Lissu atia fora bungeni

Ukweli ni kwamba Lissu hana chochote zaidi ya kucheza na lugha, nimeshawahi sema tena humu. Lisu ni mjanja katika maneno na siyo katika hoja. na siku zote wajenga hoja hawapendwi. Watu tunashadaia sana mbunge anaposimama na kunena mabaya juu ya chama fulani iwe kwa ukweli ama uongo. Lisu kama mwanaharakati na siyo mwanasiasa lazima aongee kwa style hiyo ni kama ilivyo kwa wengine wengi tu tunaowajua. Kwa mfano Lipumba pale Msikitini (ingawa inasemekana Nchemba ndiyo aliitengeneza Video hiyo) alikuwa anaongea yasiyo mema lakini waliokuwepo pale walikua wanashangilia na kumuona shujaa.

Msimamo wangu utabaki palepale kuwa Lisu no mchezea maneno, populist, mpenda kuonewa huruma na asiweza kusimama mwenyewe kwenye siasa bila kivuli cha mtu mwingine (nacho kwa sasa ni CCM).

We gamba ni lini lissu kashindwa hoja?
Siku zote ccm ndio hawana hoja dhaidi yaku yakucheza na maneno na kutulaghai kwa maneno ambayo sasa tushayazoea kuwa ni uzushi na uongo mtupu.
 
Lissu ni sawa na wabunge 150 wa ccm, kiakili, Personality, Kiuchambuzi ...hebu nitajie mbunge yoyote wa ccm anaemkaribia uwezo huyo jamaa

Hakuna hata mmoja kiukweli labda waanze leo kuacha unafki wao kama Filikonjombe kaanza kuacha unafiki na kuwa mmbunge huru.
 
Hata wewe HAMY-D umeanza kuwa jasiri......maana kumpaisha Lissu ni ''kashfa'' kwa Buku Saba Dirty Inc


Nilishangaa sana kwa huyu Hammy-D kuandika posivtively kuhusiana na Lisu ikabidi nijiulize mara kadhaa, Huyu jamaa ameongoka au? Nasema hivyo kwa sijawahi kumsoma hata akiwa kwenye mtazamo wa kati. Sasa kama kavunja masharti ya buku 7 itakuwaje? Au petty cash imeisha na kwa maana hiyo atalipwa baada ya kubwabwanya? If that is tha case, kwa hili hatalipwa. Amekiuka makubaliano.
 
Namuonea huruma sana bi Kiroboto, kati ya wanaccm walioipotezea ccm umaarufu kwa kiwango kikubwa ni Viongozi was bunge. Wamekuwa wakionyesha Udhaifu wa wazi kiasi wananchi wanajenga hasira na maamuzi yanayofanywa na viongozi hao.
Kuipa ccm adhabu itakayo waadabisha ni Kusema hapana ccm kwenye sandukua Kura.
Na hilo wameshaliona ndio maana wameanza kulalamikia rasimu ya katiba yenye mawazo ya wananchi sasa wanataka itungwe katiba inayoibeba ccm. Tuseme HAPANA katiba ni ya Watanzania sio ya ccm

Niliwahi kuandika humu JF kuwa uongozi wa Bunge hili la sasa ndiyo ulipelekea wananchi kupendekeza spika na msaidizi wake wasitokane na wabunge kitu ambacho ni tofauti na mabunge mengi ya kidemokrasia. Unapochaguliwa kuwa spika unatakiwa utende haki uachane na mapenzi ya chama chako. Hawa hawakuwa hivi na watu waliyaona haya na kupendekeza yaliyotolewa kwenye Rasmu. Hivi kweli Spika anatarajia mshindani akiseme vizuri Chama tawala na vilevile mbunge wa Chama tawala akisifu Chama shindani bungeni? Wanaangaika kuzuia vitu ambavyo watu wanavijua.
 
ccm wajinga sana kama wamefanya vibaya wanategemea atatajwa na nani makinda ana akili za kuku
 
Hata wewe HAMY-D umeanza kuwa jasiri......maana kumpaisha Lissu ni ''kashfa'' kwa Buku Saba Dirty Inc

Pamoja na kwamba leo Ame dominate Jf, hata kwa thread za kizushi , lakini kwa hili la kumpaisha Tundu Lissu ,nasikitika kusema kwamba amepoteza haki zake zote pale ofisi ndogo Lumumba !
 
Tungekuwa na Wabunge kama Lissu Tanzania isingekuwa shamba la bibi yaani tungekuwa mbele sana bila ya ushabiki wowote Mh Tundu Lissu kamaliza yeye ni zaidi ya Caterpillar ni mtu ambaye ni jasiri sana haogopi mtu yeyeto na nakiongea anamaanisha anachoongea na ni cha ukweli mtupu,Kusema kweli huyu jamaa ana kipaji cha Uongozi ndio maana hata Jakaya Mrisho Kikwete alisema bora Dr Wilbroad Peter Slaa kuwa Rais kuliko Mh Tundu Lissu kuwa Mbunge aliona ati maake jamaa ni balaa.Big up kamanda Lissu na Chadema kwa ujumla.''Zambi iliyokubwa kuliko zote ni woga''by GodBless Jonathan Lema.
 
karibu nyumbani kijana your in gud me and cdm in general..cdm sio lissu tu ..zipo machine tu..
 
Kinana lazima awe na chuki binafsi dhidi ya Lisu, Lisu ndiye anayempa jeuri Mh Msigwa kushambulia biashara zake za meno ya tembo
 
Daa, kwa namba hiyo ni hatariiii
Japo Mimi sio mchadema, lkn ndani ya mjengo wa bunge napenda sana kumsikiliza tundu lissu anapotoa Hotuba. Nafikiri kwa sasa yeye ndie messi wa bunge linapokuja suala la kujenga hoja!
 
Japo Mimi sio mchadema, lkn ndani ya mjengo wa bunge napenda sana kumsikiliza tundu lissu anapotoa Hotuba. Nafikiri kwa sasa yeye ndie messi wa bunge linapokuja suala la kujenga hoja!
Ronaldo akiwa JJ Mnyika.
 
Back
Top Bottom