Lissu atia fora bungeni

kwanini wamezima kipaza sauti??? kweli nimeamini siasa ni kipaji nilivyo na hasira ningeweza kung'oa hapo hicho kipaza sauti na kila siku ningepigana huko bungeni duhh kazi buti mkuu Lissu

Da! Hatari!
 
kweli ukitaka kujua madame spika ni kiasi gani anapwaya kwenye kiti chake bas i asimame TunduLISU.
Hivi ni mara ngapi ccm wamekuwa wakihiitajam chadema kwenye hotuba zao?
 
Last edited by a moderator:
Nguvu inayotumika kumnyamazisha Lisu laiti ingetumika serikari kuhamia Dodoma Leo kusingekuwa na Foleni hapa Dsm wanapaswa wajue jinsi wanavyomwandama ndivyo wanavyozidi kumfanyia Promo waanamwongezea umaarufu zaidi .yapasa tubadilike maendeleo kwanza fitna na siasa za maji Taka baadae
 
Siku nzuri huanza asubuhi. niliposoma heading ya post yako, nilitaka kuona kama content yake inafanana na heading. I'm suprised kwamba inafanana. Leo umependeza mwanangu, nahisi magamba yanaendelea kukudondoka.

hahahaha.. Chilipamwao, mbona mimi ni gwanda ndani ya gamba!!

Ila ni vyema wana-CCM wenzangu ifike wakati tukubali tu kama kuna majembe CHADEMA, kama huyu Lissu, I'm proud of him.
 
Last edited by a moderator:
Mimi ni CCM, ila Lissu namvulia kofia, jamaa ni jembe.
HAMY-D vipi leo.Leo umeamua kuja kivingine kibisa.Kuna thread yako nyingine uloanzisha leo JF -siasa kuhusu Juliana Shonza kueleza ukweli kuhusu kuahidiwa ubunge wa viti maalum CCM,kama atakamilisha vema kazi alopewa ya kuikashifu CHADEMA.
 
hahahaha.. Chilipamwao, mbona mimi ni gwanda ndani ya gamba!!

Ila ni vyema wana-CCM wenzangu ifike wakati tukubali tu kama kuna majembe CHADEMA, kama huyu Lissu, I'm proud of him.

Kulingana na maagizo niliyopewa na Captain wa 7thou strikers team yule boss wetu wa zero brain propaganda nakutaarifu kuwa leo ni MARUFUKU kuonekana mitaa yaLumumba. Ukikaidi hilo utapambana na vijana wa Green guards chini ya kamanda wao mwenyewe Madelu madevu. Hamia hukohuko unakosifia, hujui sisi huwa tunajisifia wenyewe hata kwenye ujinga?
 
Last edited by a moderator:
lissu haoneshi usomi wake bali ujinga. ni jitu lenye kiburi, jeuri.... hadi najihisi kutapika!
 
Kutaja Neno Chama Cha mapinduzi siku hizi ni TUSI KUBWA!! ndo maana wanazima vipaza sauti! Nimeamini CCM kwisha kama neno hilo ni tusi!

Litakuwa kama lile la Seru-rope(thread)!! ha ha ha ha !! Uwiii!!
 
Hata wewe HAMY-D umeanza kuwa jasiri......maana kumpaisha Lissu ni ''kashfa'' kwa Buku Saba Dirty Inc

Sio hii tu, Hata ile ya kueleza Ahadi lukuki alizoahidiwa Mdada Mrembo aliyehama CDM na kuingia kwa Magamba.
HMY Huenda ameanza kujitambua kuwa buku 7 zinamtesa na kumnyima uhuru.
 
Lissu akiwa anatoa mchango wake kwenye muswada ulioletwa na serikali, amezimiwa kipaza sauti baada ya kukaidi maelekezo ya spika ya kuacha kukitaja chama cha Mapinduzi katika mchango wake.

Lakini Lissu ameendelea kuongea na kukitaja chama cha Mapinduzi huku kipaza sauti kikiwa kimezimwa kwa takribani kama dakika 4 mpaka kipaza sauti kilipo washwa tena, huu ni ujasiri wa ajabu.

Haya yote ni katika kuelezea jinsi alivyo funguliwa kesi ya rufani na bwana Kinana kupinga ubunge wake, pia na mapungufu mengine ya mahakama kama vile kushinikizwa na vyama vya siasa.

Hii ID leo people wamehack au , mbona sielewielewi hapa.
 
Kwa kweli huyu jamaa ana uelewa wa hali ya juu na anajua ni nini anatakiwa kuongea kabla hata hajasimama kuongea sio kama wabunge wengine ambao toka bunge linaanza mpaka linaisha wao ni kupongezaa upuuzi na kugonga meza mpaka mikono imeota sugu....wapo wengi ambao wakisimama kuchangia hoja yoyote hata kama ulikua na shughuli zako utaacha na kuwasikiliza....kama vile...Deo filikunjombe(CCM)...mkosamali(NCCR),Kafulila(NCCR) na wote wa CDM....
 
Back
Top Bottom