Lissu atia fora bungeni

Lissu atia fora bungeni

Lissu ni sawa na wabunge 150 wa ccm, kiakili, Personality, Kiuchambuzi ...hebu nitajie mbunge yoyote wa ccm anaemkaribia uwezo huyo jamaa

Kapitein John Komba au hata Livingstone Lusinde aka Kibajaji.Ah ni mtazamo tu mi niko nalala.
 
Lissu uko juu ni mwanaharakati wa ukweli, keep on we are with you................, huyo bibiye yuko kichama zaidi ndio maana hataki utaje chama cha magamba
 
Mpaka kieleweke kamanda wetu wamukizimia kipasa sauti wakashindwa kukuzimia sauti aliyokupa mungu watashindwa daima
 
Naomba Mungu siku wakimzimia LISU tena kipaza sauti wpate kiharusi hapo hapo.....IKITOKEA HIYO hawatarudia tena....nanai atakubali kupata kiharusi?!!!
 
Lissu akiwa anatoa mchango wake kwenye muswada ulioletwa na serikali, amezimiwa kipaza sauti baada ya kukaidi maelekezo ya spika ya kuacha kukitaja chama cha Mapinduzi katika mchango wake.

Lakini Lissu ameendelea kuongea na kukitaja chama cha Mapinduzi huku kipaza sauti kikiwa kimezimwa kwa takribani kama dakika 4 mpaka kipaza sauti kilipo washwa tena, huu ni ujasiri wa ajabu.

Haya yote ni katika kuelezea jinsi alivyo funguliwa kesi ya rufani na bwana Kinana kupinga ubunge wake, pia na mapungufu mengine ya mahakama kama vile kushinikizwa na vyama vya siasa.
Kwa taarifa tu Lissu hajaanza ujasiri leo. 1996 ndiye aliye toa siri za kufukiwa wachimbaji wadogowadogo na mwekezaji kwa AMRI ZA CCM kule BULYANHULU. Watu walifukiwa na makatapila ya mwekezaji mzungu mpaka leo hii hakuna tamko lolote. Tundu Lissu innawezekana ni mwema sana kuliko anavyoonekana. Mungu awabariki wapigania haki na uhuru wote.
 
Back
Top Bottom