Wanapima upepo, saizi wako katika mikakati ya kuirudisha imani ya wananchi ambayo imepotea.
Ndio maana unaona hizi pesa zina mwagwa kwa hawa wanaoitwa kontenti krieata.
Tafsiri yake kwa sasa hawako tayari kuona mtu mwingine ambaye yupo kinyume na serikali aliye na ushawishi na mwenye kuaminika kwa wananchi, apate fursa ya kuongea lolote kuhusu serikali.
Japo naona pia kwa upande mwingine kuna pressure serikali inaipata kutoka nchi za kimataifa ikiwemo swala la vikwazo kutokana na hii kesi ya Lissu.
Sasa hapo ni kinachofuata ni calculation of the risk.
Kama upande wa serikali utaona ni risk sana kumuacha Lissu huru katika hiki kipindi ambacho ina struggle kurudisha imani kuliko risk za vikwazo ambavyo tutawekewa, basi siwezi kushangaa kuona danadana Mahakamani.