Lissu; Nia njema ya Magufuli inatupeleka pabaya

Tatizo la fikra za level ya Nyumbu ni kuamini anayebwatabwata na kutoa matamko mengi ndio mwenye akili.

Hadi sasa sijasikia msomi aliyemchallange kisomi profesa Mruma...naona watu wanahamia topic za mrabaha na kuacha kuijadili kwa hoja ripoti ya tume.

Huyu lissu anasahau hao acacia waliwahi kunyimwa hati za uadilifu kama kampuni ya madini??
Kumbe walinyimwa eeh? Nchi gani??
 
That's y siachi kumuombea maisha marefu. Japokuwa vizuri havidumu,lakini Mungu ajaribu kutusamehe na atuwachie mtu huyu kwa muda mrefu. Kwa Maana Naona kama tuna adhibiwa,kwanini Mungu anaruhusu mabaradhuli Haya kila siku yatuonee na kututesa? Basi atuwachie mtetezi huyu aliyetuletea.
Live long Tundu Lissu na wapigania haki wote,akiwemo BAK wangu. Maisha marefu kwako kaka angu.
Dada Mungu akubariki, nimekupenda bure, huyu mtu kajitoa muhanga dhidi ya majitu katili na mitekaji...ref ben 8, Mungu wa mbinguni amlinde Lisu dhidi ya wauaji wa nchi hii.
 
Dada Mungu akubariki, nimekupenda bure, huyu mtu kajitoa muhanga dhidi ya majitu katili na mitekaji...ref ben 8, Mungu wa mbinguni amlinde Lisu dhidi ya wauaji wa nchi hii.
Yeye ni shujaa wetu. Na wengine wote wanaotutafutia haki waTz wote,Mungu awabariki na awape ulinzi dhidi ya Haya mabaradhuli ya kila kona.
Tuko pamoja kaka.
 
Timu A
Mazuzu ya Lumumba

Timu B
Manyumbu ya Ufipa

Watanzania wenzangu, tumefikaje hapa? Na si ajabu kila mmoja anapigania demokrasia. Something is not right somewhere na kama tukiendelea hivi kuna giza huko mbele ya safari. Sad!
 
Yeye ni shujaa wetu. Na wengine wote wanaotutafutia haki waTz wote,Mungu awabariki na awape ulinzi dhidi ya Haya mabaradhuli ya kila kona.
Tuko pamoja kaka.
Amen dada, ninamfahamu Lisu kwa asilimia nyingi zaidi ya miaka 22 yaani tangu 1995. Ni mtetezi wa kweli, anajiamini na hatetereki hata kidogo, pia amejaaliwa mke jasiri sana ndiyo maana anapambana bila kuchoka kwani ana mtu wa kumback, Mungu awalinde
 
Timu A
Mazuzu ya Lumumba

Timu B
Manyumbu ya Ufipa

Watanzania wenzangu, tumefikaje hapa? Na si ajabu kila mmoja anapigania demokrasia. Something is not right somewhere na kama tukiendelea hivi kuna giza huko mbele ya safari. Sad!
Hii ni yanga na simba isikupe taabu, tatizo ni tukitaja ukabila, worry out ma friend
 
Mwambie atulie na kusubiri ripoti ya Tume ...halafu mwanaume achukue maamuzi.

Yaani kwa kuwa mugabe kanyooshwa kwa hiyo na sisi tuchutame tu...hii akili ya level ya Nyumbu kabisa...ingekuwa hivi watu wangeacha kupigana kwa kuangalia mtu anavyopigwa tu.
Wee kamwe huwezi kumuelewa Lissu...

Ova
 
ANAANDIKA TUNDU LISU...

Suala sio nia njema ya Rais. Suala ni consequences za hiyo nia njema. The road to hell is paved with good intentions.

Mugabe most likely alikuwa na nia njema. The consequences za nia njema hiyo ni kwamba Zimbabwe ya leo haina hata sarafu yake na imegeuka kuwa ya kuomba chakula wakati ilikuwa a major food exporter.

Kama kweli Rais Magufuli ana nia njema angeanza na mfumo mzima wa kisheria, sio kuhangaika na magwangala.

100% ya uzalishaji wa dhahabu ya Geita unafanyikia mgodini na Geita Gold Mine ni mgodi mkubwa kuliko yote nchini.

Kwa logic ya Magufuli ni kwamba GGM hawatuiibii kwa sababu tu smelting yote inafanyikia Geita.

Acacia wanayeyushia dhahabu yote ya Nyamongo mgodini Nyamongo.

Kwa logic hiyo hiyo, hawa wezi wa mchanga wa Bulyanhulu na Buzwagi hawaibi Nyamongo kwa sababu tu wanafanya kila kitu Nyamongo.

Resolute walisafisha 100% ya dhahabu yao Nzega mpaka walipokomba kila kitu na kuacha mashimo na maji ya sumu tu.

Kwa logic ya wazalendo wetu, hatukuibiwa Nzega kwa sababu wawekezaji hao hawakusafirisha mchanga wa dhahabu.

Acacia walishakomba kila kitu Tulawaka na kuacha mashimo na maji ya sumu. Kwa sababu tu hawakusafirisha mchanga, basi hawakuwa wezi.

Hii ni logic ya mtu asiyeelewa biashara ya uchimbaji dhahabu katika nchi hii kabisa.

Tangu tumeanza kuwakaribisha wawekezaji hawa, hatujawahi kufikisha 10% ya mapato ya kikodi kutokana na mauzo ya dhahabu yote iliyochimbwa na kuuzwa nje.

Sio kwa sababu wawekezaji walikuwa wana-underdeclare mchanga wa dhahabu, bali ni kwa sababu sheria zetu zinawaruhusu kutokulipa kodi kama hawajatangaza faida.

Ni sheria, sheria, sheria. Sio mchanga wa dhahabu. Hilo ni changa la macho tu la kufumbia wasioelewa.

Kama Magufuli ana nia njema angeanza na sheria. Hajaanza na sheria, hana nia njema.

Mnaambiwa tusiogope kushtakiwa. Mnatiwa ujinga na hao hao waliowaruhusu wageni kuchota mali zetu: akina Magufuli na CCM yao.

Tumeshalipishwa na tunaendelea kulipishwa mabilioni mengi kutokana na kesi za Richmond/Dowans, IPTL/Tegeta Escrow, City Water, Samaki wa Magufuli, n.k. kwa sababu tumekuwa tunakiuka mikataba 'kwa nia njema.'

Tumekuwa tunaingia hasara kubwa kama taifa kwa sababu za kijinga. Badala ya kukataa ujinga huu tunaushabikia kwa sababu tu umefanywa 'kwa nia njema.'

Magufuli atauachia huo mchanga wa dhahabu kwa wenyewe. Mark my words.

Hana jinsi.

Sheria yetu ya madini inasema huo mchanga ni mali yao. Na imesema hivyo tangu mwaka '98.

Mkataba wao unasema ni mali yao. Na umesema hivyo tangu mwaka 2000.

Mikataba ya kimataifa tuliyosainishwa na wenye nia njema hawa inasema mchanga ni mali ya Acacia.

Mchanga huo umehakikiwa na TRA, TMAA, GST na SGS. Zote hizi ni taasisi za Serikali hii hii na zimepewa mamlaka kisheria na kimkataba na Serikali hii hii kuhakiki mchanga huo.

Kamati ya Prof. Mruma haina mamlaka hayo. Ripoti yake haina maana yoyote kiushahidi.

Sio kupiga ramli au kuagua kusema kwamba tutapigwa asubuhi kwenye arbitral tribunals za kimataifa.

Tutawarudishia mchanga na tutawalipa hasara yote waliyopata kwa sababu ya matendo yenye nia njema lakini yasiyozingatia sheria wala busara katika mambo haya.

Tunarushiwa changa la macho lingine. Tunaambiwa kuna Kamati ya wachumi na wanasheria inaleta ripoti nyingine. Hii itakuwa Kamati ya nne tangu mwaka 2004. Tulikuwa na Kamati ya Dr. Jonas Kipokola (2004); Lau Masha (2006) na Jaji Mark Bomani (2008). Tumekuwa na taarifa lukuki za watafiti binafsi na kwa muda mrefu. Ni kitu gani hasa cha kiuchumi au kisheria ambacho hatukijui hadi sasa na ambacho kinahitaji kuundiwa Kamati nyingine??? Wajinga ndio waliwao. Mimi sio mjinga. Na sijahongwa kama hawa wanajiita wazalendo. Ninapinga na nitaendelea kupinga ujinga huu unaotupeleka kuzimu.....

Tundu Lisu
 
Kwa kifupi Mh. Tundu Lissu anatuasa tusiwe na tabia ya kupuuza historia iliyopo ktk makabrasha ya Tume na Tafiti za kina Dr. Jonas Kipokola (2004) , Lau Masha (2006), Tume ya Bomani (2008) n.k

Na hapa kuna la kujifunza kuwa somo la historia pia lina muingiliano wa karibu na somo la uchumi, utawala bora, kuzuia magonjwa ya mlipuko, Kemia, uhandisi na fani nyingi tu ili kuweza kujikwamua tulipokosea.

Lakini inaonekana yote tunayofanyia kazi ktk ngazi za elimu ya juu, tafiti na tume za uchunguzi au hata uzoefu-kazini huwa tunayasahau au kuyapuuza kwa makusudi au ndiyo tabia yetu na kisha kutukwamishwa kuendelea mbele kwa kupuuza umuhimu wa historia.

The Importance of History for Economic Development
The most recent studies, using microlevel data and more sophisticated identification techniques, have moved beyond testing whether history matters and attempt to identify exactly why history matters. The most commonly examined channels include institutions, culture, knowledge and technology, and movements between multiple equilibria. Source: The Importance of History for Economic Development
 
Back
Top Bottom