Viongozi wawe makini sana, na ofisi ya DPP isimame kwenye maadili. Kuwashtaki watu kwa kosa kubwa kama la uaini kijinga kijinga hivi ni kufanya hili kosa lionekane la kawaida sana.
Hii nchi ukiona watu wana vichwa vikubwa, suti kubwa na wanapiga makelele huko barabarani wakitaka kupishwa unaweza kudhani wanafikiri sawa sawa.
Hoja zinajibiwa kwa hoja, hakuna namna nyingine ya kujibu hoja. Mwenyekiti wa CCM atafute watu smart wanaoweza kujenga hoja awape nafasi. Hii tabia ya kuteua kwa kuangalia nani anasifu zaidi na nani anavaa sana kofisa zenye picha ndio haya sasa unakuja kutumia uhaini kujibu hoja za kisiasa.