu na hawa mafisadi wa MACCM yameshapewa hongo/rushwa yanaangalia pembeni huku tukiendelea kuibiwa kwa miaka chungu nzima.

Ndio mkuu maana serikali iliununua Mgodi ikapawa Shirika la madini la taifa (STAMICO) Hivi navyoongea TULAWAKA imefungwa ati ilikua ikiendeshwa kwa hasara ilhali Barrick waliwauzia ukiwa unatoa faida!

Mikono ya CCM ina laana.
 
Kuwa mfuas wa kijani inahitaji moyo,maana akil inatakiwa unaiweka mfukon,Mungu awe nawe TL maana una wakati mgumu kutetea maslahi ya Nchi,unahatarisha maisha yako,unapata msukosuko kwa kutetea maslah ya Nchi,wachache waliojivika ngoz ya Kondoo kumbe ndan ni Mbwa mwitu wanashiriki kuingamiza Nchi yetu kwa mikataba isiyo na maslahi kwa Nchi yetu,Mungu akulinde na azid kukupa moyo wa ushupavu
 
Namwelewaga Sana huyu Jamaa anayeitwa Tundu Antipas Lissu. Msomeni hapa wenyewe

"ANAANDIKA TUNDU LISU...

....Suala sio nia njema ya Rais. Suala ni consequences za hiyo nia njema. The road to hell is paved with good intentions.

Mugabe most likely alikuwa na nia njema. The consequences za nia njema hiyo ni kwamba Zimbabwe ya leo haina hata sarafu yake na imegeuka kuwa ya kuomba chakula wakati ilikuwa a major food exporter.

Kama kweli Rais Magufuli ana nia njema angeanza na mfumo mzima wa kisheria, sio kuhangaika na magwangala.

100% ya uzalishaji wa dhahabu ya Geita unafanyikia mgodini na Geita Gold Mine ni mgodi mkubwa kuliko yote nchini.

Kwa logic ya Magufuli ni kwamba GGM hawatuiibii kwa sababu tu smelting yote inafanyikia Geita.

Acacia wanayeyushia dhahabu yote ya Nyamongo mgodini Nyamongo.

Kwa logic hiyo hiyo, hawa wezi wa mchanga wa Bulyanhulu na Buzwagi hawaibi Nyamongo kwa sababu tu wanafanya kila kitu Nyamongo.

Resolute walisafisha 100% ya dhahabu yao Nzega mpaka walipokomba kila kitu na kuacha mashimo na maji ya sumu tu.

Kwa logic ya wazalendo wetu, hatukuibiwa Nzega kwa sababu wawekezaji hao hawakusafirisha mchanga wa dhahabu.

Acacia walishakomba kila kitu Tulawaka na kuacha mashimo na maji ya sumu. Kwa sababu tu hawakusafirisha mchanga, basi hawakuwa wezi.

Hii ni logic ya mtu asiyeelewa biashara ya uchimbaji dhahabu katika nchi hii kabisa.

Tangu tumeanza kuwakaribisha wawekezaji hawa, hatujawahi kufikisha 10% ya mapato ya kikodi kutokana na mauzo ya dhahabu yote iliyochimbwa na kuuzwa nje.

Sio kwa sababu wawekezaji walikuwa wana-underdeclare mchanga wa dhahabu, bali ni kwa sababu sheria zetu zinawaruhusu kutokulipa kodi kama hawajatangaza faida.

Ni sheria, sheria, sheria. Sio mchanga wa dhahabu. Hilo ni changa la macho tu la kufumbia wasioelewa.

Kama Magufuli ana nia njema angeanza na sheria. Hajaanza na sheria, hana nia njema.

Mnaambiwa tusiogope kushtakiwa. ******* ujinga na hao hao waliowaruhusu wageni kuchota mali zetu: akina Magufuli na CCM yao.

Tumeshalipishwa na tunaendelea kulipishwa mabilioni mengi kutokana na kesi za Richmond/Dowans, IPTL/Tegeta Escrow, City Water, Samaki wa Magufuli, n.k. kwa sababu tumekuwa tunakiuka mikataba 'kwa nia njema.'

Tumekuwa tunaingia hasara kubwa kama taifa kwa sababu za kijinga. Badala ya kukataa ujinga huu tunaushabikia kwa sababu tu umefanywa 'kwa nia njema.'

Magufuli atauachia huo mchanga wa dhahabu kwa wenyewe. Mark my words.

Hana jinsi.

Sheria yetu ya madini inasema huo mchanga ni mali yao. Na imesema hivyo tangu mwaka '98.

Mkataba wao unasema ni mali yao. Na umesema hivyo tangu mwaka 2000.

Mikataba ya kimataifa tuliyosainishwa na wenye nia njema hawa inasema mchanga ni mali ya Acacia.

Mchanga huo umehakikiwa na TRA, TMAA, GST na SGS. Zote hizi ni taasisi za Serikali hii hii na zimepewa mamlaka kisheria na kimkataba na Serikali hii hii kuhakiki mchanga huo.

Kamati ya Prof. Mruma haina mamlaka hayo. Ripoti yake haina maana yoyote kiushahidi.

Sio kupiga ramli au kuagua kusema kwamba tutapigwa asubuhi kwenye arbitral tribunals za kimataifa.

Tutawarudishia mchanga na tutawalipa hasara yote waliyopata kwa sababu ya matendo yenye nia njema lakini yasiyozingatia sheria wala busara katika mambo haya.

Tunarushiwa changa la macho lingine. Tunaambiwa kuna Kamati ya wachumi na wanasheria inaleta ripoti nyingine. Hii itakuwa Kamati ya nne tangu mwaka 2004. Tulikuwa na Kamati ya Dr. Jonas Kipokola (2004); Lau Masha (2006) na Jaji Mark Bomani (2008). Tumekuwa na taarifa lukuki za watafiti binafsi na kwa muda mrefu. Ni kitu gani hasa cha kiuchumi au kisheria ambacho hatukijui hadi sasa na ambacho kinahitaji kuundiwa Kamati nyingine??? Wajinga ndio waliwao. Mimi sio mjinga. Na sijahongwa kama hawa wanajiita wazalendo. Ninapinga na nitaendelea kupinga ujinga huu unaotupeleka kuzimu......".

Tundu Lisu
WEWE TUNDU LISSU NI MHAINI WA KIFIKRA NA HUNA UZALENDO WOWOTE: NONSENSE
 
I dont see specific issue...hapa sana sana ni blah blah tu.

Naona lissu anatamani kumeza matapishi yake ya juzi na inashindikana.
Ningeshangaa kama ungeona "specific issue", si unasubiri mpaka aone mkuu ambaye yuko tayari kufa na tai!
 
Ningeshangaa kama ungeona "specific issue", si unasubiri mpaka aone mkuu ambaye yuko tayari kufa na tai!
Mwambie atulie na kusubiri ripoti ya Tume ...halafu mwanaume achukue maamuzi.

Yaani kwa kuwa mugabe kanyooshwa kwa hiyo na sisi tuchutame tu...hii akili ya level ya Nyumbu kabisa...ingekuwa hivi watu wangeacha kupigana kwa kuangalia mtu anavyopigwa tu.
 
Mwambie atulie na kusubiri ripoti ya Tume ...halafu mwanaume achukue maamuzi.

Yaani kwa kuwa mugabe kanyooshwa kwa hiyo na sisi tuchutame tu...hii akili ya level ya Nyumbu kabisa...ingekuwa hivi watu wangeacha kupigana kwa kuangalia mtu anavyopigwa tu.
Kamsome tena kuhusu kusubiri ripoti ya tume!
 
Mataahira ya Lumumba yakitia timu hapa haki ya nani patachimbika,, yaani yaongozwe na Cocochanel, halafu Lizaboni akifuatiwa na jingalao? Sijui kama mtahimili mashambulizi!!! Ngoja mimi nikalale!!
Tatizo la fikra za level ya Nyumbu ni kuamini anayebwatabwata na kutoa matamko mengi ndio mwenye akili.

Hadi sasa sijasikia msomi aliyemchallange kisomi profesa Mruma...naona watu wanahamia topic za mrabaha na kuacha kuijadili kwa hoja ripoti ya tume.

Huyu lissu anasahau hao acacia waliwahi kunyimwa hati za uadilifu kama kampuni ya madini??
 
Back
Top Bottom